Notification texts go here Contact Us Buy Now!

CHUNGU LAKINI NDIO DAWA

CHUNGU LAKINI NDIO Dawa 


*DARASA LA MAHUSIANO*

Usilazimishe kila mtu unayekutana nae kwenye maisha ya MAPENZI awe wako milele. Wapo watu wanakuja Maishani mwako kukujenga kiakili na kifikra, Kuna wengine watakuja ili kukufundisha namna ya kuishi na mwenza wako, Wapo wengine watakuwepo ili kukupa mbinu za kumdhibiti mwenza wako ki Mahaba.

Kuna wengine kazi yao ni kukuimarisha ki NAFSI ili moyo wako usiishi kwa mateso, Na wengine watakuja kwako kukufanya uijue thamani yako hata kama watakuwa wanapita tu, Kwa hivyo unalo jukumu la kukubaliana na MAJIRA ili uweze kumpata ambaye yeye huyo ATAKUKUTA UMEKOMAA na kuwa mwenye UFAHAMU.

Uonapo unanyanyasika sana kwenye MAPENZI ujue uko shuleni, Kubali kufundishwa ili baadaye uweze kumuacha Mwalimu aendelee na kufundisha wengine na wewe ukawe mhitimu.

Inaumiza kuona uliyempenda yeye alikuwa na sababu zake kwako lakini haina maana ndo huwezi kumpata mwingine NOOOO. Ziko nyakati ngumu zimeandikwa kwako lakini kwa IMANI yako Kuna nyakati nzuri zitakuja na utasahau yaliyokuumiza...
Kubali kudharulika ili uheshimiwe,
Kubali kutupwa ili uokotwe,
Kubali kutemewa mate ili aje wa kukuosha,
Kubali kushushwa thamani ili THAMANI YAKO ISHIKWE NA WAJUAO THAMANI YAKO.

Sio kila aliyesema NAKUPENDA alimaanisha, Wengine husema ili kukupumbaza lakini nikutie MOYO haimaanishi umeumizwa mara ngapi? Umelia mara ngapi? Umekata tamaa kwingi, Neno moja nimelitaka kwako UMTUMAINIE MUNGU. Ishi kwenye gereza la Matumaini. Hakuna gumu la kumshinda MUNGU.

Uliyepo kwenye mahusiano mazuri au ndoa zuri andika comment yako nzuri kuwapa FARAJA wanaopitia magumu kwenye
MAHUSIANO NA NDOA ZAO.

*WHATSAPP  KUJIUNGA GROUP*.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.