MAHITAJI
Nyama ya kusaga kilo 1Vitunguu maji 2Vitunguu saumu 2Tangawizi 1Nyanya 4Mafuta ¼ litaChumvi kijiko 1 cha chaiKaroti 2Pilipili hoho 1Ndimu. 1
MAELEKEZO YA JINSI YA KUPIKA
Menya vitunguu na ukate kwenye vipande vyembamba sanaMenya na kwangua karoti iwe kama ujiMenya pilipili hoho na kisha kata vipande vyembambaMenya nyanya na zikate kawaidaMenya, osha na kisha kwangua tangawiziTwanga vitunguu saumuBandika sufuria ya kupikia jikoniWeka nyama na anza kukoroga ili kuzuia isigandie kwenye sufuria na kuunguaWeka kitunguu maji huku ukiendelea kukoroga kwa muda wa dakika 10 Weka kitunguu saumu na tangawiizi. Endela kukoroga kwa muda wa dakika 5 zaidi.Weka mafuta kidogo sana ili kufanya viungo viize.Weka pilipili hoho, karoti na kamulia ndimu. Ongeza chumvi kidogo. Endelea kukoroga.Weka nyanya, koroga na funika sufuria na mfuniko kwa muda kama dakika 10.Funua angalia kama imeiva. Unaweza kujiramba.