Notification texts go here Contact Us Buy Now!

NGUMU KUMEZA; (18+) Sehemu ya 07- Muandishi: Jclassic boy (Next level Author)

ILIPOISHIA “Dany tafadhali nakuomba uo……” Mery alinyamaza gafla huku macho yakitazama kwenye lifti, nikageuka na kumuona Mose akitoka kwenye lifti hizo, akanitazama kwa macho makali huku akinifwata nilipo simama. “Wewe mwana haramu umekuja hadi huku si ndio” Mose alizungumza na kutaka kuniparamia, ila safari hii sikuhitaji kuwa fala tena kwa maana, kitendo cha kunisogelea nikamuwasha ngumi sita za kasi zilizo tua katika sura yake na kumfanya ayumbe na kuanguka chini. Kila mtu aliye kuwa katika eneo hilo akashangaa. Mose akaanza kujizoa zoa na kunyanyuka, akasimama wima japo kwa kuyumba, akajaribu kurusha ngumi ila zote nilizikwepa, nikamtisha kidogo aniachia sura, nikavuta ngumi moja kali kabla haijafika karibu na shingo yake nikauzuia mkono. “Usirudie tena” Mose alicho kikosea ni kunitukania mama yangu, hapo sasa nikaweka ustaarabu pembeni na kuanza kumtembezea kichapo, hadi walinzi wanao linda eneo hilo wakaja kunikamata. Nikiwa katika kizuizi cha walinzi hao nikashangaa kuona gari ya polisi ikija eneo hilo. “Mtuhumiwa mwenyewe huyu hapa” Alizungumza mzee mmoja aliye valia suti ya kaki. Askari hao wakanisogelea wakiwa na bunduki zao. “Nyoosha mikono, una haki ya kukaa kimya hadi pale utakapo fika kituoni kwa mahojiano” Sikuwa mbishi, wakanifunga pingu za mikononi na kunipakiza kwenye gari lao na kuondoka eneo hilo. “Afande ninaomba nimpigie mwanasheria wangu aje kituoni?” Nilizungumza tukiwa njiani. Askari huyo hakuweza kunijibu chochote zaidi ya kunikata jicho baya. Tukafika kituo cha polisi. Wakanifungua pingu, wakaniamuru kuvua mkanda, viatu, kutoa waleti mfukoni. Nikafanya hivyo kitu lilicho mstusha askari aliye kuwa akinipapasa ni bastola yangu niliyo kuwa nimeichomeka kiunoni. “Jamani huyu ni jambazi” Askari huyo alizungumza kwa sauti ya juu na kuwafanya askari wengine wote kituoni kunitazama mimi huku wengine walio na bunduki kuninyooshea mimi, huku wakiniamuru kunyoosha mikono juu kwa ukali sana. ENDELEA

NGUMU KUMEZA SEHEMU YA 07

SIMULIZI HII NI KWA WASOMAJI WENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 18.
ILIPOISHIA
“Dany tafadhali nakuomba uo……”
 Mery alinyamaza gafla huku macho yakitazama
kwenye lifti, nikageuka na kumuona Mose akitoka
kwenye lifti hizo, akanitazama kwa macho makali
huku akinifwata nilipo simama.
“Wewe mwana haramu umekuja hadi huku si ndio”
Mose alizungumza na kutaka kuniparamia, ila
 safari hii sikuhitaji kuwa fala tena kwa maana,
kitendo cha kunisogelea nikamuwasha ngumi sita za
 kasi zilizo tua katika sura yake na kumfanya
ayumbe na kuanguka chini.
 Kila mtu aliye kuwa katika eneo hilo akashangaa.
 Mose akaanza kujizoa zoa na kunyanyuka,
 akasimama wima japo kwa kuyumba, akajaribu
kurusha ngumi ila zote nilizikwepa, nikamtisha
 kidogo aniachia sura, nikavuta ngumi moja kali
kabla haijafika karibu na shingo yake nikauzuia
mkono.

“Usirudie tena”
Mose alicho kikosea ni kunitukania mama yangu,
 hapo sasa nikaweka ustaarabu pembeni na kuanza
kumtembezea kichapo, hadi walinzi wanao linda
eneo hilo wakaja kunikamata. Nikiwa katika kizuizi
 cha walinzi hao nikashangaa kuona gari ya polisi
 ikija eneo hilo.
 “Mtuhumiwa mwenyewe huyu hapa”
 Alizungumza mzee mmoja aliye valia suti ya kaki.
Askari hao wakanisogelea wakiwa na bunduki zao.
“Nyoosha mikono, una haki ya kukaa kimya hadi
 pale utakapo fika kituoni kwa mahojiano”
Sikuwa mbishi, wakanifunga pingu za mikononi na
kunipakiza kwenye gari lao na kuondoka eneo hilo.

“Afande ninaomba nimpigie mwanasheria wangu
 aje kituoni?” Nilizungumza tukiwa njiani. Askari huyo hakuweza
kunijibu chochote zaidi ya kunikata jicho baya.
 Tukafika kituo cha polisi. Wakanifungua pingu,
wakaniamuru kuvua mkanda, viatu, kutoa waleti
 mfukoni. Nikafanya hivyo kitu lilicho mstusha
askari aliye kuwa akinipapasa ni bastola yangu
niliyo kuwa nimeichomeka kiunoni.
“Jamani huyu ni jambazi”
Askari huyo alizungumza kwa sauti ya juu na
kuwafanya askari wengine wote kituoni kunitazama
mimi huku wengine walio na bunduki
 kuninyooshea mimi, huku wakiniamuru kunyoosha
mikono juu kwa ukali sana.


ENDELEA
Nikafwata kama wanavyo hitaji, nikainyoosha
 mikono yangu juu huku nikimtazama askari aliye
nichomoa bastola yangu.
“Piga magoti wewe mjinga”
Askari mwengine alisisitiza kwa sauti ya ukali,
 taratibu nikapiga magoti. Askari huyo akachukua waleti yangu na kuifungua, akaanza kuikagua
 vitambulisho vyangu. Nikamuona akistuka baada
ya kutoa kitambulisho changu cha kazi.
 Akanitazama mara mbili mbili huku macho
 yakimtoka na jasho likimwagika.
 “Kuna nini kinacho endelea hapa”
Nilisikia sauti ya kike, nyuma yangu. Ikanibidi
 kugeuka na kumkuta mkuu wa polisi ambaye
ninamtambua ni rafiki wa karibu sana na K2 na
 mara nyingi niliweza kumuona akija ofisini kwetu.

“Mkuu kuna huyu kijana alifanya fujo, ndio
 tumemleta hapa kituoni”
 Mwanamama huyo mrefu kwenda juu, aliye valia
 suruali ya kaki pamoja na shati la kaki, lenye nyota
kadhaa kwenye bega lake, akazunguka na kuja
 kusimama mbele yangu.
 “Mumegundua nini?”
Alimuuliza askari aliye shika kitambulisho changu.
Askari huyo akaonekana kupata kigugumizi na
kujikuta mkuu wake akikichukua kitambulisho
hicho na kukisoma. Akanitazama kwa haraka kisha
 akayarudisha macho yake kwenye kitambulisho
hicho.

“Nani aliwapa amri ya kwenda kumkamata?”
Askari wote wakaka kimya. Kila mmoja alimtazama
mwenzake, mwanamama huyo kwa ishara
akaniomba ninyanyuke juu. Nikanyanyuka na
kuwafanya askari wote kuduwaa.
“Mrudishieni kila kitu chake, unatoa toa macho ya
 nini?”
 Askari aliye chukua waleti na bastola yangu,
akanirudishia huku mwili mzima ukimtetemeka.
 Sikulijali juu ya woga wake nikachukua kila kitu changu,
nikavaa mkanda pamoja na viatu vyangu.
“Samahani kijana, naomba tukayazungumze ofisini
kwangu”
Mwana mama huyo alizungumza huku
akinitazama. Nilipo maliza kufunga kamba za viatu
 vyangu, nikaongozana naye hadi kwenye ofisi yake
 iliyopo gorofani.

Akanikaribisha kwenye kiti
kilichopo mbele ya meza yake kisha yeye akakaa
kwenye kiti kilichopo nyuma ya meza yake hiyo
 yenye mafaili mengi pamoja na
simu ya upepo.
 “Samahani kwa usumbufu wa vijana wangu, naona
 walikuchukua pasipo kujua kwamba wewe ni nani”
 “Kwa hilo halina tabu, ni vyema nikaondoka na
kwenda kuripoti kazini kwangu kwamba kazi yangu
ilizuiwa na vijana wako”
 “Hapana hapana, wachukulie ni vijana wenzako
wale. Endapo wataingia kwenye tabu wengine ndio
kwanza hata pesa ya serikali hawajaitafuna”
“Kwa hiyo na mimi nikafukuzwe kazi kwa ajili ya
 vijana wako, unatambua kabisa kazi yangu ilivyo
 na uhatari wa hali ya juu, ila bado vijana wako
wakaamua kuniharibia ndio nini sasa”
Nilizungumza kwa kumkoromea mama huyo baada
ya kugundua ameingiwa na hofu kidogo.

“Basi ngoja naweza kuzungumza na bosi wako, ili
 kukukingia kifua, si unajua tena sote sisi ni
watumishi wa umma na kazi yetu ni moja”
Mama huyo alizungumza huku akichomoa simu
yake aina ya Samsung Galaxy note 3. Akaminya
minya baadhi ya namba ambazo sikuziona na
kuiweka simu yake sikioni huku akinitazama usoni.
“Shosti vipi?”
 “Safi vipi”
 Kutokana na simu hiyo kuwa na sauti kubwa
kidogo niliweza kuisikia sauti ya K2, nikatamani
 kumpokonya simu mama huyo ila nikajikuta
nikishindwa na kubaki nikiwa nimemkazia macho.

“Safi tu, bwana nina ombi moja”
‘Ombi gani?"
“Kuna kijana wako hapa alikamatwa na vijana
 wangu akiwa kwenye kazi yake wakidai alifanya
 vurugu kwenye moja ya ofisi sasa nikaona
nikujulishe mapema isije akaja huko ukamuwajibisha”
 ‘Anaitwa nani?’
“Anaitwa Daniel Thamson Kajenge”
‘Mmmmm’
“Mbona unaguna sasa?”
 ‘Hapana, upo naye hapo au amesha ondoka?’
“Nipo naye hapa ofisini kwangu”
‘Hembu mpatie simu’
Mama huyo akanipatia simu yake, taratibu
nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Hallo”
“Hivi Dany unachanganyikiwa siku hizi?”
 K2 alizungumza kwa ukali na kunifanya nimtazame
mama huyu kwa jicho la kuiba nikagundua
 anayafwatilia mazungumzo yangu kwa umakini.

“Hapana mkuu”
 “Ni kitu gani kilicho kupeleka huko kituoni. Mbona
 unafanya kazi zako kipuuzi kama sio professional
aliye fuzu mafunzo eheee?”
“Hapana mkuu haito jitokeza tena”
 “Au unahisi kukupa kum* yangu ndio kunakufanya
uwe unakuwa mbovu kwenye kazi, mbona hapo
 nyuma ulikuwa unafanya kazi zako kwa umakini
eheee?”
 K2 alizidi kunifokea hadi mama huyo nikaamini
anayasikia mazungumzo hayo. Nikaka kimya kwani
 sikujua cha kumjibu K2 ambaye tangu asubuhi
alisha nivuruga.
“Sasa hiyo ripoti hadi inafika kesho saa moja
asubuhi ninaihitaji ofisini kwangu. Sasa wewe kaa
kaa na kuwaza kum* na mku*** wangu uone
mwisho wake utakuwa ni nini. Utavuna upuuzi
 wako huo”
Simu ikakatwa, nikaishusha taratibu sikioni
 mwangu na kumkabidhi mwana mama huyo aliye
baki akiwa amenikodolea macho.

“Hivi nilicho kisikia ni kweli au……?”
 Mwana mama huyo alizungumza huku akiendelea
kunikodolea macho yake. Sikuwa na kitu cha
kumjibu zaidi ya kukaa kimya.
 “Nakuomba niondoke tafadhali”
 “Sawa unaweza kwenda”
Nikanyanyuka na kumuacha mwana mama huyo
 akinisindikiza kwa macho hadi natoka ofisini
 mwake. Nikashuka kwenye ngazi na kukutana na
 askari aliye kuwa akisoma kitambulisho changu
 cha kazi. Sikumsemesha kitu zaidi ya kumpita.
 Nikapita mapokezi kila askari akabaki akiwa
amenikodolea macho. Moja kwa moja nikatoka
kituoni. Kusema kweli akili yangu haikuwaza
 chohote zaidi ya kurudi nyumbani kwangu.

“Bosi nikupeleke wapi?”
Dereva mmoja wa pikipiki alisimama pembeni
 yangu huku akinitazama. Taratibu nikajikuta
 nikipanda pikipiki hiyo.
“Nipeleke Sinza kwa Remy”
 “Sawa mkuu”
 Dereva huyo mwenye pikipiki aina ya boksa
akaanza safari. Hadi tunafika maeneo ya Sinza
ndipo nikaanza kumuelekeza hadi mtaa ninao kaa.
 Nikamlipa kiasi alicho nitajia na kuingia ndani.
 Nikamkuta Mariam akiwa amekaa kwenye kibaraza
anasikiliza miziki kwenye simu yake. Nikampita
 bila salamu, na kwa jinsi shati langu lilivyo katika
vifungo nahisi aliweza kujiuliza maswali.
 Nikakatiza kwenye korido na kukutana na Asma
 akiwa anatoka kuoga, huku amejifunga tenga moja
 tu.

“Dany mambo?”
 Asma alinisalimia huku akiwa na tabasamu pana
 usoni mwake.
 “Poa za kushinda?”
“Salama”
Sikutaka kukenua kenua meno, nikafika mlangoni
 mwangu. Nikafungua mlango na kuingia, nikaanza
 kuvua nguo moja baada ya nyingine hadi
nikabakiwa na boksa. Nikawasha feni na kujitupa
 kitandani, kila nikiwaza jinsi ya kuifanya kazi niliyo
pewa na ofisi nikajiona nimevuruga mpangilio
mzima.
 “Ohooo Mungu wangu nisaidie”
Nilizungumza huku nikiwa nimetizama juu. Sikuwa
na jibu la uhakika wa nini nifanye. Mazingira ya
chumba changu nilivyo yaacha asubuhi kwa muda
 huu hayaniridhishi kabisa.

Nikaanza kufanya usafi
wa kubadilisha mashuka na kuweka shuka jengine,
nilipo maliza hapo nikahamia kwenye kufagia na
kufuta futa vumbi kwenye meza ya Tv pamoja na
redio yangu. Sikuishia hapo nikavaa pensi na
 tisheti nikatoka nje nikiwa na ndoo ndogo nikakinga
 maji nusu na kurudi nayo chumbani kwangu na
kuanza kudeki kila sehemu.
Nikamaliza kufanya usafi wangu huo, nikachukua
 nguo zangu zote chafu na kutoka nazo nje, nikiwa
 nimeziweka kwenye dishi langu. Nikaanza kufua,
nikiwa ninaendelea kufua Asma akatoka akiwa
amevalia suruali iliyo mbana makalio yake
 makubwa.

“Nakuona leo umeamua kuwa dobi”
“Yaa kidogo dogo si unajua maisha ya ubachela”
“Kweli ila unabidi ufanya uoe Dany, kazi ndogo
 ndogo kama hizo za kufua zitakuondokea”
 “Ni kweli ila bado nipo nipo kwanza si unajua
 wanawake wa sasa ni pasua vichwa na wengine
hatupendi mambo hayo ya kuumizwa kichwa”
Asma akachukua kigoda kilichopo eneo hilo la
uwani ambapo kuna jiko la wa mama wa kupikia.
Akakaa pembeni ya tanki kubwa la maji lililopo
hapa nyumani kwetu.

“Ni kweli, lakini kwa sasa hata wanaume
 munapasua vichwa. Wanawake wanawapenda ila
hampendeki sijui kwa nini?”
 “Sio wote. Hivi jana ilikuwaje kwa juma kwa
maana ninaona alitaka kukua kwa kisu?”
“Yaani Dany kaka yangu mimi nimesha jichokea.
Mwanaume hapendeki, mwanaume ana wivu
nashindwa hata nimfananishe na kitu gani. Yaani
unavyo niona hapa hata kwenda kwa majirani
hataki. Kila kitu amenunua na kuweka ndani, ni
mimi na Tv na Tv na mimi, nikichoka ni kulala tu”
“Kwa nini anakuwa hivyo, hakuamini au?”
 “Kigezo chake kwamba mimi ni mzuri kwa hiyo
 nikitoka nje watu wataniiba”
“Hahaaa sasa jana ilikuwaje hadi akakupiga?”
 “Jana unajua kisa cha kupigwa ni kwamba.
 Tulikuwa tunaangalia myereka ya kina Jonh Cena,
 sasa mimi nikasema John Cena ni mzuri ana kifua
 kikubwa, basi hapo ndipo ugomvi ukaanza.
 Akaanza kusema ooooh sijui umalaya umezidi hadi
ninawasifia wanaume kwenye Tv ooooh kimepanda
kimeshuka. Sasa nikawa ninamjibu mwenzangu
kama ninamtania kumbe akachukulia serious, ndio
akaanza kunipiga na kutaka kunichoma na kisu”

Mazungumzo ya Asma yakanifanya nicheke na
kujikuta hata mawazo ya kazini kwangu yakikaa
 pembeni kwa maana katika maisha yangu
 sikuwahi kuona wivu wa namna hiyo.
“Yupo wapi sasa mume wako?”
“Kasafiri kaenda Arusha, kapeleka mzigo wa
mafuta”
 “Mzigo wa mafuta?”
 “Ndio mume wangu ni dereva wa magari makubwa
 yale ya mafuta, siku nyingine hupeleka mafuta
Rwanda, Burudi, Congo”
 “Ahaaa, sasa jana ulivyo rudi chumbani
hakukoroma?”
“Wee ana ubavu, akikoroma tu namwambia
ninakuja kukugongea basi anakaa kimya”
 Nikamaliza kusuuza nguo zangu, Asma akaniomba
kunisaidia kwenda kuzianika. Sikuwa na hiyana
nikamuachia kindoo nilicho jaza nguo hizo na
mimi nikamalizia kuyafua mashuka yangu.

“Asante mwaya”
 “Usijali kaka yangu, sasa ngoja mimi niandae
 chakula cha usiku”
 “Nihesabu basi”
“Usijali, ila unakula ndizi nyama wewe”
“Ahaa hapo mbona umenifikisha”
 “Basi ngoja niandae chap chap, si unajua muda
 umesonga”
 “Poa”
 Asma akaondoka na kuniacha nikiwa ninasuuza
mashuka yangu. Nikamaliza shughuli hiyo na
 kuzunguka nyuma ya nyumba kwenye kamba za
kuanikia nguo, nikaanika mashuka yangu na kurudi
sehemu nilipo kuwa ninafulia. Nikamwaga maji ya
mapovu chooni na kuanza kuyasuuza mabeseni
hayo.

“Nani amemwaga maji ya mapovu chooni?”
 Mariam alizungumza huku akinitazama usoni,
 nikatambua analifahamu jibu lake, ila anatafuta
mbinu za kuzungumza na mimi. Sikujibu chochote
zaidi ya kubeba mabeseni yangu yote na kurudi
 nayo chumbani kwangu. Nikayaweka chini ya
 uvungu na kujitupa kwenye sofa.
“K2 mamae ipo siku nitakuonyesha kwamba mimi
 mtoto wa mbwa”
 Nilijikuta nikizungumza mazungumzo hayo huku
 nikikagua namba zilizo piga kwenye simu yangu
kipindi nikiwa nipo nje ninafua, na namba ya K2 ni
 moja wapo.
 ‘Huyu ataniletea chakula kweli, au ana nizingua?’
Nilijiuliza swali hilo huku nikiwasha Tv kufwatilia
taarifa ya habari ya saa mbili usiku inayo rushwa
na kituo cha ITV.
 Hadi taarifa ya habari inamalizika saa tatu kasoro
Asma hakuleta chakula chochote. Nikataka
 kunyanyuka kwenye sofa ili nijiandae kwenda
 kununua chakula ila, mlango wangu ukagongwa.

“Nani?”
“Mimi”
Nikasikia sauti ya Asma, kwa haraka nikanyuka na
kwenda kufungua mlango. Nikamkuta akiwa
amesimama huku mkononi mwake ameshika
 ‘hotpot’ kubwa pamoja na sahani isiyo na chakula.
 “Karibu ndani, si vyema kupeana chakula
 mlangoni”
 Asma akatabasamu na kuingia ndani. Moja kwa
moja akaelekea mezani na kuweka ‘hotpot’ hilo
mezani pamoja na sahani hiyo.
“Chumba chako umekipangilia vizuri, unaweza
 kusema unaishi na mwanamke”
 “Unajua usafi mimi nilifundishwa tangu kipindi nipo
 sekondari ya bweni, kwa hiyo nimekulia kwenye
 mazingira ya usafi safi hadi hapa nilipo”
 “Kweli Dany, kuna wanaume ukiingia vyumba vyao
 utatamani kukimbia kwa manaa vimepangiliwa
vibaya kama stoo”
 Asma alizungumza huku akipakua chakula hicho,
kinacho nukia vizuri hadi nikajikuta utumbo wangu
ukitetemeka kwa njaa na hamu ya kula chakula
 hicho.

“Oooho nimesahau kijiko”
 “Usijali vijiko ninavyo”
 “Umeviweka wapi?”
Nikamuonyesha kiji trei cha kuwekea vyombo,
akachukua kijiko kimoja na kuja kukiweka kwenye
sahani ya chakula. Kabla hatujazungumza chochote
sote wawili tukaisikia sauti ya Juma huko nje.
 “Mariam umemuona wapo Asma?”
Nikamuona Asma akihisi kuishiwa nguvu, kutoka
chumbani kwangu akiwa anatamani kutoka ila
anashindwa atatoka vipi kwa maana chumba
 changu ndio cha kwanza kabisa kwa upande wa
 uwani isitoshe endapo atatoka na kukutana na
mume wake basi inaweza kuzuka kesi nyingine ya
kufikiriana vibaya. ITAENDELEA



SIMULIZI HII NI KWA WASOMAJI WENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 18. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA. USIKOSE SEHEMU YA 08 YA KISA HICHI CHA KUSISIMUA. INAPATIKANA PIA KWENYE GROUP ZA WHATSAPP NA FACEBOOK.


NGUMU KUMEZA; (18+)    Sehemu ya 07-   Muandishi: Jclassic boy (Next level Author)





Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.