Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JINSI YA KUPIKA KABICHI ILIOCHANGANYWA NA MAYAI


JINSI YA KUPIKA KABICHI ILIOCHANGANYWA NA MAYAI

Kabichi ni aina ya mboga za majani ambayo hupikwa kwa  mapishi tofauti. Unaweza kupika kabichi yenyewe bila kuchanganya na chochote pia  unaweza kupika kwa kuchanganya na nyama, mayai au chochote unachoona kinafaa  mboga yako itakuwa nzuri  na kuweza kuliwa na ugali, wali na hata kupikia pilau.

Leo  tutaangalia jinsi ya kupika kabichi iliyochanganywa na mayai, ambapo tunaanza na mahitaji pamoja na  hatua za kufuata katika upikaji wa kabichi iliyochanganywa na mayai. -MAHITAJI ·  Kabichi moja ya ukubwa wa wastani ·  Mayai manne (4) ·  Mafuta robo lita ·  Vitunguu vinne (4) ·  Karoti kubwa moja ·  Pilipili manga kiasi ·  Chumvi kiasi kwa ladha 
JINSI YA KUPIKA KABICHI HATUA KWA HATUA

1.  Chukua kabichi ulikatekate kisha ulioshe.

2.  Washa jiko lolote ulilonalo liwe la mkaa, gesi au umeme.

3.  Kisha bandika kabichi ulilolikatakata na kuliosha liache liive kidogo kisha ipua.

4.  Menya nyanya, katakata vitunguu, karoti uviweke tayari kwa mapishi.

5.  Bandika sufuria jikoni na utie mafuta ya kupikia, yakipata moto tia vitunguu ukaange mpaka vibadilike rangi kisha tia nyanya ukaange.

6.  Nyanya zikishaiva tia karoti kaanga kidogo.

7.  Baada ya hapo tia pilpili manga pamoja na kabichi ulilolichemsha.

8.  Vunja mayai uliyoandaa na kisha changanya na kabichi ililoungwa tayari na ukoroge hadi mboga yako ikauke.

Mpaka kufikia hapo mboga yetu ya kabichi iliyochanganywa na mayai itakuwa imeiva na tayari kwa kuliwa kwa chakula ukipendacho iwe ugali, wali hata pilau.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

تعليقان (2)

  1. [video]https://www.youtube.com/watch?v=nuFbeYeZ60o[/video]
  2. Kabeji Ya Kukaanga



    Vipimo:

    Kabeji - ¼ kabeji

    Karoti - 2

    Kitunguu - 2 viwili

    Nyanya - 1

    Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha chai

    Pilipili mboga - ½

    Chumvi - kiasi

    Pilipili manga - ½ kijiko cha chai

    Bizari ya manjano - ¼ kijiko

    Pilipili zilorowekwa katika siki

    (hot pepper rings) - 2 vijiko vya supu

    Mafuta - 2 vijiko vya supu

    Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

    Katakata kabeji, karoti, vitunguu, pilipili mboga, nyanya weka kando.
    Tia mafuta katika karai kaanga vitunguu hadi vilainike na kuanza kugeuka rangi. Usiache vikageuka rangi sana.
    Tia nyanya, nyanya ya kopo, chumvi, pilipili manga, bizari, endelea kukaanga kidogo.
    Tia karoti endelea kukaanga kidogo.
    Tia kabeji na pilipili mboga kaanga kidogo tu.
    Zima moto na changanya na pilipili zilokatwakatwa na kurowekwa katika siki (hot pepper rings) ikiwa tayari kuliwa.
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.