Notification texts go here Contact Us Buy Now!

NGUMU KUMEZA; (18+) Sehemu ya 08- Muandishi: Jclassic boy (Next level Author)

ILIPOISHIA “Nani?” “Mimi” Nikasikia sauti ya Asma, kwa haraka nikanyuka na kwenda kufungua mlango. Nikamkuta akiwa amesimama huku mkononi mwake ameshika ‘hotpot’ kubwa pamoja na sahani isiyo na chakula. “Karibu ndani, si vyema kupeana chakula mlangoni” Asma akatabasamu na kuingia ndani. Moja kwa moja akaelekea mezani na kuweka ‘hotpot’ hilo mezani pamoja na sahani hiyo. “Chumba chako umekipangilia vizuri, unaweza kusema unaishi na mwanamke” “Unajua usafi mimi nilifundishwa tangu kipindi nipo sekondari ya bweni, kwa hiyo nimekulia kwenye mazingira ya usafi safi hadi hapa nilipo” “Kweli Dany, kuna wanaume ukiingia vyumba vyao utatamani kukimbia kwa manaa vimepangiliwa vibaya kama stoo” Asma alizungumza huku akipakua chakula hicho, kinacho nukia vizuri hadi nikajikuta utumbo wangu ukitetemeka kwa njaa na hamu ya kula chakula hicho. “Oooho nimesahau kijiko” “Usijali vijiko ninavyo” “Umeviweka wapi?” Nikamuonyesha kiji trei cha kuwekea vyombo, akachukua kijiko kimoja na kuja kukiweka kwenye sahani ya chakula. Kabla hatujazungumza chochote sote wawili tukaisikia sauti ya Juma huko nje. “Mariam umemuona wapo Asma?” Nikamuona Asma akihisi kuishiwa nguvu, kutoka chumbani kwangu akiwa anatamani kutoka ila anashindwa atatoka vipi kwa maana chumba changu ndio cha kwanza kabisa kwa upande wa uwani isitoshe endapo atatoka na kukutana na mume wake basi inaweza kuzuka kesi nyingine ya kufikiriana vibaya. ENDELEA
ILIPOISHIA
“Nani?”
“Mimi”
Nikasikia sauti ya Asma, kwa haraka nikanyuka na
kwenda kufungua mlango. Nikamkuta akiwa
amesimama huku mkononi mwake ameshika
 ‘hotpot’ kubwa pamoja na sahani isiyo na chakula.
 “Karibu ndani, si vyema kupeana chakula
 mlangoni”
 Asma akatabasamu na kuingia ndani. Moja kwa
moja akaelekea mezani na kuweka ‘hotpot’ hilo
mezani pamoja na sahani hiyo.
“Chumba chako umekipangilia vizuri, unaweza
 kusema unaishi na mwanamke”
 “Unajua usafi mimi nilifundishwa tangu kipindi nipo
 sekondari ya bweni, kwa hiyo nimekulia kwenye
 mazingira ya usafi safi hadi hapa nilipo”
 “Kweli Dany, kuna wanaume ukiingia vyumba vyao
 utatamani kukimbia kwa manaa vimepangiliwa
vibaya kama stoo”
 Asma alizungumza huku akipakua chakula hicho,
kinacho nukia vizuri hadi nikajikuta utumbo wangu
ukitetemeka kwa njaa na hamu ya kula chakula
 hicho.

“Oooho nimesahau kijiko”
 “Usijali vijiko ninavyo”
 “Umeviweka wapi?”
Nikamuonyesha kiji trei cha kuwekea vyombo,
akachukua kijiko kimoja na kuja kukiweka kwenye
sahani ya chakula. Kabla hatujazungumza chochote
sote wawili tukaisikia sauti ya Juma huko nje.
 “Mariam umemuona wapo Asma?”
Nikamuona Asma akihisi kuishiwa nguvu, kutoka
chumbani kwangu akiwa anatamani kutoka ila
anashindwa atatoka vipi kwa maana chumba
 changu ndio cha kwanza kabisa kwa upande wa
 uwani isitoshe endapo atatoka na kukutana na
mume wake basi inaweza kuzuka kesi nyingine ya
kufikiriana vibaya.


ENDELEA
“Jamani Dany nitafanyaje, huyo ni mume wangu?” Asma alizungumza kwa sauti ya chini huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga, hata shuhuli ya kuniandalia chakula ikakata. Kwa haraka haraka nikafikiria kitu cha kufanya. Nikatoka nje na kukuta Juma akiwa amesimama uwani, akanitazama kwa jicho kali linalo onyesha dhairi kwamba bado ana kinyongo na mimi. Mariam akanitazama kwa macho ya kuiba na kukaa kimya hata swali alilo ulizwa na Juma hakulijibu.
“Mariam mbona unanichunia, si nimekuuliza swali?” “Mimi sijui ni wapi alipo mke wako” Kabla Juma hajazungumza chochote, nje tukasikia kelele za watu. Kwa haraka Mariam akanyanyuka na kukimbilia nje, Juma naye akafwata wote wawili wakatoka nje.

Nikarudi chumbani kwangu na kumkuta Asma akiwa amesimama, huku akiwa hana raha kabisa. Nikafungua pazia na kuchungulia kwenye korido sikumuona mtu wa aina yoyote aliye simama.
“Njoo njoo” Asma akanyata hadi sehemu nilipo mimi, nikatazama tena hakuna mtu na mlango wa mbele ukawa umefungwa na si rahisi kwa mtu kumuona akitoka. Kwa haraka Mariam akatoka na kukimbilia uwani na moja kwa moja nikamshuhudia akikimbilia bafuni. Kidogo na mimi nikashusha pumzi na kupata amani kwa maana ninaamini kitu ambacho kingekwenda kudhaniwa na kila mtu ni kwamba mimi na Asma tuna mahusiano ya kimapenzi wakati si kitu sahihi.

Kelele zilizidi kusikika nje na kujikuta na mimi nikitoka kwenda kushuhudia ni kitu gani kinacho endelea. Nikiwa nimefika mlango wa kutokea nje, kabla sijaufungua akaingia mama mwenye nyumba.
“Mama vipi huko kuna nini?”
“Nyumba ya mzee Jongo inawaka moto” Mama Mariam alizungumza kwa haraka haraka huku jasho likimwagikia, akaingia chumbani kwake na kunifanya na mimi kutoka kwa haraka na kwenda kushuhudia. Nikatoka getini na kupishana na watu wengi wakikimbilia ilipo nyumba ya mzee Jongo. Na mimi nikaungana nao na kwenda hadi sehemu ilipo nyumba hiyo.
Nikafika na kukuta nyumba hiyo ya kifahari ikiteketea kwa moto mwingi huku vijana na wamama wakijitahidi kuuzima moto huo na kuokoa baadhi ya vitu vya garama vilivyomo kwenye nyumba hiyo.

“Jamani mwanangu” Mzee Jongo alilalama huku machozi yakimwagika, watu cha kushangaza walibaki wakimkodolea macho. Kwa haraka nikamsogelea na kumuuliza mwanaye huyo yupo wapi.
 “Ndani baba yangu, gorofani kule” Mzee Jongo alinijibu huku akinitazama usoni mwangu. Nikatazama moto huo unao endelea kuteketea. Kwa haraka nikafanikiwa kuona sehemu ambayo ninaweza kuingilia na haina moto mwingi. Nikaanza kukimbia kuelekea ndani. Nikafika kwenye mlango wa uwani ambao wanautumia kama dharura, nikasukuma kwa kujirusha na kuanguka nao hadi chini. Moshi mwingi nilio kutana nao hakunizuia kuweza kuingia huku nikiwa nimebana pumzi zangu kwa umaridadi mkubwa kabisa ili nisiweze kuvuta moshi huo. Nikapandisha hadi gorofani, nikasikia sauti ya msichana ikilia kwenye moja ya chumba ambacho mlango wake umefungwa.

Nikajivuta nyuma kwa haraka na kuupiga teke mlango huo ulio funguka na kunipa nafasi ya mimi kuweza kuingia ndani. Nikamkuta binti mrefu akiwa ameanguka chini, hii ni baada ya mimi kuusukuma mlango wake. Kitanda chake kilisha anza kushika moto, kitu ambacho kimemuokoa na kumuweka hai hadi sasa hivi ni ukubwa wa chumba chake na uchache wa vitu vya ndani.
 “Panda mgongoni mwangu haraka” Nilimuambia binti huyo ambaye mara nyingi niliweza kumuona akitoka kwenye nyumba hiyo ya kifahari siku za nyuma akitumia gari lake aina ya Harrier Lexus na ni msichana mwenye nyodo sana na asiye penda hata kusalimiwa na vijana wa hapa mtaani kwetu.
 Akapanda mgongoni mwangu. Nilipo hakikisha amekaa vizuri, nikavuta pumzi nyingi itakayo nisaidia kutoka na kuupita moshi huo mwingi.

“Moja, mbili, tatuuuu” Nikatoka kwa haraka na kuanza kushusha ngazi hizo zilizo tengenezwa kwa saruji. Moshi mwingi na mkali na uzito wa msichana huyu aliye nishikilia vizuri, vilichangia sana kuanza kunifanya nianza kuhisi kuishiwa na nguvu. Nikaanza kupita katika njia ambayo nilipita hapo awali, kwa bahati mbaya nikakuta apande wa mbao unao waka moto ukiwa umeziba mlango wa dharura hata mlango weyewe nilio kuwa nimeusukuma umeanza kushika moto.
“Shuka mgongoni upite” “Eheee……?” Binti huyo aliniuliza huku akizidi kuning’ang’ania kwa nguvu akionyesha ni dhairi kwamba anaogopa kabisa kushuka. Ikanibidi kumshusha kwa nguvu kisha nikauchukua mlango ambao unawaka moto, sikujali kama ninaungua au laa. Kwa kuutumia mlango huo nikaanza kusukuma mbao iliyo zuia hapo mlangoni.

Binti huyo badala ya kunisaidia alianza kulia huku akipiga mayowe, nikatamani hata kumziba makofi ila nikaona nikitumia hasira sote tutateketea kwa moto ndani hapo. Cha kumsukuru Mungu mbao hiyo ikakatika na kutupa uwazi wa kuweza kupita.
“Pita wewe” Nilizungumza kwa ukali, binti huyo akaanza kuweweseka. Nikamtandika kofi moja la shavu kumtoa mawenge yake ambayo ninahisi yanataka kutupelekea kifo.
 “Eheee” “Msen** nini, nimekuambia pita unashangaa nini?” Binti huyo akapita kwa haraka na kufanikiwa kutoka nje, nikapita na mimi ila kabla sijafanikiwa kupita kuna kipande cha bao kinacho waka moto kikaniangukia mgongoni na kushika kwenye tisheti yangu, nikahitahidi na kutoka nje na kuanza kuminyana na tisheti yangu ambayo imenibana mwili wangu kuivua.

Kwa bahati nzuri nikafanikiwa kuivua, japo kuna baadhi ya maeneo ya mgongoni nilipata majeraha ya kuungua pamoja na mikononi.
 “Umeungua” Aliniambia binti huyo niliye muokoa kutoka ndani, Mzee Jongo akatufwata hadi sehemu tulipo simama na binti yake. Wakakumbatiana na mwanaye kwa furaha. Nikataka kuondoka ila mzee Jongo anakizuia.
“Nakushukuru sana kijana” “Asante”
“Unaitwa nani kijana?” “Dany” “Asante sana” “Dany umeungua mgongoni?” Binti huyo alizungumza na kumfanya baba yake kunitazama mngongoni.
“Mungu wangu, unatakiwa kwenda hospitalini” “Hakuna haja mzee wangu” “Noo umeungua sana, sema hujioni” Mzee Jongo alizungumza kwa msisitizo.

“Lucy si unaweza kuendesha gari vizuri?” “Ndio dady” “Mpeleke mwenzako, hospitalini akapatiwe matibabu” “Sawa dady” Lucy akaelekea kwenye maegesho ya magari yao ambayo yapo mbali kidogo na nyumba yao kubwa inayo zidi kuteketea kwa moto. Lucy akapiga honi na kuniashiria nimfwate kwenye gari lake. Nikaeleke hadi sehemu alipo, kwa ishara akaniomba kuingia ndani ya gari, tukatoka kwenye geti la upande wa pili wa nyumba hiyo ambalo ametufungulia mlinzi wao. Safari ya kuelekea hospitali ikaanza, ndani ya gari sote tulikaa kimya, ikanibidi kuuvunja ukimya wetu.

“Chanzo cha moto ni nini?” “Kusema kweli sifahamu kwa maana mimi mwenyewe nilikuwa nimesha anza kulala” “Ahaa sawa” Kutokana damu imesha anza kutulia, hapo sasa ndipo nilipo anza kuyasikia maumivu ya majeraha ya moto niliyo yapata mgongoni na mikononi. Tukafika hospitalini, kwa haraka tukaelekea mapokezi huku nikiwa kifua wazi, sikuona aibu ya kutembea hivyo ila nilicho kifikiria kwa muda huo ni jinsi gani majeraha hayo yanavyo weza kutulia kwa maana yananiuma kupita maelezo. Lucy akawaelezea manesi tatizo langu, kwa haraka nikaingizwa kwenye chumba cha matibabu, nikachomwa sindano kwenye mkono wangu wa kushoto.

“Hii ni sindano ya nini?” “Kutuliza maumivu” “Sawa” Nesi anaye nihudumia akaanza kunipaka dawa ya maji maji, aliyo nieleza ni ya kusafisha kidonda na kuua backteria ambao wameingia kwneye majeraha yangu. Alipo maliza akanipaka dawa nyingine kisha mikononi akanifunga bandeji.
“Itabidi leo upumzike hapa, kesho tunaweza kukuruhusu” “Sawa. Ninaomba uniitie huyo msichana niliye kuja naye hapo nje” “Sawa” Nesi huyo akakusanya vitendea kazi vyake kisha akatoka, akaingia Lucy huku akinitazama usoni. “Vipi wamekuhudumia vizuri?” “Ndio” “Ohhh masikini pole mwaya” “Asante”
 “Sasa wamekuambiaje?” “Wameniambia leo nipumzike hapa kesho ndio wanaweza kuniruhusu”
“Daaa, sawa basi nitalipia kila kitu, kisha nitakwenda nyumbani kuangalia ni kitu gani kinacho endelea na asubuhi na mapema nitakuwa hapa”
“Sawa” Lucy akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akatoka ndani humo.

Baada ya dakika kama sita hivi nesi mwengine akaja na kunimba nimfwate, tukaelekea kwenye moja ya chumba chenye kitanda cha peke yake, huku kikiwa na Tv, sofa pamoja na choo cha ndani kwa ndani.
“Utalala humu kaka, ukiwa na tatizo lolote basi utawasiliana na mimi, simu ipo hapo mezani”
“Sawa dada yangu”
 Nikaingia bafuni na kukuta kioo, hapo ndipo nikageuka na kujitazama mgongoni. Nikatamani kuzimia, kwa maana kidonda ni kikubwa sana karibia nusu ya mgongo mzima.
“Haya ndio matatizo ya kujifanya shujaa” Nilizungumza huku nikiendelea kujitazama, jinsi gozi ilivyo babuka. Nikarudi chumbani nikawasha tv, hapakuwa na jipya.

‘Kesho kazini itakuwaje?’
Ni swali jengine nililo jiuliza huku nikilala kifudi fudi juu ya kitanda hicho. Kuchoka ukijumlisha na mawazo mengi yanayo kisumbua kichwa changu nikajikuta nikiwa nimelala fofofo.

“Unaendeleaje?” Nilisikia sauti ya Lucy iliyo nifanya kufumbua macho yangu. Nikamkuta Lucy na mzee Jongo wakiwa wamesimama pembeni ya kitanda nilicho lala.
“Kijana vipi?”
“Safi mzee shikamoo” “Marahaba, unajisikiaje na hali” “Ahaa maumivu kwa mbali tu” Nilizungumza huku nikinyanyuka kitandani. Nikakaa kitako huku nikiwatazama. Leo ndipo nikapata nafasi ya kumtazama Lucy vizuri. Kusema kweli ni msichana ambaye amebarikiwa asilimia tisini na tisa ya uzuri. Kila sehemu ya mwili wake imeumbwa na kuumbika, ninaamini mwenyezi Mungu alitumia muda weke mwingi sana wa kumuumba Lucy. Urefu wake wa futi sita na pointi kadhaa kwenda juu, uliweza kuendana kabisa na muenekano wa sura yake iliyo kaa kama Mrwanda.
Kifua chake kimebeba maziwa madogo wastani, huku tumbo lake kikiwa limepigwa pasi. Sasa maeneo ya kiunoni sasa hapo ndipo kwenye kila aina ya maufundi ya mola.

Kuna msemo unao sema ukisikia kwamba kuna wanawake wameumbwa ni kweli wameumbika, basi Lucy naye yupo kwa wale ambao ni kweli wameumbika.
 Kiuno chembamba wastani, kimeshikilia hispi zilizo jichora kama namba nane, makalio makubwa kiasi yanayo shikiliwa na hipsi hizo zilizo shikiliwa na miguu iliyo jaziwa. Unywele mrefu ambao ni wa asili wa Lucy unao fika mgongoni ndio unao zidi kumpa vigezo vingi vya uzuri.
 “Dany mbona unamshangaa sana binti yangu?” Sauti ya mzee Jongo ilinistua na kujikuta nikimtazama usoni mzee huyo.
“Ahaa hapana nafikiria ile ajali ya jana ya moto. Vipi mzee mumepata kutambua chanzo ni nini?” “Ndio, ni mtungi wa gesi, msichana wa kazi aliweza kusahau kuufunga sasa sijui ikawaje ukalipuka na kusababisha moto”
“Pole sana mzee” “Ahaa nimesha poa. Lucy kamuite nesi waje kumshuhulikia kijana kama kuna chochote cha kufanya waje kumfanyia” “Sawa baba”

Kitendo cha Lucy kutoka, kwa kona ya jicho langu la kushoto ndipo nikapata nafasi ya kuona wezere la Lucy jinsi linavyo tingishika kwenye suruali yake aliyo ivaa. Kitendo cha macho yangu kumtazama mzee Jongo macho yetu yakakutana na kumfanya mzee huyo kutabasamu naamini alinistukia kwa kile nilicho kifanya.
 “Kijana hivi unafanya kazi gani?”
“Ahaa mimi, mimi nipo ofisi moja hivi ya serikali”
 “Ofisi gani kwa maana mimi nipo ofisi ya raisi” Kusikia hivyo nikastuka kidogo ila nikajikaza kwa maana hawa ndio watu wakubwa wa nchi hii.

“Mimi nipo ofisi ya usalama wa taifa” “Ohoo, safi sana. Ndio maana jana usiku nikawa ninakufikiria kijana jasiri kama wewe kwa mtaa ule wetu sijaona, kumbe upo huko?”
“Ndio” “Basi inabidi nifanye kitu kwa ajili yako kwa maana nisiwe mnafki, pasipo wewe leo hii mimi nisinge kuwa na furaha hii” “Kwa nini mzee” “Huyu ndio binti yangu wa pekee, tangu mama yake afariki akiwa binti mdogo basi upendo wangu nikaumalizia kwa binti yangu, na endapo kama jana angefariki nahisi hata mimi leo nisinge kuwa hai” “Usijali mzee wangu” “Lazima nijali, wewe ni mtu ambaye hukunitazama kama wale watu walio kuwa wamenizunguka. Uliweza kuyahatarisha maisha kwa ajili ya Lucy wangu. Sasa ni kwanini nisikupe zawaidi” Mzee Jongo alizungumza huku akitabasamu.

Wakaingia Lucy na nesi aliye nihudumia jana. Akaja akiwa na vifaa vyake, akasalimiana na mimi pamoja na mzee Jongo kisha akaanza kunisafisha kidonda changu.
“Kimesha anza kukauka, usivae nguo za kubana sana”
“Sawa nesi” “Je kidonda chake kitapona baada ya muda gani?” Mzee Jongo alizungumza huku akimtazama nesi huyo usoni.
 “Siku nne hadi tano kitakuwa kimesha kauka. Tutamuandikia sindano za kukausha hicho kidonda kwa haraka na kila siku atakuwa anakuja kuchoma ndani ya siku hizo nne” “Sawa, Lucy jukumu hilo utalichukua wewe sawa” “Sawa dady” “Je leo tunaweza kuondoka naye?”
“Ndio leo hali yake ni nzuri sio kama jana”
“Sawa, Dany utaongozana na sisi sawa”
 “Sawa mzee” “Lile shati umekuja nalo”
 “Ndio baba, ila nimelisahau kwenye gari” “Nenda kachukue mwenzako atatokaje” Lucy na nesi wakatoka na kutuacha mimi na mzee Jongo.

“Lucy mwanangu anamatatizo ambayo, yanatakiwa kutatuliwa na mwanaume”
“Matatizo gani tena mzee” “Ahaa bwana mdogo, usitake nikufafanulie naamini umesha jua. Mwanangu ana tatizo ambalo akipata mwanaume shababi basi anaweza kulitatua kwa haraka na atajivunia kuwa na mwanagu” Nikatambua mzee Jongo ana maanisha nini, ila sikujali ni kwanini ameamua kuniambia mimi swala hilo.
“Kwa nini umeniambia mimi hilo swala”
 “Ahaaa nimekuambia hilo ili umchangamkie bwana. Niliweza kumtunza mwanangu hadi sasa amefikisha miaka ishirini na nne naamini bado kufu……” Mzee Jongo akanyamaza baada ya Lucy kuingia akiwa ameshika shati jipya lililopo kwenye mfuko wake wa nailon.

Lucy akaufungua mfuko huo na kulitoa shati hilo ambalo kwa haraka haraka ni saizi yangu kabisa.
“Mvalishe mwenzio, si unaona mikononi ana mabandeji”
Lucy akanza kunivalisha, alipo maliza nikanyanyuka kitandani. Tukatoka nje tukiwa tumeongoza, tukaingia kwenye gari na safari ikaanza huku Lucy akiwa ndio dereva.
“Daughter utaniacha kazini, kisha mutaelekea home sawa” “Sawa Dady” Sikujua ni nyumbani wapi tunapo elekea, tukafika kazini kwa mzee Jongo akashuka, akiwa anashuka akanikonyeza hapo ndipo nikajua kwamba mzee alicho kuwa anakizungumza kina ukweli na si masihara.

“Njoo ukae siti ya huku mbele” Lucy alizungumza, ikanibidi kushuka kupanda siti ya mbele ambayo hapo awali alikuwa amekalia mzee Jongo. Safari ikaanza kuelekea nyumbani kwao.
“Tunakwenda wapi?” “Nyumabani, kuna nyumba yetu ipo masaki ndipo tunapotakiwa kwenda kuishi” “Ahaa sawa, ila itabidi unipeleke kwangu”
 “Huko labda baadaye kwa maana baba ameagiza nikupeleke kwanza Masaki na ameagiza uishi hapo hadi utakapo pona” Lucy alizungumza huku akizidi kuendesha gari lake. Tukafika kwenye jumba jengine la kifahari ambalo linaonekana ndio lipo kwenye hatua za mwisho kabisa za matengenezo.

“Karibu Dany” Lucy alizungumza mara baada ya kushuka kwenye gari, tukaelekea ndani. Nilisha wahi kuingia kwenye majumba ya kifahari ndani ya hili jiji la Dar es Salaam ila katika hili jumba la Mzee Jongo ni maradufu. Jumba limejengwa kwa ustadi wa hali ya juu huku nashi zake kwenye kuta na milango kwa ndani zikiwa ni mithili ya madini ya dhahabu. “Twende” Lucy alizungumza mara baada ya kuniona nikiwa ninashangaa shangaa. Tukaingia kwenye lifti japo ni nyumba ya gorofa moja ila ina lifti yake. Tukafika juu, nikakuta sebule nyingine hii ikiwa imeizidi sebule ya chini mara dufu.

“Hichi ndio chumba utakacho kuwa unakitumia kwa maagizo ya baba kama jinsi alivyo sema” Nikaingia kwenye chumba hicho, kwa jinsi kilivyo kikubwa kikanifanya nibaki nimeduwaa.
“Njoo nikuonyeshe kitu” Lucy alizungumza huku akielekea kwenye mlango mmoja ulipo ndani ya chumba hicho, akaufugua na kuingia ndani na mimi nami nikaingia ndani.
 “Hili ni bafu, sinki hilo la kuogea lote limetengenezwa na madini ya dhahabu hata hayo mabomba unayo yaona hapo pembeni yametengenezwa kwa madini ya dhahabu” Lucy alizungumza, kitendo cha yeye kugeuka na kunitazama, usoni tukagongana vifua na kujikuta chuchu zake zilizo simama vizuri zikigusana na kifua changu kilicho jengeka vizuri kwa mazoezi. INAENDELEA





SIMULIZI HII NI KWA WASOMAJI WENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 18. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA. USIKOSE SEHEMU YA 09 YA KISA HICHI CHA KUSISIMUA. INAPATIKANA PIA KWENYE GROUP ZA WHATSAPP NA FACEBOOK. 










Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.