'CHOMBEZO YA MAPENZI'
'INAITWA'
--MWANACHUO?.--
MTUNZI;Isaack Kanyankole
NO;0625915000
KUTOKA;DSM TZ
EPISODE;02
...ILIPOISHIA...
Ila kipindi nikiwa naendelea kutazama barabarani,,,nilishtuka baada ya kusikia kelele za watu wakiwa wanaomba msaada na mara kishindo kikubwa kilisikika katika eneo hilo mwili wangu wote uliishiwa nguvu baada ya kuona tukuo ambalo sikutarajia kuliona siku hiyo!?..
...ENDELEA...
Ajari mbaya iliweza kutokea katika eneo hilo gari ambalo lilikuwa lina watu liliweza kuparamia fuso uso kwa uso hama kwa hakika ilikuwa ni ajari mbaya sana,,sikuweza kufika kwenye tukio kwamaana nilijawa na hofu na uwoga hivyo ilinibidi kurudi nyumbani huku nikiwa nina maswali mengi sana kichwani. Thomaides sikuweza kufahamu alipokuwa ameenda hivyo baada ya kufika nyumbani nilivua nguo kwa haraka na kukaa kitandani huku nikiwaza juu ya ajari mbaya ambayo nilikuwa nimeishuhudia kwa macho yangu.
"Dah,,hama kwa hakika sisi ni wasafiri sizani kama kuna mtu ambaye atapona maana sio ajari ile,,ona watu ambao walikuwa wanatafuta riziki zao barabarani wameswagwa dah,,inauma sana". Nilijiongea kwa sauti huku nikiwa nimefumba macho yangu nikiwa natafakari juu ya ajari ambayo niliiona kwa macho yangu.
"Aha!!,,,yaaani,,,yaani asikwambie mtu wale wote ambao walikuwa wanauza pembezoni mwa barabara wameswagwa wote na pia hata waliokuwemo kwenye gari sizani kama kuna mtu atapona duh..maana nimefika kwenye tukio siwezi kusimulia nilichokiona hama kwa hakika tunatembea na kifo mbele yetu". Thomaides alizungumza akiwa anaiingia ndani.
"Dah,,,yaani nimekuwa na hofu kubwa sana nafikiri na sisi kama tungewahi kuvuka na sisi tungepitiwa kwamaana inaonesha wazi gari hilo breki zilikuwa zimeferi na pia dereva alikuwa kwenye mwendo mkali sana ndo maana nafikiri ikatokea hivyo".
"Dah,,ni kweli ila ungefika kwenye tukio usingeamini na kwa jinsi ambavyo wewe muoga hama hakika ungeogopa sana duh yaani,,yaani viungo vya binadamu vilikuwa vimetapakaa kwenye eneo hilo la barabara".
"Acha basi usiseme hayo". Safari hii niliongea nikiwa nasimama kwamaana nilihisi mwili wangu wote kusisimka baada ya Thomaides kuzungumza juu ya kile ambacho alikiona.
"Hebu washa televisheni ili tuweze kufahamu zaidi waliopona lakini sizani kama kuna mtu ambaye amepona maana duh".
"Sawa ila acha kuzungumza uliyoyaona ndomaana mimi sikutaka kufika maana najijua mimi nilivyomuoga na hata Babaangu alinishawishi kusomea udaktari ila nilikataa katukatu maana nilijijua nilivyomuaga heri ya kuwa daktari wa barabara kuliko binadamu maana mimi ni muoga sana". Niliongea nikiwa nawasha televisheni na baada ya kuwasha nilikaa kwenye sofa ambalo lilikuwa kando kidogo na kitanda.
"Weka kwenye channel ya ITV nafikiri wataweka habari sasahivi?". Thomaides alizungumza akiwa anavugua nguo.
"Poa". Niliitikia nikiwa naweka kwenye channel ya ITV na kweli kipindi hichohicho naweka kwenye channel hiyo walikuwa wakitang'aza habari hiyo ya ajari.
"Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde ni kwamba hakuna hata mmoja ambaye ameweza kupona kwenye ajari iliyotokea mabibo hivyo ndugu na jamaa ambaye alikuwa ana mtu kwenye gari hilo anashauriwa kufika muhimbili ili kuweza kuchukua mwili na kwenda kuzika kituo cha ITV na uongozi wote unawapa pole kwa wale waliofikwa na msiba huu Mungu azilaze roho za marehemu mahari pema peponi Amina".
"Dah,,ni kweli ambacho nilikuwa nakiwaza maana ajari haikuwa ya kawaida kabisa ile na pia tumechelewa kuweka ila amna tatizo ilimradi tumepata habari kamili".
"Ni kweli ila unajua wale wote ambao walikuwa barabarani wote wameswagwa yaani duh kila sehemu barabarani kumetapakaa damu japokuwa mimi sio muoga kama wewe lakini sitaki kukumbuka kwa kile ambacho nilikiona kwenye ajari hiyo dah inasikitisha sana leo hii uko salama harafu unapelekwa nyumbani ukiwa maiti duh inauma sana".
"Kweli kabisa inauma sana ila uwezi kupindua Mungu alichopanga".
"Ni kweli sikatai ila sio kila jambo ambalo linatokea Mungu anakuwa amepanga mengine yanapangwa na mwanadamu".
"Simu yako inaita na pia nafikiri leo hii tupike maana tumeshinda nyumbani".
"Sawa ni wewe ila zamu yako ya kupika na kuhusu mboga ni wewe juzi mimi ndo nilitoa".
"Poa basi ngoja nielekee hapo mbele kuchukua mboga". Niliongea nikiwa navaa kaushi na traka na baada ya kumaliza kuvaa nilitoka chumbani na kuelekea walipokuwa wanauza mboga.
"Ohooo,,David vipi siku hizi naona umepotea sana?".
"Hapana kaka,,sema tu ni mambo ya chuoni yanaingiliana ila tupo pamoja na vipi unauzaje leo maana bei yako kila siku inabadilika". Niliongea nikiwa natazama samaki waliokuwepo.
"Ni kweli bei inabadilika kuling'ana na huko ninapowato si unajua tena kule wanavyokubana kwenye kuuza na wewe lazima huku ubane kidogo...kwa upande wa kushoto kuna samaki wa elfu mbili na upande wa kulia ni samaki wa shilingi elfu nne ni wewe na pia kuna dagaa mchele".
"Ohooo basi nipatie dagaa mchele wa shilingi elfu mbili".
"Ok,,poa na pia Sabrina siku hizi anakutafuta sana anadai siku hizi ulimtelekeza".
"Mmmh,,acha mambo yako kwani yeye kwasasa yuko wapi?".
"Kwasasa anauza kwenye duka hilo la nguo". Jordan aliongea akiwa ananionesha duka ambalo Sabrina alikuwa anauza nguo.
"Poa ngoja kwanza nikamuone maana ni muda kidogo".
"Poa ila kuwa makini".
"Kwanini umesema hivyo?". Nilizungumza nikiwa nageuka na kumtazama Jordan usoni.
"Amna ila kuwa makini".
"Sawa". Ilinibidi kuitikia na kuelekea kwenye duka ambalo Sabrina alikuwa anafanya kazi na kweli niliweza kumkuta Sabrina akiwa amekaa huku akionekana kuandika kwenye kaunta buku.
"Oho!,,vipi David yaani toka siku ile umeamua kunisusia ehe?". Sabrina alizungumza akiwa ananisogelea nilipokuwa nimesimama.
"Hapana sema nabanwa chuoni".
"Dah,,yaani kumpenda mtu anayesoma chuo kuna kazi yaani kila kitu unasingizia chuo ona sasa umeanza kujitetea na chuo chako".
"Hapana sio kwamba najitetea na chuo yaani kwa muda huu tuna mitihani ndomaana sionekani mara kwa mara tunakuwa kwenye makundi ya kudiskasi".
"Sawa bwana na vipi bado unanipenda".
"Ndio bado nakupenda ila kwasasa si unajua pia na mwenye nyumba pale nyumbani yupo na unajua anavyogomba sana...usiwe na shaka najua unachotaka hata mimi niko vibaya nina kiu na wewe,,ndani ya siku...!". Kabla ya kumalizia neno ambalo nilitaka kusema nilikatishwa na sauti kutoka nje.
"We Sabrina,,Sabrina". Sauti hiyo ilimfanya Sabrina kubaki amepigwa na butwaa huku akinitazama kwa hofu na pia alionekana waziwazi kutetemeka.
Na hapohapo niliweza kukumbuka kauli ya Jordan hivyo na mimi nilijawa na wasiwasi huku nikigeuka na kutazama kwa nje na mara Sabrina alinishika mkono kwa nguvu na kunipeleka mahari fulani iliyokuwa na nguo nyingi na kunifunika huku akiweka kidole kinywani mwake akiashilia waziwazi nisipige kelele wala kufurukuta!?..