Mahitaji:
🔗Mchele wa basmat au kawaida 🔗Mafuta vijiko 4 vya chakula
🔗Njegere zilizowekwa ktk fridge 🔗Kitunguu maji 1 kilichokatwakatwa 🔗Kitunguu thoum kilichopondwa kijiko 1 🔗Karoti 1 kubwa
🔗korosho robo kikombe
🔗maharage ya kijani
🔗Majani ya kotmir kiasi
🔗Mdalasini vijiti 3
🔗Chumvi
JINSI YA KUPIKA.
1.Chemsha maji kisha yaweke pembeni 2.Tia mafuta yakipata moto kaanga vitunguu maji vikibadilika rangi tia vitunguu thoum.
3.Tia mchele na mahitaji yote na maji uliochemsha kisha acha wali uchemke uwive utakua unaugeuza geuza kama wali wa kawaida
4.Wali ukisha kaukia tia katika oven au mkaa ukauke vizuri baada ya robo saa utakua tayari. Kula na michuzi ya aina zote,mboga nk