Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MADHARA 10 YANAYOTOKANA NA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO

Athari kuu 10 zinazoweza kusababishwa na vidonge hivyo ni pamoja na kutokwa na damu ukeni baada ya hedhi ya kawaida. Kwa mujibu wa wataalam wa mpango huo, athari hiyo huweza kuwapata asilimia 50 ya wanawake wote wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango.

*MADHARA 10 YANAYOTOKANA NA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO*

**

Athari kuu 10 zinazoweza kusababishwa na vidonge hivyo ni pamoja na kutokwa na damu ukeni baada ya hedhi ya kawaida. Kwa mujibu wa wataalam wa mpango huo, athari hiyo huweza kuwapata asilimia 50 ya wanawake wote wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango. Hali hii huweza kuwatokea ndani ya miezi mitatu baada ya kuanza matumizi ya dawa hizi. Kwa ujumla, hali hiyo huweza kukoma kwa zaidi ya asilimia 90, pindi mwanamke anapoanza kutumia pakti ya tatu ya dawa hizo katika kipindi hicho cha kutokwa damu ukeni. Mwanamke anapotokewa na hali hiyo kwa mfululizo wa siku tano au zaidi baada ya kumaliza siku zake za kawaida za hedhi, anashauriwa kuwasiliana na mhudumu wa afya wakati akiendelea kutumia dawa hizo.

Athari ya pili, ni kujisikia kichefuchefu. Mara nyingi hali hiihumtokea mwanamke mwanzoni tu baada ya kuanza kumeza vidonge vya uzazi wa mpango, ingawa hali hii inaweza kukoma baada ya siku chache. Inashauriwa pia kwa mwanamke anayepatwa na hali hii ya kichefuchefu kuwasiliana na mhudumu wa afya kama ataona hali hiyo inazidi.

Matiti kujaa au kuwa na maumivu, ni athari nyingine inayoweza kusababisha na matumizi ya vidonge hivyo. Hali hii huweza kumpata baada ya kuanza kutumia vidonge hivyo, na huweza kukoma ndani ya wiki moja tu. Hata hivyo, inashauriwa kwamba ikiwa matiti hayo yatatokwa na uvimbe au maumivu yasiyoisha, ni muhimu kutafuta tiba kwa wahudumu wa afya, ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya kinywaji chenye kafeini (caffeine) na chumvi na kuvaa brauzi isiyobana matiti.

Maumivu ya kichwa ni athari nyingine inayoweza kumtokea mwanamke, ingawa pia kuumwa kichwa kunaweza kuwa na dalili za magonjwa mengine. Hata hivyo, kama itatokea maumivu hayo ya kichwa yakaanza tu mara baada ya kumeza vidonge hivyo, hiyo itakuwa ni dalili ya athari mojawapo na ni vyema kutoa taarifa kwa mhudumu wa afya.

Vidonge vya uzazi wa mpango huweza pia kuongezeka uzito wa mtumiaji, ingawa tafiti nyingine zimeshindwa kuthibitisha uhusiano kati ya vidonge hivyo na mabadiliko ya uzito wa mtumiaji. Aidha, baadhi ya wanawake hupatwa na tatizo la maji kuganda kwenye matiti na maeneo ya nyonga baada ya kutumia vidonge hivyo.

Mabadiliko ya hisia huweza pia kumtokea mwanamke anayeanza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Inashauri kwamba pindi mwanamke anapoona dalili hii, ni muhimu kumjulisha mhudumu wa afya ili kuweza kujadili ni jinsi gani ataweza kutumia dawa hizo, kwa sababu dalili hii ni mbaya kiafya kwa mtu mwenye historia ya ugonjwa wa Kushuka Moyo (Depression).

FAHAMU KWA KINA MADHARA YA NJIA ZINGINE ZA KUZUIA MIMBA NA JINSI GANI ZINAATHIRI MWILI WAKO HASA KWA WANAWAKE.

Athari nyingine ya dawa hizi ni kutokwa na uchafu ukeni. Baadhi ya wanawake, mara tu baada ya kutumia vidonge hivi hutokwa na uchafu ukeni, ikiwa ni pamoja na kupatwa na uwezekano wa kupungua au kuzidi kwa ute wakati wa tendo la ndoa. Ni muhimu sana mwanamke anapobaini dalili hizi, kuonana na mhudumu wa afya ili kubaini kama hali hiyo imesababishwa na athari ya vidonge au kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa.

Wanawake wengine huweza kujikuta wakikosa siku zao za hedhi baada ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Ingawa ugonjwa wa msongo wa mawazo (stress), magonjwa, mchoko wa safari unaweza kusababisha hali hii, lakini inashauriwa kupima kama mtu amaepatwa na ujauzito hata kama anatumia vidonge hivi kama itatokea kukosa hedha katika mazingira tata.

Kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni athari nyingine inayoweza kumkuta mwanamke anayetumia vidonge vya uzazi wa mpango kutokana na vichocheo vilivyomo ndani ya dawa hizo, ingawa pia magonjwa kama ya kisukari, shinikizo kubwa la damu na kadhalika yanaweza pia kuchangia tatizo hilo.

Athari ya 10 na ya mwisho kwa wanawake wanaotumia vidonge hivyo, ni mabadiliko ya taswira ya kitu anachokiona mbele yake, hasa kwa wanawake wanaovaa miwani ya macho. Kwa kuwa macho ni moja ya eneo muhimu la ufahamu kwa mwanadamu, hali hii inapowapata wanawake, inashauri kuonana mara moja na daktari wa macho pindi tu dalili hizi zinapoanza kujitokeza.



NDIO MAANA UKAKUTA MWANAMKE ANAETUMIA HUDUMA HII ANAKUWA ANA VIMBA MWILI TUU

*  *

*KUBEMENDA MTOTO* ➡Hii ni hali ya mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwen...
SOMA ZAIDI UJUE UKWELI KUHUSU KUBEMENDA MTOTO

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.