NGUMU KUMEZA SEHEMU YA 06
ILIPOISHIAKitendo cha kuingia tu, nikamkuta K2 amesimama
akinisubiria, kofi zito likatua shavuni mwangu
nahisi hadi sekretari wake aliweza kusikia kwa
maana mlango bado haukuwa umefunga vizuri.
“Hii ofisi ni ya baba yako?”
K2 aliniuliza kwa sauti ya ukali hadi nikahisi mwili
mzima ukizizima kwa woga. Sikujibu kitu na sura
yangu nikawa nimeiinamisha chini, nikiyasikilizia
maumivu makali ya kibao hicho. Kwa kidole kimoja
akaninyanyua uso wangu na kunitazama huku sura
yake ikiwa bado imejikunja.
“Unahisi kunitom*** kwako ndio kunaweza
kukufanya ukawa mzembe kazini?” “Hapana mkuu”
Nilijibu huku machozi yakinilenga lenga.
“Hata nikikupa kum* yangu au mkun** wangu,
bado huwezi kukiuka sheria na misingi ya kazi.
Unakuja saa mbili?, nakupigia simu hupokei
unajihisi wewe ni kidume si ndio?” k2 alizidi
kufoka, na kunifanya nianze kujiapiza kimoyo moyo
kwamba kamwe sinto rudia kufanya naye
mapenzi, kwa manaa ubabe anao ufanya kwa
wafanyakazi wengine nilihisi kwangu utapungua,
kumbe ndio umeongezeka mara mbili zaidi ya
hapo mwanzo.
“Potea mbele ya macho yangu na ukawaulize
wenzako ni kitu gani ambacho nimeagiza wao
kukifanya. Pumbavu wewe” Nikapiga saluti na
kugeuka, nikafika mlangoni na kukishika kitasa cha
mlango huku dukuduku la kuhitaji kuzungumza
kitu likiwa linanisumbua moyoni mwangu.
‘Potelea pote’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikigeuka na
kumtazama K2 aliye nigeuzia mgongo wake akielekea
kukaa kwenye kiti chake.
“Sikiliza, kuanzi leo. Nijue kama mfanyakazi wako
na si mwanaume utakaye iona mbo** yangu
ikiingia kwenye kum** yako. Jana ndio ilikuwa
mwanzo na ndio itakuwa mwisho” K2 akageuka na
kustuka kusikia maneno hayo niliyo yazungumza,
nikafungua mlango na kutoka kwa hasira, iliyo
yafanya machozi yangu kutiririka hadi secretary akanishangaa .
IFAHAMU HALI YA UTE WA MLANGO WA UZAZI KWA AKINAMAMA(VAGINAL MUCUS) UNAVYOCHANGIA KUPATIKANA KWA MIMBA
ENDELEA
Nikajifuta machozi nikiwa kwenye korido ya
kuelekea kweye ofisi yatu. Nikaingia ndani ya ofisi
wala sikumsalimia mfanyakazi yoyote jambo ambalo
si kawaida kwa maana watu wamenizoea kwa
ucheshi wangu kwa kila mmoja.
“K2 kasha fanya yake”
Rafiki yangu mmoja alizungumza huku akinitizama
hadi nina kaa kwenye kiti changu. Kwa jinsi
ninavyo jijua nikiwa na hasira macho yangu
yanavyo kuwa nikaamini kila mmoja anauona
wekundu wa macho yangu. Nikafumba macho huku
nikiziba masikio, nikijaribu kushusha pumzi
taratibu, ikiwa ni njia moja kupunguza hasira.
“Mambo vipi jamani”
Nilizungumza huku nikitabasamu na kuwafanya
watu wote kuangua kicheko. Kila mmoja akaitikia
alipo maliza kucheka.
“Munacheka nini sasa?”
“Ahaaa najua K2 kasha fanya yake”
“Ahaaa hakuna kitu kama hicho”
“Kwenda huko. Dany sikuwahi kukuona ukiwa na
hasira ila leo nimekuona”
“Nilikuwa naigiza”
“Hahaaaaa, bongo movie umeileta humu ndani?”
“Si unajua siku moja moja kucheka inabidi
nipaweke pembeni. Enhee niambie huyo bi mkora
katoa kazi gani?”
“Kaka umepewa kazi ya kwenda kukusanya taarifa shirika la nyumba la Taifa”
“Kuna nini tena”
Jumbe akaniletea faili na kuniwekea mezani.
Nikalifungua na kuanza kupitia ukurasa mmoja
hadi mwengine.
Kazi iliyo kubwa ni kwenda
kufwatilia mapato ya ujenzi wa nyumba zinazo
jengwa Kigamboni, na inaonyesha kuna ubadhilifu
wa pesa umefanyika. Nikalifunga faili hilo na
kuliingiza kwenye droo yangu.
“Jamani baadaye” “Poa poa Dany”
“Nyinyi hamtoki leo?”
“Ahaa sisi kila mtu ana kazi yake”
“Ahaaa poa poa”
Nikaelekea kwenye lifti, nikaingia na kushuka moja kwa moja.
Nikatoka nje ya jengo, nikatembea hadi barabarani,
nikakodi bajaji iliyo nipelekea hadi katika ofisi za
shirika la nyumba la Taifa. Moja kwa moja nikaelekea
sehemu ya mapokezi na kumkuta dada mmoja
mweupe aliye valia sare nadhifu sana.
“Habari yako dada?”
“Safi, nikusaidie nini?”
“Ahaa naweza kuonana mkurugenzi wa fedha?”
“Hapana mkurugenzi hayupo”
“Meneja kwa niaba yake?”
“Yupo kwenye kikao cha bodi”
“Muhasibu je?”
“Naye pia yupo kwenye kikao cha bodi”
“Na kinaisha saa ngapi?”
“Kusema kweli sijafahamu kinaisha saa ngapi kwa
maana wameingia muda si mrefu”
“Basi ngoja niwasubirie hapa”
“Sawa”
Nikakaa kwenye viti vilivyo eneo hilo la mapokezi.
Nikaitoa simu yangu mfukoni na kukuta meseji ya
K2. Nikaifungua na kukuta ikiwa imeandikwa
ujumbe wa kuniomba msamaha kwa kilicho tokea
ofisini. Nikajikuta nikiachia msunyo hadi sekretari
akanitazama na kutabasamu.
Nikairudisha simu yangu mfukoni nikachukua
gazeti lililopo pembeni na kuaza kulisoma, huku
nikivuta vuta muda kuwasubiria viongozi hao
ambao ninahitaji kuzungumza nao. Hadi inafika saa
saba kamili hapakuwa na dalili yoyote ya viongozi
hao kumaliza kikao chao.
“Kaka samahani ninatoka, ninakwenda lunch”
“Hao viongozi bado wapo kwenye kikao?”
“Ndio naona kikao leo kimekuwa kirefu sana”
“Sawa”
Secretary huyo akaondoka, nikabaki nikiwa nina
tazama wafanyakazi wanao toka na wengine
kuingia. Wazo la kwenda kupata chakula likanijia.
Nikatoka nje ya ofisi hizo, nikatembea sehemu
hadi kwenye mgahawa uliopo karibu sana na ofisi
hizo. Nikakuta wafanyakazi wengi wa shirika hilo
wakiwa wamejazana. Nikatazama tazama kila
sehemu na kumuona yule secretary akiwa amekaa
peke yake kwenye moja ya meza. Nikaenda hadi
alipo kaa na kukaa kwenye kiti hicho.
“Umekuja na wewe?”
“Yaa naona njaa kidogo imeniamsha”
“Karibu mimi ndio nipo katikati”
Muhudumu akanifwata kwa ajili ya kunihudumia.
“Muna pronse?”
“Ndio, unahitaji wakavu au walio pikwa rosti?”
“Niletee wakavu pamoja na chipsi kavu”
“Sawa kaka”
“Na niletee juisi ya ukwaju”
Muhudumu akaondoka.
Nikamtazama dada huyo
jinsi anavyo kula chipsi yai aliyo iagiza, huku
pembeni kukiwa na kuku aliye kaangwa vizuri.
“Hivi mgahawa huu chakula wanacho kipika ni
kizuri?”
“Sanaaaa..., yaani wafanyakazi karibu wote wa ofisi za
hapa karibu tunakimbilia hapa wakati wa kula”
“Wee!!”
“Yaa, wewe ni mgeni kwani?”
“Yaa ni mgeni wa eneo hili”
“Wewe ofisi zako zipo wapi?”
“Ahaa zipo kariakoo”
“Ahaa unafanya kazi gani?”
“Ni mfanya biashara wa duka tu. Sema leo nilikuwa
na miadi ya kuonana na hao viongozi watatu sema
nao wapo kwenye kikao”
Muhudumu akaniletea chakula nilicho muagiza
pamoja na juisi. Nikaanza kula huku nikijaribu
kumchunguza dada huyo, niliye ona ananifaa
kwenye kazi yangu iliyo nileta hapo.
“Unaitwa nani?”
“Mimi?”
“Ndio?”
“Mery”
“Ok mimi ninaitwa Dany”
“Una jina zuri, nina mtoto wa kaka yangu naye
anaitwa Dany basi ni mkorofi huyo”
“Hahaa mbona mimi sio mkorofi”
“Mmm sifahamu kwa sababu sijakaa na wewe”
“Sijui ninaweza kuipata namba yako ya simu?”
“Kusema kweli huwa sitoagi namba ya simu kwa
mtu ambaye simfahamu?”
“Kwa nini?”
Hata kabala Mery hajajibu, jamaa mmoja mrefu
mweusi aliye valia tisheti ya shirika hilo la nyumba la Taifa
akasimama pembeni ya meza yetu na kutuangalia
wote wawili hususani Mery.
“Huyu nani?”
“Ni…..ni ni”
Mery alijing’ata ng’ata huku akionyesha dariri za
kumuogopa jamaa huyo aliye nikazia macho baada
ya kunitazama.
Kila mwanaume anazaliwa na Tezi dume.Jamaa akachukua glasi yangu ya
juisi na kunimwagia kichwani na kuwafanya watu
karibia wote walio kuwepo kwenye mgahawa huo
kushangaa.
“Mose, una fanya nini sasa?”
Mery akashushwa na kofi zito lililo mfanya arudi
kukaa, mara baada ya kunyanyuka kidogo.
Nikajikuta nikitabasamu huku nikijipangusa uso
wangu ulio jaa juisi hiyo ya ukwaju.
“Hivi wewe msen*** unapenda sana kuvamia
mademu za watu si ndio?”
Jamaa alizungumza huku akinitazama kwa macho
ya hasira. Nikashusha pumzi huku nikijaribu
kuizuia hasira yangu.
“Wewe fala si ninakusemesha?”
Jamaa ambaye nilisikia jina lake kwamba anaitwa
Mose alinishika tai na kuninyanyua kwa nguvu
kwenye kiti nilicho kalia. Watu waliopo karibu na
meza yetu wakanyanyuka na kujaribu kumshika
huyo jamaa anaye itwa Mose.
“Muheshimiwa acha hayo si unajua watu wengi”
“Niacheni nimuonyeshe huyu mjinga ana kazi ya
kuparamia paramia wanawake wa watu hapa
mjini”
Mose alizungumza huku akiendelea kunikwida.
Sikuzungumza chochote zidi ya kumtazama Mose
anacho taka kukifanya. Watu wakafanikiwa kumtoa
jamaa huyo mwilini mwangu na kujikuta akiondoka
na vifungo vyangu viwili vya shati.
“Na wewe twende”
Mose akamshika mkono Mery na kuondoka naye.
Nikawatazama jinsi wanavyo toka kwenye mlango
wa mgahawa huo. Nikachukua waleti yangu na
kwenda sehemu ya malipo na kumuuliza
muhudumu aliye nihudumia.
MWISHO WA YOTE: Watanzania kuanza kupima UKIMWI kwa mate?“Una nidai pesa ngapi?”
“Elfu ishirini na tatu”
“Yule dada niliye kuwa nimekaa naye pale
amelipia?”
“Hapana”
“Na yeye munamdai bei gani?”
“Elfu kumi na tisa”
Nikatoa elfu arobaini na tano na kumkabidhi
muhudumu huyo. Kila nilipo pita ndani ya
mgahawa huo watu walinitazama huku wengine
wakionekana kunionea huruma.
“Ila Mose muonevu, yeye kakuta watu wemekaa tu
anawakoromea”
“Ila yule siku atakuja kupata kidume mwenzake
atampiga hadi afurahi”
“Kinacho upa ujeuri ni huo uhasibu wake”
Wadada wawili walio kuwa wamekaa kwenye meza
ya karibu na mlango nilidaka mazungumzo yao
na nikawa nimepata pointi kwamba kumbe mose
ndio muhasibu ambaye ninatakiwa
kumfanyia upepelezi.
Nikafungua mlango na kutoka
moja kwa moja nikarudi katika jengo lao.
Nikamkuta Mery akiwa anamwagikwa na machozi
huku pembeni akiwepo msichana mwengine
akionekana kumfariji.
“Mbona unalia?”
Nilizungumza na kumfanya Mery kunyanyua
kichwa chake alicho kuwa amekiinamisha.
Akastuka kuniona eneo hilo na kuanza kufuta
machozi yake.
“Kaka ni vyema ukaondoka kwa maana Mose
akikukuta hapa unaweza kumsababishia matatizo
mengine Mery”
“Kwani ofisi ya huyo Mose ipo wapi?”
Dada huyo akataka kunielekeza ila Mery
akamuwahi na kumzuia kwa kumshusha mkono
wake alio kuwa ameunyanyua kwa kutaka
kunielekeza ofisi hiyo ilipo.
“Dany tafadhali nakuomba uo……”
Mery alinyamaza gafla huku macho yakitazama
kwenye lifti, nikageuka na kumuona Mose akitoka
kwenye lifti hizo, akanitazama kwa macho makali
huku akinifwata nilipo simama.
“Wewe mwana haramu umekuja hadi huku si ndio”
Mose alizungumza na kutaka kuniparamia, ila
safari hii sikuhitaji kuwa fala tena kwa maana,
kitendo cha kunisogelea nikamuwasha ngumi sita za
kasi zilizo tua katika sura yake na kumfanya
ayumbe na kuanguka chini.
Kila mtu aliye kuwa katika eneo hilo akashangaa.
Mose akaanza kujizoa zoa na kunyanyuka,
akasimama wima japo kwa kuyumba, akajaribu
kurusha ngumi ila zote nilizikwepa, nikamtisha
kidogo aniachia sura, nikavuta ngumi moja kali
kabla haijafika karibu na shingo yake nikauzuia
mkono.
NI RAHISI KUFANYA NGONO NA WASICHANA WANAOKWENDA KANISANI KULIKO AMBAO HAWAENDI KANISANI“Usirudie tena”
Mose alicho kikosea ni kunitukania mama yangu,
hapo sasa nikaweka ustaarabu pembeni na kuanza
kumtembezea kichapo, hadi walinzi wanao linda
eneo hilo wakaja kunikamata. Nikiwa katika kizuizi
cha walinzi hao nikashangaa kuona gari ya polisi
ikija eneo hilo.
“Mtuhumiwa mwenyewe huyu hapa”
Alizungumza mzee mmoja aliye valia suti ya kaki.
Askari hao wakanisogelea wakiwa na bunduki zao.
“Nyoosha mikono, una haki ya kukaa kimya hadi
pale utakapo fika kituoni kwa mahojiano”
Sikuwa mbishi, wakanifunga pingu za mikononi na
kunipakiza kwenye gari lao na kuondoka eneo hilo.
“Afande ninaomba nimpigie mwanasheria wangu
aje kituoni?” Nilizungumza tukiwa njiani. Askari huyo hakuweza
kunijibu chochote zaidi ya kunikata jicho baya.
Tukafika kituo cha polisi. Wakanifungua pingu,
wakaniamuru kuvua mkanda, viatu, kutoa waleti
mfukoni. Nikafanya hivyo kitu lilicho mstusha
askari aliye kuwa akinipapasa ni bastola yangu
niliyo kuwa nimeichomeka kiunoni.
“Jamani huyu ni jambazi”
Askari huyo alizungumza kwa sauti ya juu na
kuwafanya askari wengine wote kituoni kunitazama
mimi huku wengine walio na bunduki
kuninyooshea mimi, huku wakiniamuru kunyoosha
mikono juu kwa ukali sana. INAENDELEA.
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 01
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 02
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 03
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 04
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 05
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 06
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 07
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 08
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 09
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 10
SIMULIZI HII NI KWA WASOMAJI WENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 18. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA. USIKOSE SEHEMU YA 07 YA KISA HICHI CHA KUSISIMUA. INAPATIKANA PIA KWENYE GROUP ZA WHATSAPP NA FACEBOOK.