NGUMU KUMEZA SEHEMU YA 07
SIMULIZI HII NI KWA WASOMAJI WENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 18.ILIPOISHIA
“Dany tafadhali nakuomba uo……”
Mery alinyamaza gafla huku macho yakitazama
kwenye lifti, nikageuka na kumuona Mose akitoka
kwenye lifti hizo, akanitazama kwa macho makali
huku akinifwata nilipo simama.
“Wewe mwana haramu umekuja hadi huku si ndio”
Mose alizungumza na kutaka kuniparamia, ila
safari hii sikuhitaji kuwa fala tena kwa maana,
kitendo cha kunisogelea nikamuwasha ngumi sita za
kasi zilizo tua katika sura yake na kumfanya
ayumbe na kuanguka chini.
Kila mtu aliye kuwa katika eneo hilo akashangaa.
Mose akaanza kujizoa zoa na kunyanyuka,
akasimama wima japo kwa kuyumba, akajaribu
kurusha ngumi ila zote nilizikwepa, nikamtisha
kidogo aniachia sura, nikavuta ngumi moja kali
kabla haijafika karibu na shingo yake nikauzuia
mkono.
“Usirudie tena”
Mose alicho kikosea ni kunitukania mama yangu,
hapo sasa nikaweka ustaarabu pembeni na kuanza
kumtembezea kichapo, hadi walinzi wanao linda
eneo hilo wakaja kunikamata. Nikiwa katika kizuizi
cha walinzi hao nikashangaa kuona gari ya polisi
ikija eneo hilo.
“Mtuhumiwa mwenyewe huyu hapa”
Alizungumza mzee mmoja aliye valia suti ya kaki.
Askari hao wakanisogelea wakiwa na bunduki zao.
“Nyoosha mikono, una haki ya kukaa kimya hadi
pale utakapo fika kituoni kwa mahojiano”
Sikuwa mbishi, wakanifunga pingu za mikononi na
kunipakiza kwenye gari lao na kuondoka eneo hilo.
“Afande ninaomba nimpigie mwanasheria wangu
aje kituoni?” Nilizungumza tukiwa njiani. Askari huyo hakuweza
kunijibu chochote zaidi ya kunikata jicho baya.
Tukafika kituo cha polisi. Wakanifungua pingu,
wakaniamuru kuvua mkanda, viatu, kutoa waleti
mfukoni. Nikafanya hivyo kitu lilicho mstusha
askari aliye kuwa akinipapasa ni bastola yangu
niliyo kuwa nimeichomeka kiunoni.
“Jamani huyu ni jambazi”
Askari huyo alizungumza kwa sauti ya juu na
kuwafanya askari wengine wote kituoni kunitazama
mimi huku wengine walio na bunduki
kuninyooshea mimi, huku wakiniamuru kunyoosha
mikono juu kwa ukali sana.
ENDELEA
Nikafwata kama wanavyo hitaji, nikainyoosha
mikono yangu juu huku nikimtazama askari aliye
nichomoa bastola yangu.
“Piga magoti wewe mjinga”
Askari mwengine alisisitiza kwa sauti ya ukali,
taratibu nikapiga magoti. Askari huyo akachukua waleti yangu na kuifungua, akaanza kuikagua
vitambulisho vyangu. Nikamuona akistuka baada
ya kutoa kitambulisho changu cha kazi.
Akanitazama mara mbili mbili huku macho
yakimtoka na jasho likimwagika.
“Kuna nini kinacho endelea hapa”
Nilisikia sauti ya kike, nyuma yangu. Ikanibidi
kugeuka na kumkuta mkuu wa polisi ambaye
ninamtambua ni rafiki wa karibu sana na K2 na
mara nyingi niliweza kumuona akija ofisini kwetu.
“Mkuu kuna huyu kijana alifanya fujo, ndio
tumemleta hapa kituoni”
Mwanamama huyo mrefu kwenda juu, aliye valia
suruali ya kaki pamoja na shati la kaki, lenye nyota
kadhaa kwenye bega lake, akazunguka na kuja
kusimama mbele yangu.
“Mumegundua nini?”
Alimuuliza askari aliye shika kitambulisho changu.
Askari huyo akaonekana kupata kigugumizi na
kujikuta mkuu wake akikichukua kitambulisho
hicho na kukisoma. Akanitazama kwa haraka kisha
akayarudisha macho yake kwenye kitambulisho
hicho.
“Nani aliwapa amri ya kwenda kumkamata?”
Askari wote wakaka kimya. Kila mmoja alimtazama
mwenzake, mwanamama huyo kwa ishara
akaniomba ninyanyuke juu. Nikanyanyuka na
kuwafanya askari wote kuduwaa.
“Mrudishieni kila kitu chake, unatoa toa macho ya
nini?”
Askari aliye chukua waleti na bastola yangu,
akanirudishia huku mwili mzima ukimtetemeka.
Sikulijali juu ya woga wake nikachukua kila kitu changu,
nikavaa mkanda pamoja na viatu vyangu.
“Samahani kijana, naomba tukayazungumze ofisini
kwangu”
Mwana mama huyo alizungumza huku
akinitazama. Nilipo maliza kufunga kamba za viatu
vyangu, nikaongozana naye hadi kwenye ofisi yake
iliyopo gorofani.
Akanikaribisha kwenye kiti
kilichopo mbele ya meza yake kisha yeye akakaa
kwenye kiti kilichopo nyuma ya meza yake hiyo
yenye mafaili mengi pamoja na
simu ya upepo.
“Samahani kwa usumbufu wa vijana wangu, naona
walikuchukua pasipo kujua kwamba wewe ni nani”
“Kwa hilo halina tabu, ni vyema nikaondoka na
kwenda kuripoti kazini kwangu kwamba kazi yangu
ilizuiwa na vijana wako”
“Hapana hapana, wachukulie ni vijana wenzako
wale. Endapo wataingia kwenye tabu wengine ndio
kwanza hata pesa ya serikali hawajaitafuna”
“Kwa hiyo na mimi nikafukuzwe kazi kwa ajili ya
vijana wako, unatambua kabisa kazi yangu ilivyo
na uhatari wa hali ya juu, ila bado vijana wako
wakaamua kuniharibia ndio nini sasa”
Nilizungumza kwa kumkoromea mama huyo baada
ya kugundua ameingiwa na hofu kidogo.
“Basi ngoja naweza kuzungumza na bosi wako, ili
kukukingia kifua, si unajua tena sote sisi ni
watumishi wa umma na kazi yetu ni moja”
Mama huyo alizungumza huku akichomoa simu
yake aina ya Samsung Galaxy note 3. Akaminya
minya baadhi ya namba ambazo sikuziona na
kuiweka simu yake sikioni huku akinitazama usoni.
“Shosti vipi?”
“Safi vipi”
Kutokana na simu hiyo kuwa na sauti kubwa
kidogo niliweza kuisikia sauti ya K2, nikatamani
kumpokonya simu mama huyo ila nikajikuta
nikishindwa na kubaki nikiwa nimemkazia macho.
“Safi tu, bwana nina ombi moja”
‘Ombi gani?"
“Kuna kijana wako hapa alikamatwa na vijana
wangu akiwa kwenye kazi yake wakidai alifanya
vurugu kwenye moja ya ofisi sasa nikaona
nikujulishe mapema isije akaja huko ukamuwajibisha”
‘Anaitwa nani?’
“Anaitwa Daniel Thamson Kajenge”
‘Mmmmm’
“Mbona unaguna sasa?”
‘Hapana, upo naye hapo au amesha ondoka?’
“Nipo naye hapa ofisini kwangu”
‘Hembu mpatie simu’
Mama huyo akanipatia simu yake, taratibu
nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Hallo”
“Hivi Dany unachanganyikiwa siku hizi?”
K2 alizungumza kwa ukali na kunifanya nimtazame
mama huyu kwa jicho la kuiba nikagundua
anayafwatilia mazungumzo yangu kwa umakini.
“Hapana mkuu”
“Ni kitu gani kilicho kupeleka huko kituoni. Mbona
unafanya kazi zako kipuuzi kama sio professional
aliye fuzu mafunzo eheee?”
“Hapana mkuu haito jitokeza tena”
“Au unahisi kukupa kum* yangu ndio kunakufanya
uwe unakuwa mbovu kwenye kazi, mbona hapo
nyuma ulikuwa unafanya kazi zako kwa umakini
eheee?”
K2 alizidi kunifokea hadi mama huyo nikaamini
anayasikia mazungumzo hayo. Nikaka kimya kwani
sikujua cha kumjibu K2 ambaye tangu asubuhi
alisha nivuruga.
“Sasa hiyo ripoti hadi inafika kesho saa moja
asubuhi ninaihitaji ofisini kwangu. Sasa wewe kaa
kaa na kuwaza kum* na mku*** wangu uone
mwisho wake utakuwa ni nini. Utavuna upuuzi
wako huo”
Simu ikakatwa, nikaishusha taratibu sikioni
mwangu na kumkabidhi mwana mama huyo aliye
baki akiwa amenikodolea macho.
“Hivi nilicho kisikia ni kweli au……?”
Mwana mama huyo alizungumza huku akiendelea
kunikodolea macho yake. Sikuwa na kitu cha
kumjibu zaidi ya kukaa kimya.
“Nakuomba niondoke tafadhali”
“Sawa unaweza kwenda”
Nikanyanyuka na kumuacha mwana mama huyo
akinisindikiza kwa macho hadi natoka ofisini
mwake. Nikashuka kwenye ngazi na kukutana na
askari aliye kuwa akisoma kitambulisho changu
cha kazi. Sikumsemesha kitu zaidi ya kumpita.
Nikapita mapokezi kila askari akabaki akiwa
amenikodolea macho. Moja kwa moja nikatoka
kituoni. Kusema kweli akili yangu haikuwaza
chohote zaidi ya kurudi nyumbani kwangu.
“Bosi nikupeleke wapi?”
Dereva mmoja wa pikipiki alisimama pembeni
yangu huku akinitazama. Taratibu nikajikuta
nikipanda pikipiki hiyo.
“Nipeleke Sinza kwa Remy”
“Sawa mkuu”
Dereva huyo mwenye pikipiki aina ya boksa
akaanza safari. Hadi tunafika maeneo ya Sinza
ndipo nikaanza kumuelekeza hadi mtaa ninao kaa.
Nikamlipa kiasi alicho nitajia na kuingia ndani.
Nikamkuta Mariam akiwa amekaa kwenye kibaraza
anasikiliza miziki kwenye simu yake. Nikampita
bila salamu, na kwa jinsi shati langu lilivyo katika
vifungo nahisi aliweza kujiuliza maswali.
Nikakatiza kwenye korido na kukutana na Asma
akiwa anatoka kuoga, huku amejifunga tenga moja
tu.
“Dany mambo?”
Asma alinisalimia huku akiwa na tabasamu pana
usoni mwake.
“Poa za kushinda?”
“Salama”
Sikutaka kukenua kenua meno, nikafika mlangoni
mwangu. Nikafungua mlango na kuingia, nikaanza
kuvua nguo moja baada ya nyingine hadi
nikabakiwa na boksa. Nikawasha feni na kujitupa
kitandani, kila nikiwaza jinsi ya kuifanya kazi niliyo
pewa na ofisi nikajiona nimevuruga mpangilio
mzima.
“Ohooo Mungu wangu nisaidie”
Nilizungumza huku nikiwa nimetizama juu. Sikuwa
na jibu la uhakika wa nini nifanye. Mazingira ya
chumba changu nilivyo yaacha asubuhi kwa muda
huu hayaniridhishi kabisa.
Nikaanza kufanya usafi
wa kubadilisha mashuka na kuweka shuka jengine,
nilipo maliza hapo nikahamia kwenye kufagia na
kufuta futa vumbi kwenye meza ya Tv pamoja na
redio yangu. Sikuishia hapo nikavaa pensi na
tisheti nikatoka nje nikiwa na ndoo ndogo nikakinga
maji nusu na kurudi nayo chumbani kwangu na
kuanza kudeki kila sehemu.
Nikamaliza kufanya usafi wangu huo, nikachukua
nguo zangu zote chafu na kutoka nazo nje, nikiwa
nimeziweka kwenye dishi langu. Nikaanza kufua,
nikiwa ninaendelea kufua Asma akatoka akiwa
amevalia suruali iliyo mbana makalio yake
makubwa.
“Nakuona leo umeamua kuwa dobi”
“Yaa kidogo dogo si unajua maisha ya ubachela”
“Kweli ila unabidi ufanya uoe Dany, kazi ndogo
ndogo kama hizo za kufua zitakuondokea”
“Ni kweli ila bado nipo nipo kwanza si unajua
wanawake wa sasa ni pasua vichwa na wengine
hatupendi mambo hayo ya kuumizwa kichwa”
Asma akachukua kigoda kilichopo eneo hilo la
uwani ambapo kuna jiko la wa mama wa kupikia.
Akakaa pembeni ya tanki kubwa la maji lililopo
hapa nyumani kwetu.
“Ni kweli, lakini kwa sasa hata wanaume
munapasua vichwa. Wanawake wanawapenda ila
hampendeki sijui kwa nini?”
“Sio wote. Hivi jana ilikuwaje kwa juma kwa
maana ninaona alitaka kukua kwa kisu?”
“Yaani Dany kaka yangu mimi nimesha jichokea.
Mwanaume hapendeki, mwanaume ana wivu
nashindwa hata nimfananishe na kitu gani. Yaani
unavyo niona hapa hata kwenda kwa majirani
hataki. Kila kitu amenunua na kuweka ndani, ni
mimi na Tv na Tv na mimi, nikichoka ni kulala tu”
“Kwa nini anakuwa hivyo, hakuamini au?”
“Kigezo chake kwamba mimi ni mzuri kwa hiyo
nikitoka nje watu wataniiba”
“Hahaaa sasa jana ilikuwaje hadi akakupiga?”
“Jana unajua kisa cha kupigwa ni kwamba.
Tulikuwa tunaangalia myereka ya kina Jonh Cena,
sasa mimi nikasema John Cena ni mzuri ana kifua
kikubwa, basi hapo ndipo ugomvi ukaanza.
Akaanza kusema ooooh sijui umalaya umezidi hadi
ninawasifia wanaume kwenye Tv ooooh kimepanda
kimeshuka. Sasa nikawa ninamjibu mwenzangu
kama ninamtania kumbe akachukulia serious, ndio
akaanza kunipiga na kutaka kunichoma na kisu”
Mazungumzo ya Asma yakanifanya nicheke na
kujikuta hata mawazo ya kazini kwangu yakikaa
pembeni kwa maana katika maisha yangu
sikuwahi kuona wivu wa namna hiyo.
“Yupo wapi sasa mume wako?”
“Kasafiri kaenda Arusha, kapeleka mzigo wa
mafuta”
“Mzigo wa mafuta?”
“Ndio mume wangu ni dereva wa magari makubwa
yale ya mafuta, siku nyingine hupeleka mafuta
Rwanda, Burudi, Congo”
“Ahaaa, sasa jana ulivyo rudi chumbani
hakukoroma?”
“Wee ana ubavu, akikoroma tu namwambia
ninakuja kukugongea basi anakaa kimya”
Nikamaliza kusuuza nguo zangu, Asma akaniomba
kunisaidia kwenda kuzianika. Sikuwa na hiyana
nikamuachia kindoo nilicho jaza nguo hizo na
mimi nikamalizia kuyafua mashuka yangu.
“Asante mwaya”
“Usijali kaka yangu, sasa ngoja mimi niandae
chakula cha usiku”
“Nihesabu basi”
“Usijali, ila unakula ndizi nyama wewe”
“Ahaa hapo mbona umenifikisha”
“Basi ngoja niandae chap chap, si unajua muda
umesonga”
“Poa”
Asma akaondoka na kuniacha nikiwa ninasuuza
mashuka yangu. Nikamaliza shughuli hiyo na
kuzunguka nyuma ya nyumba kwenye kamba za
kuanikia nguo, nikaanika mashuka yangu na kurudi
sehemu nilipo kuwa ninafulia. Nikamwaga maji ya
mapovu chooni na kuanza kuyasuuza mabeseni
hayo.
“Nani amemwaga maji ya mapovu chooni?”
Mariam alizungumza huku akinitazama usoni,
nikatambua analifahamu jibu lake, ila anatafuta
mbinu za kuzungumza na mimi. Sikujibu chochote
zaidi ya kubeba mabeseni yangu yote na kurudi
nayo chumbani kwangu. Nikayaweka chini ya
uvungu na kujitupa kwenye sofa.
“K2 mamae ipo siku nitakuonyesha kwamba mimi
mtoto wa mbwa”
Nilijikuta nikizungumza mazungumzo hayo huku
nikikagua namba zilizo piga kwenye simu yangu
kipindi nikiwa nipo nje ninafua, na namba ya K2 ni
moja wapo.
‘Huyu ataniletea chakula kweli, au ana nizingua?’
Nilijiuliza swali hilo huku nikiwasha Tv kufwatilia
taarifa ya habari ya saa mbili usiku inayo rushwa
na kituo cha ITV.
Hadi taarifa ya habari inamalizika saa tatu kasoro
Asma hakuleta chakula chochote. Nikataka
kunyanyuka kwenye sofa ili nijiandae kwenda
kununua chakula ila, mlango wangu ukagongwa.
“Nani?”
“Mimi”
Nikasikia sauti ya Asma, kwa haraka nikanyuka na
kwenda kufungua mlango. Nikamkuta akiwa
amesimama huku mkononi mwake ameshika
‘hotpot’ kubwa pamoja na sahani isiyo na chakula.
“Karibu ndani, si vyema kupeana chakula
mlangoni”
Asma akatabasamu na kuingia ndani. Moja kwa
moja akaelekea mezani na kuweka ‘hotpot’ hilo
mezani pamoja na sahani hiyo.
“Chumba chako umekipangilia vizuri, unaweza
kusema unaishi na mwanamke”
“Unajua usafi mimi nilifundishwa tangu kipindi nipo
sekondari ya bweni, kwa hiyo nimekulia kwenye
mazingira ya usafi safi hadi hapa nilipo”
“Kweli Dany, kuna wanaume ukiingia vyumba vyao
utatamani kukimbia kwa manaa vimepangiliwa
vibaya kama stoo”
Asma alizungumza huku akipakua chakula hicho,
kinacho nukia vizuri hadi nikajikuta utumbo wangu
ukitetemeka kwa njaa na hamu ya kula chakula
hicho.
“Oooho nimesahau kijiko”
“Usijali vijiko ninavyo”
“Umeviweka wapi?”
Nikamuonyesha kiji trei cha kuwekea vyombo,
akachukua kijiko kimoja na kuja kukiweka kwenye
sahani ya chakula. Kabla hatujazungumza chochote
sote wawili tukaisikia sauti ya Juma huko nje.
“Mariam umemuona wapo Asma?”
Nikamuona Asma akihisi kuishiwa nguvu, kutoka
chumbani kwangu akiwa anatamani kutoka ila
anashindwa atatoka vipi kwa maana chumba
changu ndio cha kwanza kabisa kwa upande wa
uwani isitoshe endapo atatoka na kukutana na
mume wake basi inaweza kuzuka kesi nyingine ya
kufikiriana vibaya. ITAENDELEA
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 01
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 02
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 03
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 04
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 05
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 06
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 07
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 08
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 09
- NGUMU KUMEZA | Sehemu ya 10
SIMULIZI HII NI KWA WASOMAJI WENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 18. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA. USIKOSE SEHEMU YA 08 YA KISA HICHI CHA KUSISIMUA. INAPATIKANA PIA KWENYE GROUP ZA WHATSAPP NA FACEBOOK.