Amna asiyejua kuwa jiko ndio sehemu ya muhimu sana katika nyumba ikifuatiwa na vyoo. kwanza kwasababu ndio sehemu chakula cha nyumbani kinapo andaliwa na kuhifadhiwa. Je, ni vitu gani vinyavyofanya jiko lako lionekane la kisasa zaidi
Kama unachakuongezea usisite kuandika kwa comment ili kuwasaidia na wengine wanao jitahidi kuwa na JIKO LA KISASA.
Vifuatavyo ni vitu 10 vitakavyolifanya Jiko lako liwe la kisasa
Rangi ya jiko lako:
Hii inaweza ikawa ni rangi ya kupaka au ni tiles but what matters ni rangi unazo tumia. Ilijiko lako lionekane nadhifu epuka kutumia rangi ambazo zinaleta giza mfano dark green, dark blue etc instead tumia rangi kama light green, light blue na yellow. Lakini ukitaka Jiko lako liwe na muonekano wa kisasa zaidi nakushauri utumia rangi nyeupe iwe kama base ya rangi ya jikoni kwako. hapa namaanisha hata vifaa utakavyo nunua pendelea viwe vya rangi nyeupe kwani ufanya jiko lionekane safi na huwa rangi nyeupe haifichi uchafu. Na ili kulifanya lisiwe kama kachumbari epuka kutumia rangi zaidi ya mbili kwenye kuta na makabati ya jikoni.
Mwanga (lights):
Hakikisha jiko lako lina mwanga wa kutosha wakati wote iwe mchana ama usiku. uwepo wa mwanga wa kutosha inafaida ya kufanya jiko lako liwe na mwenekano mzuri na pia mwanga unsaidia kufukuza wadudu amabao wanavutiwa na mwanga hafifu.
Usafi wa jiko lako:
Hakikisha jiko lako ni safi kwaniza kwenye kuta hadi kwenye vyombo unavyotumia. Na ilikulifanya jiko lako liwe safi lazima uhakikishe unvyo vifaa vyote vya kufanyia usafi ikiwemo sabuni yenye harufu nzuri, mabrush, vitambaa vya kufutia vyombo na meza na bila kusaha dustbin yenye mfuniko. Pia unaweza ukatumia airfresher kama vile Air Freshener Dispenser Machine ambayo italifanya jiko lako liwe na harufu nzuri na sio shombo za vyakula au unaweza ukanunua Jameelah Air Freshener ambayo ni ya kuspray
Vyombo Vya Kisasa:
Uwezi sema unajiko la kisasa kama bado unatumia vyombo vya low quality. Ili jiko lako liwe la kisasa hakikisha unatumia vyombo high quality na nikisema high quality simaanishi vya bei ghali but namaanisha vyombo vya kawaid ambavyo utavichaguwa viwe vina blend na mwonekano wa jiko lako. na kwa hapa tuna zungumzia Mordern Kitchen ambayo ni tofauti na African tradition kitchen. So kwa modern kitchen jitahidi uwe na vyomba vya kisasa. Mfano wa vyombo hivyo ni kama:
oven (zipo hadi za 350,000 Tshs via Jumia)
Vyombo vya kupikia vya kisasa kama sufuria zisizo natia chakula
Dinner set
Mapangilio wa jikoni:
Kwa kawaida jikoni ni mahali ambapo panakuwaga na vitu vingi sana. Kuna vyombo, vyakula na vifaa vingine na vingine ambavyo havitakiwi kuwa jikoni but sometime utavikuta jikoni. Ili jiko lako liwe la kisasa zaidi hakikisha unapunguza idadi ya vitu jikoni has vile ambavyo huvitumii na pili ni kuwa na mpangilia mahalumu wa vyombo vyako sio kila chombo kinakuwa hakiwa mwelekeo. Ukishakuwa na mpangilio wa vyombo vyako inakuwa rahisi katika arrangement ya jiko lako kwa kuwa kila utakapokuwa umetumia chombo utakirudisha mahali pake baada ya kukitumia na kukisafisha.
Kama unachakuongezea usisite kuandika kwa comment ili kuwasaidia na wengine wanao jitahidi kuwa na JIKO LA KISASA.