RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA KUMI.
MTUNZI : ALEX KILEO..
______________
ILIPOISHIA
______________.
Sajenti Minja akaona njia sahihi ya kujiokoa ni
kuingia chini ya uvungu wa gari, akaingia,
Kayoza hakumuona.
kayoza alipomaliza kumnyonya yule
askari, akamuona Omari kashika bastola
anachungulia chini ya gari, Kayoza kama mshale, akalisogelea lile gari,
kisha akalibeba juu, akalitupa umbali mrefu.
Alikuwa na nguvu
kwelikweli, kama mashine au
mnyama mkubwa.
Baada ya kurirusha gari, akawa anamsogelea
Sajenti Minja aliyekuwa amelala chini huku akiwa amekata tamaa.
Kayoza alipomfikia,
akamkamata Sajenti Minja mabega
na kumnyanyua juu, Sajenti Minja akawa kama ametundikwa.
Kayoza akamvuta karibu na kumkumbatia kisha akawa anaupeleka mdomo wake
shingoni kwa Sajenti Minja huku
meno ya Kayoza yakiwa tayari kumng'ata Sajenti Minja.
Sajenti Minja akafumba macho huku akiwa tayari amekubaliana na matokeo
____________
ENDELEA..
____________
Kayoza akaingiza meno kwenye
shingo ya Sajenti Minja na kuanza kumnyonya damu, ghafla
akamuachia huku akiwa anamuangalia kwa
mshangao.
Kayoza akamuangalia
Sajenti Minja kwa dakika kadhaa. Akamfuata tena na kumshika kichwani Sajenti Minja huku akimgeuza geuza kichwa kumuangalia kama mtu anayemjua, kisha akamuachia na kugeuka nyuma huku akianza kuondoka jirani na Sajenti Minja.
Alipopiga hatua mbili tú ghafla akaanguka chini akapoteza
fahamu.
Sajenti Minja aliendelea kuganda tu,
huku yanayomtokea akihisi labda
huenda ni ndoto. Baada ya kumuona Kayoza ameanguka, sasa akawa kama
kagutuka, akatoka mbio kuelekea
eneo ambalo litakua ni salama kwake, na njia aliyokua anaelekea ni ile iliyokuwa inaelekea barabarani.
Alikimbia huku kila dakika akigeuza
shingo kuangalia kama Kayoza anamfuata
kwa nyuma, huku jeraha lake la
shingoni kalifunika na kiganja cha
mkono.
Alipowapoteza kabisa
machoni kwake, akagutuka, kisha
akaingiza mkono mfukoni, akatoa
simu, akatafuta namba anayoijua
yeye, alafu akapiga, akaonekana
kukunja sura
"hili eneo gani, hata
network hakuna?" Sajenti Minja aliongea peke yake kisha akairudisha simu
mfukoni, akakimbia kama dakika saba hivi,
ndio akaiona barabara kwa mbali.
Akajitahidi kuongeza mwendo hadi akaifikia.
Alipifika alikuwa anahema haraka haraka huku kila muda akiangalia njia aliyotokea.
Magari mawili ya mwanzo alipoyasimamisha
yalimpita, ni kutokana na hali
aliyokuwa nayo, vidonda, damu
ilimtapakaa karibia eneo lote la
mwili wake na pia eneo alilokuwepo lilikuwa linatisha na kingine cha ziada ni kwamba hakuvaa sare za polisi,
"mh....hapa nisipotumia
akili naweza kulala huku huku" Sajenti Minja alijisemea peke yake.
Gari la tatu
lilikuwa Toyota prado, na
ayelikuwa anaendesha ni mwanamama na
siti ya pembeni yake alikaa
msichana ambaye nadhani alikuwa ni mwanaye.
Sajent Minja akaichomoa
bastola yake kiunoni, kisha akawa
ameilenga ile gari na akitoa amri
isimame, yule mama akaisimamisha
huku akionekana ana hofu,
"mnaelekea wapi?" Sajenti Minja
akawauliza.
"singida mwanangu"
yule mama akajibu huku akitetemeka.
Sajenti Minja akawaonyesha kitambulisho chake,
ndipo hofu ikawatoka, kisha
akawaomba msaada, wakamkubalia,
akajipakia katika gari na kisha wakaishia
*****************
Baada ya Sajenti Minja kuondoka eneo la tukio,
ilichukua mda kama wa dakika tano
kayoza kupata fahamu.
Alishtuka akamkuta Omary yuko pembeni yake,
"mapolisi wameenda wapi?" Kayoza ndio
lilikuwa swali lake la kwanza kumuuliza
Omary,
"umewaua" Omary akajibu na kumfanya Kayoza ashangae,
"Mimi nimewaua?" Kayaza aliuliza kwa mshangao,
"Ndio, si hapo wamelala" Omary alijibu huku akiwaonyeshea kidole Askari waliikuwa wamekufa,
"na Denis nae kaenda wapi?" Kayoza akauliza
tena.
Hapo wote wakashtuka,
wakaenda kuingalia gari waliyokuwa
nayo lakini hawajamkuta, ndipo Omary akakumbuka kuwa aliporejewa na fahamu pembeni yake kulikuwa na mtu, ndipo alipohisi huyo mtu atakuwa Denis.
Wakarudi mpaka eneo la mwanzo, masikini ya mungu, walimkuta
Denis Paul Simiwe, akiwa amelala
huku damu zikiwa zimeganda kwenye
pua na midomo yake.
wote wakajikuta machozi yanawatililika mashavuni.
"Tuondoke, hili eneo sio salama" Omary alimtahadhalisha Kayoza,
Wakachukua kitambulisho cha Denis
kama kumbukumbu ya jamaa yao,
kisha wakabeba mabegi yao, wakawa
wanaelekea barabani.
walipofika barabarani
walikaa kama nusu saa, wakaiona
gari ndogo inakuja na aliyekuwa anaendesha ni mzee mmoja wa makamo.
Omary alisimama katikati ya barabara na kuipungia
mkono ile gari, ikasimama,
"shikamoo mzee"
wakamsalimia kwa pamoja,
"marhaba waheshimiwa" Mzee makamo aliwaitikia.
"mzee tunaomba
Lifti" Omary akasema katika sauti
tulivu,
"mnaelekea wapi?" Mzee wa makamo akawauliza,
"tulikuwa tunaenda
tanga, ila hata ukitufukisha eneo
lenye usafiri tutakushukuru" Omary akajibu,
"vizuri, hata mi naelekea
Tanga, mbona mko katika hali hiyo?"
yule Mzee wa makamo akauliza baada ya kuwaona wana damu katika baadhi ya sehemu mwilini,
"tumepata
ajali"Omary akajibu huku akijifuta damu shavuni,
"poleni sana,
ingieni twendeni" Mzee
akaongea.
Wakaingia, safari ikawa
inaendelea, mwendo kama wa nusu
saa hivi, yule mzee kupitia kioo cha
juu mbele, alishuudia kitu,
kinachoendelea kwenye siti ya
nyuma, ambayo walikaa wakina
kayoza, akapata mshtuko,
akapunguza mwendo wa gari, kisha akageuka ili kuhakikisha kama ni kweli au kioo kinamdanganya?..
******ITAENDELEA******