Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 4

Estimated read time: 3 min
JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU

       SEHEMU YA 4

        WHATSAPP 0655585220

         ZANZIBAR

ILIPOISHIA:
Baada ya yule paka kumaliza kulamba damu ya mama mkubwa iliyokua inavuja kutoka tumboni, alinirukia kifuani nilipokua nimelala pale kitandani. Kisha akanipa taarifa ya leo jioni KUNA ZAWADI NZURI ATANILETEA!!!
TUSONGE PAMOJA SASA:
Alivyomaliza kuzungumza tu yale maneno aliyeyuka(potea kimaajabu) palepale, nikabaki mwenye majonzi na huzuni kubwa, kwakweli nilikua siamini kabisa kama haya yanayonitokea ni ya kweli ama niko usingizini, nilihisi mungu ameamua kunionea mimi tu.
Kila kukicha nilikua ni mwenye kuomba msaada kutoka kwake hali hii iondoke, ila inatokea kinyume na kuwa afadhali ya jana, wakati nikiwa nimezungukwa na msongo mzito wa mawazo pale kitandani.
Mara macho yakaanza kuniwasha, kila nikitaka kusogeza mkono siwezi, huku macho yanazidi kuwasha ile mbaya, nikajikuta najitahidi sana kuyafunga kwa kuyakandamiza na kuyafungua ili nifanye kama kuyakuna lakini bado!!!, mpaka machozi yakaanza kunitoka, sasa ile nageuza uso wangu pembeni nilishtuka sana!!!
Ni mama yangu niliyekua namuona, amevalia nguo nyeupe, na yeye machozi yanamtiririka huku kilio kikali kikawa kinamtoka. Sikuelewa kabisa kipi kilichokuwa kinamliza mama yangu.
Alilia sana, sana sana yani!! Mpaka nguvu zikamuishia akaanguka chini na kuanza kugalagala pale chini kwenye michirizi ya damu iliyobakia. Nikajikuta nami machozi yanazidi kunitoka, ilinihuzunisha sana kwa kweli!
"Naomiii..... Naomii, Naomi mwanangu! Naomba unisamehe sana binti yangu!!".Mara mama akaanza kulalamika, nikaacha kulia na kumsikiliza
"..... Yote ni kutosikiliza wazazi wangu, niliambiwa mimi nisije kuolewa na baba yako ila nilikaidi ushauri, Ona sasa yalonikuta! Ona yanayowakuta wanangu!!! Daaaah!!! Mungu saidia wanangu hawa jamani!!!".
Nikapata picha nyingine hapa, kwamba kumbe mama na yeye wazazi wake walimkataliaga kuolewa na baba ila yeye akakataa ushauri huo na kuamua kufata nafsi yake. Leo hii mama amekua anajilaumu.
.....
Wakati mama akiwa anajilaumu pale chini, mara yule paka nae akatokea palepale, safari hii yule paka yupo katika umbile kubwa ( la mfano wa binadamu).
Alikua anatisha sana, mdomo wake yule paka umelowa damu, huku anamtumbulia macho, macho makali sana.Mama akawa anarudi kinyume nyume huku analalamika....
" Usinitafune tena tafadhali, naomba usinitafune!!!"
Inamaana huyu paka alimtafuta mama??!, Nilijiuliza bila kupata jibu. Mara baba akawa anaingia kwa kasi sana chumbani.
Hakuonekana mwenye kuwaona kabisa wale ninaowaona mimi (yani yule paka na marehemu mama), akaja moja kwa moja akaniinua kitandani pale nilipokua nimelala kisha tukatoka nje kwa kasi sana.
Usoni alionekana anavujwa na jasho sana baba yangu, huku macho yakionesha ni mtu mwenye huzuni kubwa na aliyepoteza matumaini.
Alinihamishia chumba kingine, kisha akaniweka kitandani....
"Usijali mwanangu Naomi, haya yote yatakwisha ni majaribu ya M/mungu tu!, ngoja nikakuletee chakula na baadae kidogo polisi watakuja, kuna uchunguzi kidogo wanataka waufanye!!". Baba alizungumza lakini kwa kumuangalia tu, inaonesha anatoa maneno ila ubongo wake unawaza mengi zaidi ya anayotoa.
Baba alienda akanichukulia uji kisha akanipa, baada ya hapo akaniaga akaniambia hatochelewa kurudi, ukizingatia pia dada Mwajuma tuko nae pale kwahiyo atakua ananingalia huku akiendelea na shughuli zake.
***
Nililala pale kitandani mpaka usingizi ukanichukua, kuja kushtuka giza limeshaingia, mara naona kama wanaume wawili wamesimama pembeni yangu.Akili ikanijia ni wale mapolisi alioniambia baba.
Kidogo, yule paka naye akatokea kati yao, baada ya mawenge ya usingizi kukaa sawa, kumbe wale wanaume nao si watu bali ni mapaka!!!, Nilishtuka!.
" Usishtuke Naomi!! Usishtuke!!! Nimekuletea ile zawadi niliyokuahidi mchana!!!". Yule paka mwenye sauti ya kike (wa katikati)aliongea.
Kisha akaendelea...
"...... Najua wewe ni msichana bikra!!!, Nimeleta hawa wanaume waje wakutoe bikra yako siku ya leo, NA HII ITATUONGEZEA NGUVU KWENYE KAZI ZETU!! Ahahahhhhhhhh!!", Alimalizia na kicheko.
Tobaa, yani sijawahi kukutana na mwanaume hadi umri huu na leo nahitajika niingiliane na mapaka watu, nikijiangalia sijiwezi kwa chochote yani!!.
***
JE NINI KITAENDELEA KATIKA MKASA HUU?? JE, NAOMI ATAINGILIANA NA MAPAKA??
USIKOSE SEHEMU TAMU IJAYO!!!

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.