Notification texts go here Contact Us Buy Now!

UTAMU WA MAMDOGO SEHEMU YA 01

MTUNZI: Geofrey Mustafa, Artist Jafa.
Mahali: Ubungo Riverside, DSM
WhatsApp: 0713024247. Umri__+

               
"KISA NA MAJINA SIO KWELI NI STORY TU"


**SEHEMU YA KWANZA**.


Naitwa Tizo Mtindo nimezaliwa mkoani TABORA wilaya ya urambo kijiji cha Mpunze elimu ya msingi niliipata hapo hapo katika kijiji chetu cha mpunze, mwaka 2003 Baba aliona tumbako imeshuka sana bei kuliko gharama za uandaaji wake maana lazima uchukue mbolea za luzuku na madawa bado inabidi uwalipe wafanya kazi wako pesa ya msimu mzima, alafu Pesa zenyewe hazifiki kwa muda muafaka. Akajaribu kutundika mizinga ili tujaribu kuuza asali, lakini bado mahitaji yalikuwa ni makubwa kuliko kipato ambacho tunapata tukiuza iyo asali.
 Basi baba akamkabidhi familia Mama pamoja na wajomba zangu, kisha yeye akaondoka zake kuelekea mkoani morogoro kutafuta maisha maana alipata sifa ya uzuri wa mkoa wa morogoro kwa kilimo akaona bora afike kabisa.

Kwa bahati nzuri mwaka uo huo wa 2003 tukaama mkoani TABORA nakuamia morogoro katika wilaya ya Kilombero kijiji cha Mbingu kata ya Igima, Baba aliuza kila kitu kuanzia Nyumba na vinginevyo vyote, tulipofika tu morogoro tulifurahi maana ilikuwa ni nchi yenye kupendeza nchi yenye kijani kibichi nchi yenye matunda na ndizi zakutosha kwa Mara ya kwanza tukiwa bado tupo Tazara nilishuudia fungu au chani moja la ndizi mbivu likiuzwa Tsh: 200.! Ndizi kubwa na zimeiva vizuri kabisa....Niliishangaa safi ya milima ya Udizunga jinsi inavyo tiririsha maji kama Juggle au Paradise vile, ilikuwa inavutia kwakweli na ni ajabu sana....maana maji yanatoka mlimani juu kabisa hayakatiki...aisee so amazing..!!

Basi baada ya miaka kadhaa kupita baba alijenga Nyumba kubwa Sana tu na tulikuwa tukilima mashamba makubwa makubwa kuanzia heka 10 nakuendelea za mpunga maisha yalibadilika sana tena sana. Basi Baba aliamua kuwapa taarifa za iyo neema    nakuwashawishi kabisa ndugu zetu wangine waamie morogoro huku akiwaambia waachane na kilimo cha biashara ya tumbako ambazo wanunuzi wasipokuja inakuwa ni hasara kubwa Sana sababu tumbako sio Chakula huwezi kula zaidi yakuzishangaa tu. Kwaiyo waje morogoro kuna kila aina ya kilimo na ardhi haichaguo mmea ata ukipanda mguu wako unaota, wee fikiri mpunga unavunywa Mara mbili ndani ya msimu mmoja yani mwezi wa 3 na 6.
Basi walikuja wajomba zangu watatu na familia zako kisha tukawapokea hapo nyumbani tulipofika wapuzike ndio watafute Nyumba yao. Walikuja wengi sana kumfuata Baba isipokuwa alibaki mmoja tu bamdogo Erasto ambaye alikuwa anasubiri afunge ndoa na mchumba wake wa muda mlefu Mamdogo wangu mtarajiwa anayeitwa Sakina.
Basi baada ya wiki moja wakawa tayari wamefunga ndoa huko matwiga kijijini kwao Mamdogo Sakina kunakoitwa Majojoro.

Basi siku ya ijumaa saa mbili usiku tulienda kumsubiria bamdogo Erasto Tazara wakitokea mbeya maana usafiri mkubwa wakufika hapa Mbingu ilikuwa ni Trein tu, vinginevyo mpaka uzungukie mikumi uje mpaka Ifakara uchukue Noah au Trector ndio ufike Mbingu mngeta chita na mlimba. Sasa watu ili kukwepa gharama iyo na mzunguko ndio wanaamuaga kupanda treni tu toka mbeya moja kwa moja hadi hapa Mbingu. Basi ilipofika saa tatu kasoro trein aina Express ikawa imewasili Station ya Tazara hapa Mbingu.
"Hii treni ni Mali ya wazambia na safari zake ni Tanzania to Zambia inaishia huko kampliposhi sasa ipo speed sana tofauti na Ordinary ambayo ni ya Tanzania hii inapiga ruti za Dar es salam mpaka Mbeya sababu inatembea taratibu sana ata gharama zake ni nafuu kwa kifupi hii inaitwa mkombozi wa wanyonge"
Ayo yalikuwa maneno ya Baba akiniambia huku tunakimbia kurudi mabehewa ya nyuma kabisa maana ndio bamdogo alisema wapo huko na kilichofanya tuwe na wasi wasi ni mizigo aliyibeba inaweza kupitiliza...!!
"Bamdogo Erastoooooo....Mimi Tizoo ukwapii Baba... Weee bamdogo Erasto weee huko wapi Baba jamani..Mimi ni Tizo..!!"
"Aisee sisi tupo hapa bwana... Wee Tizooo..!!"
Niligeka nikamuona Bamdogo Erasto kasimama huku pembeni yake akiwa amekaa mdada wa umri wa kati rangi ya ngozi yake ni maji ya kunde, huku USO wake ukiwa ni wa duara macho ya goroli alafu jicho laini najua mafundi wamehelewa yani lile jicho ambalo demu akikutazama unaweza kusema anakutega kumbe Hana habari na wewe kabisa ila ndio alivyo umbwa..!!
"Weee Tizo unashangaa nini wewe alala..!!"
Baba alinishitua kwa kunitikisa begani maana nilikuwa nimemtumbulia jino uyu Dada mpaka nikajikuta nimepoteza direction yangu.

Muda uo huo na Mama pamoja na Mdogo wangu Assani pamoja na Juma wakawa wamefika Tazara basi ikawa ni furaha ilioje.
"Waooooohhh....Jamani Sakina karibu kwenye nchi za watu huku..!!"
"Asante Dada nimeshafika tayari"
"Khaaaaa! Poleni na safari mwee, kufuma pa TABORA mpaka hipa mmmhh! Safari ndefu sana mwee wa yaya mweee!!"

Basi alikuwa ni Mama akiongea na Mdogo wake uyo Mamdogo Sakina, Mimi nikaabiwa na Baba nitafute vijana wa pikipiki ili waje kubeba uwele na ulezi Bamdogo alileta mwigi tu maana sisi wanyamwezi hatuwezi kuishi bila kula ugari wa uwele au asubuhi uji wa ulezi. Mama alijaribu kupanda ulezi  hapa Mbingu ila uligoma kutokana na maji kuwa mengi kwaiyo Baba alisema bora waagize tu nyumbani TABORA alafu msimu ujao tutaenda milimani huko Ilola tukajaribu kuchoma mabiwi alafu tumwage ulezi tunaamini utakubali tu.

Asubuhi saa kumi na mbili niliondoka zangu na baiskel aina kamongo mayai kuelekea shule, nilikuwa nasoma St. Merry  shule ya Masister hapa Londo iyo nikutokana na uwezo wangu kuwa mkubwa darasani kwaiyo Baba hakutaka nisome shule za yebo yebo, nilishukuru maana ni wazazi wachache sana wenye imani na watoto wao.....

"NDIO TUNAANZA SAFARI YA HADITHI YETU, KWAIYO NAOMBA TUWE PAMOJA MPAKA MWISHO. MAONI YAKO NI MUHIMU."

                     ___ITAENDELEA__
Like comment hisia zako, hii ni story mpya.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.