Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JINSI KITAMBI KINAVYO VURUGA HOMONI NA KINAWEZA KUKUFANYA MGUMBA

Narudia tena maneno yangu Usijilinganishe na mtu kila mtu mafuta ya ziada yanamdhuru katika namna tofauti. Wengine wanakilo nyingi na wanazaa kama kaw

 Narudia tena maneno yangu Usijilinganishe na mtu kila mtu mafuta ya ziada yanamdhuru katika namna tofauti. Wengine wanakilo nyingi na wanazaa kama kawaida ila wengine kitambi kinakuwa kama Kigingi cha wewe kupata mimba.

.

1. Mwili huwa unakiwango maalumu cha mafuta ya ziada huitwa Fat threshold level. Endapo ukizidisha kiwango hicho mafuta hayo ya ziada yanatambuliwa na mwili kama Kivamizi.

2. Kinga ya Mwili huamka na kuanza Kupambana na Mafuta ya ziada. Mfano Mafuta yanapokaa juu ya Ini yanaumiza Ini kutokana na Ini kuyabaini kama sio sehemu ya Ini.

3. Kitambi husababisha mwili kuzalisha ishara ya mapigano ya kinga ya mwili dhidi ya adui yaani Mafuta ya ziada viashiria hivi huitwa Inflammatory Mediators kama TNF, IL1 IL 6, Thromboxane A2 hizi Huleta mapigano sugu mwilini na Mwili Kuchemka na Kudhurika systemic Low grade chronic inflammation.

4. Watu wengi Wenye Kilo nyingi Miili yao Kwa ndani Iko na mtafaruku mkubwa sana. Ukiwapima Viashiria kuwa mwili ndani uko kwenye mtafaruku/mapigano Hauko Tulivu unaweza kushangas mashine hazisomi.

5. Hali hio Chronic systemic inflammation husimamisha ovari za mwanamke kukomaza mayai kila mwezi. Unaweza ukawa unapata Hedhi lakini hakuna yai linalotoka Tunaita Anovulatory Cycle. Hii hali ikidumu Unashangaa hedhi inaanza kukata ukipima unaonekana hata kiwango cha mayai Kimeshuka na hata wakisisimua na sindano au vidonge mayai hayatoki Umepata Diminished Ovarian Reserve. Ukizubaa Unashangaa Hedhi Haitoki kabisa Kabisa kwa miezi kadhaa mwisho wa siku Inakata kabisa hata kabla ya miaka 40 kufika hio tunaita PRIMARY OVARIAN INSUFFICIENCY au Early Onset Menopause hatimaye HEDHI INAENDA KABISA.

.

6. Mbali na Unene Uliokithiri Pombe, vyakula vyenye sukari nyingi, vyakula vya kukaanga, Uvutaji sigara, Shisha, Bangi na madawa mengine Huongeza Ukubwa wa Tatizo Lako linalosababishwa na UNENE.

Inakuwaje sasa Unakilo nyingi HALAFU UNAAMUA KUTUKOMESHA KWENYE KUJIPIGILIA MISOSI NA VINYWAJI KUMWAGILIA MOYO?

.

Kula kiafya Mwanamke Mbali na Kupata mtoto unatakiwa uishi bila magonjwa hapa duniani na hio ndio raha kubwa duniani kuliko hata huyo mtoto anayekufanya UJIKATIE TAMAA..

.

JITAHIDI USOME KITABU CHANGU KIPYA CHA SAYANSI YA HOMONI NA UGUMBA MUDA SIO MREFU KITAKUWA SOKONI

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.