mahitajii:
*nyama robo
*kitunguu maji kimoja
*viazi mbatata viwili size ya kati
*nyanya kubwa mbili
*curry powder/binzari ya manjano
*chumvi kiasi
*tangawizi na thomu
*pilipili manga
*ndimu (ukipenda)
*mafuta ya kupikia vijiko vitatu vya chakula
JINSI YA KUPIKA:
nimeanza kuikata na kuiweka nyama viungo; niliweka chumvi, curry powder, pilipili manga, tangawizi na vitunguu thomu kisha nikaicha kama masaa mawili ili viungo vikolee vizuri nyama iwe na ladha.
baada ya hapo niliiweka jikoni nyama na kuivisha kwa moto mdogo mdogo na kuweka maji kidogokidogo ili nisiharibu ladha mpka ilipoiva.
nyama ilipoiva nikaweka yale mafuta juu yake na kukatia kitunguu humohumo huku nikiwa nakoroga koroga ili isigandie kwenye sufuria baada ya vitunguu kuwa brown nikaweka viazi na baada ya hapo nikaweka nyanya na kumalizia na vile viungo (spices) bila kusahau chumvi, hapo nikawa naweka maji kidogo kidogo mpaka viazi vilipoiva na mchuzi ukawa tayari.
enjoy !!!!
Nb: wakati wa kuchemsha nyama ukiwa ushaweka viungo au kuunga mchuzi ukiwa ushaweka nyanya na viungo usiweke maji mengi kwa wakati mmoja utaharibu ladha ya viungo.