Notification texts go here Contact Us Buy Now!

Kila mwanaume anazaliwa na Tezi dume.

Tezi dume siyo ugonjwa bali ni kiungo Kama  viungo vingine mwilini. Tezi dume inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa nikutengeneza maji maji ya uzazi wa mwanaume (shahawa), ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizo tengenezwa kutoka kwenye Korodani; na husaidia mbegu za kiume kubaki hai kwa muda
Kila mwanaume anazaliwa na Tezi dume. Tezi dume siyo ugonjwa bali ni kiungo Kama  viungo vingine mwilini. Tezi dume inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa nikutengeneza maji maji ya uzazi wa mwanaume (shahawa), ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizo tengenezwa kutoka kwenye Korodani; na husaidia mbegu za kiume kubaki hai kwa muda unaostahili.
Tatizo linakuja kiungo hiki kinapoanza kutanuka. Kiungo hiki kinatanuka taratibu taratibu mnoo. Hili ni tatizo linalowakumba wanaume wengi. Takwimu zinaonesha kwamba kati  ya wanaume 10, wa 5 na kuendelea wana dalili za kutanuka kwa Tezi dume.
Ukuaji wa Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe hai katika tezi ya kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalo zunguka mirija ya kupitisha mkojo na mbegu za kiume. Tatizo hili kwa sasa linawapata wanaume kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea, tofauti na awali lilikuwa miaka zaidi ya 50.
Takwimu kutoka kwenye shirika la CHRP (Centre for Human Right Promotion), zinaonesha kwamba kiujumla kila mwanaume katika maisha yake ana 16% za kugundulika na saratani ya Tezi Dume, mtu 1 kati ya watu 6 analo hili tatizo; 3% (1 kati 33) wanakufa kwasababu ya Saratani ya Tezi Dume. Saratani hii inaua mwanaume mmoja kila baada ya dakika 13.

VYANZO VINAVYOPELEKEA TEZI DUME KUTANUKA


Tatizo la kutanuka kwa tezi dume limekuwa kwa kasi sana hii ni kutokana na mitindo ya maisha wanaume wengi wanayoishi. Pia na elimu ndogo iliyoko kwenye jamii kuhusu afya zao.
Vifuatavyo ni vyanzo vya kutanuka kwa tezi dume:
- Ukosefu wa lishe kamili na Virutubisho muhimu mwilini.
- Uwepo wa sumu nyingi mwilini.
- Kutokufanya mazoezi.
- Matumizi ya pombe kali, na uvutaji wa sigara.
- Uzito mkubwa (uliopindukia, uliokithiri), na Kitambi.
- Kutokukaa sawa kwa vichocheo vya mwili (Hormone Imbalance).
- Msongo wa mawazo (Stress).
- Magonjwa ya zinaa.
- Umri mkubwa.
-  Upasuaji wa korodani, kuzaliwa na korodani moja.
-  Historia ya Familia (Kurithi).
- Mazingira (Ethnicity).


*DALILI  ZA KUTANUKA KWA TEZI DUME*


Mpaka mtu apate saratani ya Tezi Dume (Prostate Cancer), ujue amekaa na tatizo hilo kwa muda mrefu, si chini ya miaka isiyopungua 10.
Hii hutokana na mrundikano wa mkojo unaobaki kwenye kibofu na kwenye mrija wa mkojo (Urethra) wakati unakojoa; ukiendelea kujirundika kwenye kibofu na mrija; baada ya muda unazalisha “Uric Acid” na ndio inatengeneza saratani (cancer).

Unazijua njia rahisi za kupunguza uzito wa mwili na kuwa na afya bora?

Saratani ziko stage nne. Ya kwanza na yapili ukiwahi unaweza kupona; lakini ikishafika stage ya 3 na 4, hazitibiki. Unasaidiwa kupunguza makali kwa mionzi ukijitayarisha kupoteza maisha muda wowote.
Hivyo ukiona dalili mojawapo kati ya hizi chukua tahadhari na hatua mapema kabla hujaharibu mfumo wako mzima wa uzazi wa mwanaume.
a)    Dalili za awali 
-       Kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu
-       Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
-       Maumivu kwenye mfumo wa mkojo
-       Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
-       Kuhisi kibofu kimeja mkojo muda wote na ukienda kukojoa mkojo hautoki, lakini ukirudi kukaa unahisi kukojoa tena.
-       Homa
-       Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
b)   Dalili za mtu aliyeathirika
-       Maumivu ya mifupa hasa chini ya mgongo, kiuno na mbavu
-       Miguu kuwa dhaifu
-       Kushindwa kumudu tendo la ndoa, au Kuhisi maumivu makali wakati unamaliza tendo la ndoa
-       Kushindwa kuzuia mkojo, pindi unapohisi kukojoa
-       Kushindwa kuzuia haja kubwa (kinyesi cha maji maji)
-       Tumbo kuja gesi mara kwa mara

MADHARA YA TEZI ILIYOTANUKA


Katika hatua za awali, tezi inapotanuka hugunduliwa kwa kupimwa kwa njia ya kidole. Hii ni njia ambayo daktari huingiza kidole kwenye njia ya haja kubwa ili kuweza kubaini kama tezi imetanuka. Kipimo hiki ndicho rahisi kinacho kubalika duniani kote na kisicho na gharama. Lakini kimekuwa kikipata upinzani kutoka kwa wanaume kutokana na imani potofu ya wahusika wa tatizo hili kuona ni udhalilishaji.
Kipimo kingine ni kipimo cha damu. Damu huchunguzwa aina ya protein inayozailishwa na seli za tezi dume, kiitwacho Prostate Antigen (PSA). PSA huonesha kuwapo kwa tatizo kwenye Tezi Dume, lakini kipimo hiki hakina uwezo wa kutofautisha endapo tatizo hilo linamaanisha saratani.
Yafuatayo ni madhara ya tezi iliyotanuka:
-       Kibofu cha mkojo kuuma: hivyo hupelekea mkojo kurudi juu, na kuharibu figo na Ini … … n.k.
-       Kufunga kwa njia ya mkojo kabisa
-       Figo kushindwa kufanya kazi (Kidney Failure)
-       Kushindwa kumudu tendo la ndoa (Ndoa zinavunjika)
-       Ugumba (Infertility, Frigidity for men)
-       Kutokea kwa majipu sehemu ya Tezi Dume
-       Kifo

SULUHISHO KWA TEZI ILIYOTANUKA


a)    Suluhisho Linalopendwa
Watu wengi hukimbilia hospitali pindi wanapopatwa na madhara ya Tezi dume na kujikuta wakipewa tiba ambazo huficha tatizo hilo kwa muda mfupi kisha tatizo hujirudia kwa kasi kubwa.
Tezi iliyotanuka haiwezi kutibika kwa njia za madawa yenye makemikali au mitishamba, lakini madawa au upasuaji hupunguza maumivu ya dalili na kuzifanya zisizidi sana.
Kuna njia 3 za kudhibiti Tezi iliyotanuka
Kusubiri na kufuatilia kwa ukaribu na Daktari:
Inashauriwa kwamba kwa tatizo hili ni bora kuendelea kulichunguza bila kukimbilia tiba kali kama madawa, upasuaji na Tiba kemikali, mpaka pale mtu atakapoona hakuna njia mbadala.
Madawa
“Baadhi ya madawa wanayopewa wagonjwa wa saratani ya tezi Dume yaligunduliwa miaka 30 iliyopita, yanasababisha athari kwenye Ini, Moyo na kuvimbisha magoti. Yamepigwa marufuku katika Nchi haswa za Ulaya.”
– Johnathon Waxman, Cancer Specialist, Hammer Smith Hospital, London
Upasuaji
Njia hii ambayo madaktari hutumia inapelekea “70% ya wagonjwa kuwa mahanithi baada ya upasuaji, na 40% wanashindwa kuzuia mkojo kutoka wanapo banwa na haja ndogo.”
– Johnathon Waxman
Inasikitisha kuona wanaume wanapasuliwa bila uhakika wowote kwamba huo upasuaji utakuwa na manufaa.

Madhara ya kutopata usingizi au kulala mda mfupi?

Maoni 1

  1. *TEZI DUME*

    Tezi dume ni moja ya tezi ya uzazi ya kiume ambayo kila mwanaume anayo, tezi hii lipo chini ya kibofu cha mkojo na inazunguka njia ya mkojo toka kwenye kibofu kwenda kwenye uume.

    *NOTE:Jinsi umri unavyoongezeka tezi dume nayo huongezeka ukubwa ambao unaweza kuwa wa kawaida au Saratani.*

    Kuna aina tatu za magonjwa ya tezi dume.
    •Maambukizi ya Bakteria (Prostatitis).

    •Kukua kwa tezi dume ambayo sio Saratani (Benign Prostatic
    Hypertrophy-BPH).

    •Saratani ya tezi dume.

    *KAZI YA TEZI DUME*
    •Kutoa majimaji anayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) kutengeneza manii (semen).

    *SARATANI YA TEZI DUME*
    Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vitokanavyo na saratani kwa wanaume duniani.

    Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea.

    *VISABABISHI VYA SARATANI YA TEZI DUME*
    Chanzo hasa cha saratani ya tezi dume hakijulikani, saratani hii ina uhusiano mkubwa na;
    •Umri, Wanaume wenye umri kuanzia
    miaka 60 na kuende…
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.