MAHITAJI KWA AJILI YA KASHATA ZA NJUGU
- Njugu nusu
- Sukari nusu kilo
- Unga wa iliki kiasi
- Maji robo kikombe
JINSI YA KUPIKA KASHATA ZA NJUGU
- Kaanga njugu zako hadi ziive na kuwa kavu, kisha zitoe maganda yote ziwe nyeupe. …pepeta ili kuyatoa maganda kirahisi na kisha uzivunje vunje kiasi.
- Chukua sukari uchanganye na maji uichemshe mpaka iwe nzito ..
- NB uwe mwepesi wa kuipika haraka na kuepua ili isiwe nyeusi ….ongezea unga wa iliki.
- kisha chukua njugu zako mimina katika sukari iliyoyeyushwa ….
- Koroga koroga kwa mwiko mpaka ile sukari ikauke na kushikana vizuri na njugu
- Kisha mimina haraka katika sinia iliyopakwa samli kidogo na utandaze
- kabla ya njugu kupoa kata kata umbo upendalo. Ziache zipoe ili zipate kuwa ngumu na zitakuwa tayari kuliwa.