Notification texts go here Contact Us Buy Now!

HEBU FUATILIA MKASA HUU WA KWELI WA MAISHA

Juzi kati hapa nilipokea ushuhuda wa Brother mmoja ambae pia alikuwa kama anaomba ushauri pia,anasema yeye ni mfanyabiashara mkubwa wa viatu kuna kipindi alimpiga mimba mschana mmoja hivi ambae walikuwa wanakaa nae mtaa mmoja,ki ukweli alisema kabisa kwamba katika maisha yake haikuwa malengo yake kuja kumuoa yule mschana wala kuja kuishi nae kwasababu alikuwa anamtumia tu kama starehe,lakini baada ya kuwa amempiga mimba ilibidi kwao na huyo binti wamwite kisha wakamkalisha kitimoto,kulikuwa hakuna namna tena zaidi ya kukabidhiwa yule binti na kwenda kuishi nae.

Brother anasema kwamba hakumpenda huyo binti kabisa kutoka moyoni,alimchukua tu na kuanza kuishi nae kwa kumforce,anasema kabisa kwamba yeye hakutaka kuanza maisha ya mke na mme ghafla ghafla,alijaribu kufanya kila visa na visa ili binti arudi kwao akaombe msamaha ikiwezekana kama mimba atatunzia akiwa kwao lakini ilishindikana.

Brother anasema kwamba yule binti pamoja na yote alikuwa ni mtu wa kusali,hata alipokuwa akimkorofisha vipi na kumtukana mwisho wa siku yule binti alilia akapiga magoti na kusali kisha kuendelea na maisha kama kawaida.

Jamaa alikuwa mpenda pombe,starehe na anasa zingine,alirudi nyumbani kwa kuchelewa na muda mwingine amelewa ilimradi tu kumfanyia visa binti yule lakini binti alikuwa mgumu sana na mvumilivu licha ya ujauzito alionao,maisha yake yeye ilikuwa ni kulia na kushukuru tu kwa Mungu pindi anapoumizwa.

Lakini kitu cha kushangaza ambacho alikisema brother wetu ni kwamba tangu aanze kukaa na yule binti biashara yake ilikuwa inauza sana,hela alikuwa anapata kiasi kwamba tangu aanze biashara ile ya viatu alikuwa hapati kama anavyopata kipindi hicho,mzigo ulikuwa haukai na ilifikia kipindi mpaka akanunua na kiwanja na akaweka na msingi na matofari akafyatulisha kibao,pamoja na hayo anasema roho yake haikuwahi kuridhika kabisa kuishi na mschana ambae yey alitaka tu kumtumia kwa starehe na wala sio kama mke na mme kwahiyo manyanyaso kwa binti yule hayakuisha bali aliyaendeleza.

Anasema miezi tisa ilitimia,hatimae binti yule alizaa mtoto wa kiume,licha ya visa na misukosuko yote mwanamke yule alizaa salama kabisa,basi huduma kwa mtoto zikaanza ili maisha ya mtoto yastawi.

Lakini sasa toka mkewe huyo ajifungue ndugu yetu huyu anasema ndio kama na yeye tabia ya starehe alikuwa ameifungulia,kurudi nyumbani saa saba au saa nane lilikuwa ni jambo la kawaida sana,hakujali kama mkewe anamtoto au la..!,swala la kumpiga yule mwanamke kwake lilikuwa la kawaida,kosa kidogo au akienda kinyume kidogo basi kipigo kitakuwa ni sana.

Alisema alifanya yote hayo ilimradi tu yule binti aondoke ili amlete mwanamke aliempenda yeye na ambae alitaka ndio waishinae kama mke na mume aje akae.

Wanasema siku zote hakuna marefu yasiyo na nncha,siku moja binti yule alipanga mipango na dada yake ambae anaishi mkoa wa Mtwara akamuomba aende kuishi kwake angalau kwa miezi kadhaa apumzike na mateso ya vipigo.

Hakutaka kwenda kuishi kwao ambapo ni hapa hapa dar kwasababu kwao walikuwa wameshamchukia na kumkataa kabisa na hawakutaka kumuona kwasababu ya kubeba ule ujauzito kinyume na matarajio ya wazazi wake ambao walipanga wamsomeshe afike mbali.

Kweli mwisho wa siku alitoroka na kuelekea mtwara akiwa na mtoto mdogo wa miezi miwili,Brother anasema kwamba alihisi sasa ni wakati wake wa yeye kufurahi na kufanya uamuzi bora wa kumleta mke yule ampendae,maana akiangalia biashara zinazidi kuongezeka na kunoga,maisha safi,tayari anakiwanja na muda wowote jumba linaanza kuporomoshwa kumbe hayo yote alijidanganya.
Anasema anakumbuka kitu kimoja kwamba baada ya siku tatu toka mwanamke yule aondoke,alikutana na kikaratasi kilichokuwa na ujumbe wa maneno kutoka kwa yule mwanamke ukisema"Nimejitahidi sana kukuombea ubadilike mume wangu,niliomba sana Mungu akukuzie biashara yako,niliomba sana Mungu akuinue katika maisha yako lakini nilionekana kama mbwa kwako,sawa mimi naondoka na kukuachia maisha yako Mungu akulinde na azidi kukubariki"
Brother anasema baada ya kuusoma ujumbe ule alikichana chana kile kikaratasi na kukitupa kisha akafyonza huku akisema"Shatani mkubwa wewe bora umeondoka huna msaada wowote kwangu"...Hakujua kama sasa amepalilia miiba shambani na kuitupa kwenye njia yake.

Brother anasema katika maisha yake alitaka kuwa na mke yule ambae alimtaka yey,anasema alikuwa anataka yule mwanamke ambae hata kama wanatoka bar kwenda kunywa basi awe nae na awe mnywaji,tofauti na yule yeye alikuwa hatumii kilevi chochote zaidi ya kusali tu.

Ulipita mwezi mmoja tu toka aondoke yule mwanamke,anasema baada ya kumaliza kuongea na familia ya binti yule kuhusu kutoloka kwa mtoto wao na mambo yote kukaa sawa hapo sasa ndio aliona ni wakati muafaka wa kuleta jiko jipya nyumbani kwake lile alilokuwa analitaka yeye,ki ukweli anasema alikuwa anampenda sana huyo mwanamke wa pili aliemleta na ndio alimtaka sana awe mke wake,kwasababu alikuwa mzuri na mwenye shepu nzuri tofauti ya yule wa kwanza,hata alipokuwa akitoka nae kwenda clab marafiki zake walimsifia kwa kuwa na mke mwenye shepu mzuri na mvuto.

Anasema baada ya miezi mitatu kupita toka yule mwanamke aondoke huyo mwanamke mpya aliemleta nae alidaka ujauzito,anasema ujauzito ule ndio kama ulifungulia mlango wa maisha magumu katika safari yake ya biashara,pesa ilikuwa ngumu kweli kwake,kwa siku anaweza akaenda akarudi na elfu 10 tu tofauti na zamani ambapo kwa siku alikuwa na uwezo wa kuuza hata laki mbili,alijikuta akili yake inawaka moto,akajikuta kila kitu anakuwa mkali na mawazo yakawa ndio mawazo.

Sasa ikawa badala ya kutumia pesa anayofanyia biashara akawa anatumia pesa ya akiba ambayo angeitumia katika mambo ya kujenga na kuendeleza maisha.Siku zilienda na miezi nayo ikaenda hatimae mke wake nae huyo wa pili alijifungua mtoto wa kike,ugumu wa biashara kila siku ulizidi kushamili pia familia nayo imeongezeka.

Mtoto wao akiwa na miezi miwili walijikuta sasa wanaanza kuuza vitu vya thamani vya ndani kama Tv,saboofa n.k angalau hata wapate hela lakini pamoja na hayo hela yenyewe walioipata ilipitiliza tu kwenye mahitaji ya nyumbani,ndipo siku moja alikaa na mke wake na hatimae mke alimshauri waende kwa mganga kutafuta dawa ya biashara.

Jamaa anasema kutokana na kuwa alikuwa amepigika sana hakutaka hata kufikiria mara mbili mbili alimuuliza mke wake kama anamfahamu mganga yoyote ambae angeweza kuwasaidia na ndipo mke wake akasema kwamba kuna mganga anamfahamu,walienda na wakaambiwa kwamba kuna mkosi ambao wametupiwa na yule mwanamke alieondoka na kuna dawa wamemezeshwa pia hivyo ili mkosi huo uondoke ilihitajika walete kuku saba ambao ni aina ya vinyonyoke majogoo.Basi jamaa bila kusita anasema alienda kutoa hela zote akiamini kweli huenda ni mkosi,alizichukua na kuanza kununua kuku wa namna hiyo ambao aliwapata kwa gharama kweli,baada ya hapo walirudi kwa mganga na mganga akawatengenezea dawa ambazo sharti ni kila siku kabla hajaenda kwenye biashara anatakiwa awe anazioga,jamaa anasema alifurahi akijua matatizo yameisha lakini kumbe mganga alikuwa muongo na pesa alikuwa ameshakula.

Anasema hatimae ilitimia miaka miwili ya mihangaiko toka yule mwanamke aondoke,alijaribu kumtafuta lakini hakufanikiwa,hatimae alianza kusikia fununu za harusi nyumbani kwa yule mwanamke wake wa kwanza,alipokuja kupeleleza aligundua kwamba ndoa ile ni ya yule mke wake wa kwanza aliemuona hafai kitu alijikuta roho inamuuma sana sana na alitamani hata aonane ya yule mwanamke angalau ndoa iailishwe warudi kama zamani lakini haikuwezekana kwani alikuwa bado yupo mtwara ambako ndio ndoa inatokea...........

 Watch out for part 02 this weekend......

USIKOSE

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.