Notification texts go here Contact Us Buy Now!

AFTER DEATH (BAADA YA KIFO) SEHEMU YA 01

AFTER DEATH (BAADA YA KIFO)-01
MTUNZI-ANDREW SHADU
TELL-0677884981
EMAIL-andrewshadu44@gmail.com

UTANGULIZI....
Fred na Emile ni vijana wawili waliokuwa marafiki walioshibana licha ya kwamba walikuwa wanatoka kwenye familiya mbili tofauti zilizotofautiana sana kiuchumi. Fred alikuwa anatokea kwenye familiya ambayo ilikuwa imejaaliwa kuwa na maisha mazuri kwasababa baba yake alikuwa ni mkurugenzi wa mambo ya ndani nchini Tanzania wakati mama yake alikuwa ni mwalimu wa chuo kikuu cha dar-es-salaam(UDSM), Fred na wazazi wake walikuwa wanaishi maeneo ya Masaki ambapo wengi wao waliokuwa wanaishi hayo maeneo walikuwa ni matajiri. Tangu Fred anazaliwa hadi anafikisha umri wa miaka kumi na saba hakuwahi kupitia shida yoyote kwasababu wazazi wake walikuwa na uwezo wakumpatia kitu chochote alichokuwa anahitaji, Elimu yake yote ya msingi alisomea katika shule za masista ambazo zilikuwa ni za gharama kubwa lakini elimu yake ya secondary alisomea katika shule ya Tusiime iliyopo maeneo ya Tegeta ambapo ndipo alipokutana na rafiki yake kipenzi aitwaye Emile. Mara nyingi urafiki wa kweli huwa hauangalii tofauti yenu ya maisha au kipato bali urafiki wa kweli unakuja endapo njota zenu zinaendana. Emile alikuwa anatokea kwenye maisha ya hali ya duni sana, Maisha ambayo hata yeye hakuyapenda hata kidogo, Kula kwao kulikuwa ni kwa tabu sana hata kuvaa kwao kulikuwa ni kwa shida, Emile alianza elimu yake ya msingi katika shule ya Mtakuja iliyopo kitunda ndani ndani ambako ilikuwa ni mbali kutokea kwao maeneo ya Ulongoni ambako alikuwa anaishi, Licha ya hali ngumu ya maisha ambayo Emile alikuwa nayo lakini Emile alijaaliwa kipaji cha kusoma kwani alikuwa ni kijana ambaye alikuwa anafanya vizuri sana kimasomo Tangu alipoanza darasa la kwanza kwenye shule ya msingi mtakuja, Emile hakuwahi kushika nafasi ya pili kwani kila mitihani ambayo ilikuwa inafanyika ndani na nje ya shule yao alikuwa anashika nafasi ya kwanza hadi jina lake likawa gumzo kwenye baadhi ya shule ambazo zilikuwa zinaushindani na shule ya msingi mtakuja, Kipaji cha kusoma cha Emile ndio kilichomvutia mzungu mmoja aitwaye Jenkison aliyekuwa ni barozi wa marekani nchini Tanzania kumsomesha Emile kwenye shule ya Tusiime ambayo napo aliendelea kufanya vizuri. Yule mzungu alipanga kumsomesha Emile hadi elimu ya chuo kikuu kwani alivutiwa na utashi wa Emile, Wazazi wa Emile hawakufaidika sana na msaada wa yule mzungu kwasababu walipewa pesa kiasi ambazo hazikuwakidhi mahitaji yao japo waliona ni vyema mtoto wao asomeshwe na yule mzungu kwasababu ndio njia sahihi ya wao kuja kujikomboa kiuchumi siku za mbeleni. 
Fred na Emile walizoeana shuleni Tusiime kupitia Timu ya mpira ya shuleni apo kwasababu wote walikuwa ni wanafunzi waliokuwa wamejaaliwa kipaji cha mpira japokuwa Fred ndio alikuwa anajua kucheza zaidi kwasababu kwa uchezaji wake alifananishwa na wachezaji wengi sana maarufu kama vile Lionel messi na Mohammed Salah, Urafiki wao ulizidi kukua hadi kimasomo licha ya Fred kutokuwa vizuri darasani. Fred hakuwaza sana kuhusu jambo la Elimu kwani alijua hata akifeli wazazi wake watamtafutia kitu cha kufanya lakini kwa Emile hali ilikuwa tofauti kwasababu yeye kusoma kwake kote kulikuwa kunategemea elimu ije kumkomboa kimaisha, Hakutaka kabisa kuichezea elimu ndio maana alikuwa anasoma kwa bidiii ili aje kupata kazi nzuri ambayo itamkomboa kimaisha yeye na wazazi wake....."Emile rafiki yangu mitihani ya mwisho ndiyo inakaribia, Baba ameniambia nijitahidi nipate japo alama za kupata cheti, Najua rafiki yangu hauwezi kuniangusha utanisaidia kwenye chumba cha mtihani ili na mimi nipate cheti si ndio".....Aliongea Fred ambaye alikuwa anapata chakula cha mchana na Emile kwenye meza moja iliyopo sehemu ya kulia chakula, Emile alimtazama Fred kisha akaahidi kumsaidia kwasababu ni rafiki yake waliyeshibana tangu wanaanza kidato cha kwanza. Emile alikuwa na uhakika mkubwa wa kufaulu ule mtihani wa mwisho wa kidato cha nne kutokana na uwiano mzuri aliokuwa nao Tangu alipoanza kidato cha kwanza hata walimu wake walilifahamu Hilo. Shule nzima ya Tusiime ilikuwa inamtegemea Emile na baadhi ya wanafunzi wengine wachache ndio walitangaze jina la shule kwani kwa kipindi hicho ushindani baina ya shule za jirani ulikuwa ni mkali sana, Kila shule ilitaka itoe mwanafunzi ambaye atakuwa kinara kuliko wanafunzi wote wa shule pinzani, Emile ndiye aliyekuwa anategemewa kuwapiku wanafunzi wengi kutoka shule mbali mbali licha ya ushindani kuwa mkubwa kwasababu kwenye mitihani ya interschool (mitihani ya shule mbali mbali) ni siku moja tu pekee ambayo Emile alishika nafasi ya pili. 
Miezi ilikatika, Siku zikapita, Masaa yakasonga mbele hatimaye siku za mitihani ya kumaliza kidato cha nne zikakaribia lakini wiki mbili kabla ya mitihani hiyo kufanyika Emile alishikwa na homa kali sana, Mwanzoni ilichukuliwa kama homa ya kawaida lakini zilivyobaki siku mbili kabla ya mitihani kufanyika homa ya Emile ilipanda zaidi ikabidi akimbizwe kwenye hospitali ya muhimbili kwa ajili ya matibabu ya haraka zaidi, Wazazi wa Emile mzee chande na mama monge walilia sana baada ya kupewa taarifa za mtoto wao kulazwa kutokana na homa kali ambayo ilikuwa imemshika siku chache kabla ya kufanya mitihani ya mwisho ya kumaliza kidato cha nne. Fred pia alilizwa na mengi sana, kwanza Emile alikuwa ni rafiki yake mkubwa sana pale shuleni, pili Emile ndiye mtu pekee ambaye alimpa ahadi ya kumsaidia kwenye chumba cha mtihani ili na yeye afaulu na kupata alaza za kupewa cheti, Yule mzungu( Jenkison) ambaye alikuwa anamsomesha Emile alisikitishwa na zile taarifa japo kipindi hicho alikuwa nchini Marekani lakini aliamua kutuma pesa za gharama zote za matibabu. Hatimaye siku pendwa ya kufanyika mitihani iliwadia Emile akiwa bado yupo kitandani hoi hajiwezi kwasababu ya homa kali. Kutokana na Sheria za mitihani ya mwisho ilibidi Emile afanye ile mitihani akiwa kitandani japo alikuwa hawezi hata kuandika, Alijitahidi kutaja majibu kwasababu kuna mtu alikuwa anamsomea swali kisha yeye anajibu huku akihisi maumivu makali sana, Polisi wakusimamia udanganyifu hakuwa mbali kwani alikuwa anamlinda Emile hadi siku ya mwisho ya mitihani. Wiki moja mbele baada ya ile mitihani kupita Emile alirejewa na afya yake upya, Emile alilia sana kwani alijua kabisa hawezi kuifaulu ile mitihani kutokana na jinsi alivyoifanya pindi alipokuwa anaumwa. 

Itaendelea....
AFTER DEATH (BAADA YA KIFO) ni simulizi ambayo ina mengi yakujifunza.

Usikose muendelezo.

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.