Notification texts go here Contact Us Buy Now!

FURAHA YA KWELI NI IPI KATIKA MAISHA!!?

Bilionea Femi Otedola alipoulizwa kwenye interview, ya simu na mtangazaji wa radio, "Sir ni kitu gani unachokumbuka kilichokufanya uwe na furaha maishani?"

Femi alijibu:
"Nimepitia hatua nne za furaha katika maisha yangu na mwishowe nilielewa maana ya furaha ya kweli."

Hatua ya Kwanza ilikuwa ni kutafuta Mali na kulimbikiza. Lakini katika hatua hii sikupata furaha niliyoihitaji.

Nikaingia hatua ya pili ya kujinunulia vitu vya thamani. Lakini niligundua kuwa vitu vyote hivi vinakupa furaha ya muda tu ambayo haidumu.

Nikaingia hatua ya tatu ya kufanya miradi mikubwa. Ni katika hatua hii nilikuwa ninasambaza 95% ya diesel Nigeria yote na Africa Kwa ujumla. Pia nilikuwa mmiliki mkubwa wa vessel Africa na Asia. Lakini pia hapa sikupata furaha niliyokuwa nimeifikiria. 

Hatua ya nne ilikuwa ni kipindi ambacho rafiki aliniomba kununua wheelchairs Kwa ajili ya watoto walemavu. Walikuwa kama watoto 200 hivi. 

Baada ya kuombwa na rafiki yangu nilinunua hizo wheelchairs mara moja. 

Lakini pia aliniomba niambatane naye ili nikawakabidhi watoto zile wheelchairs. Nilijiandaa nikaambatana naye. 

Nikawagawia zile wheel chairs Kwa mikono yangu mwenyewe. Niliona furaha ikitawala kwenye nyuso za hawa watoto. Nikawaona wamekaa kwenye wheelchairs, wakizunguka na kufurahia. 

Ilikuwa ni kama wako kwenye picnic wakisherehekea ushindi wa bahati nasibu. 

NiIihisi furaha ya kweli ndani yangu. Nilipoamua kuondoka mtoto mmoja alinishika miguu yangu. Nilijaribu kujinasua taratibu lakini alinikazia macho akinitazama usoni.

Niliinama chini nikamuuliza, kuna kitu kingine unahitaji?

Jibu alilolitoa mtoto huyu sio tu kwamba lilinipa furaha bali pia lilinifanya nibadili kabisa mtazamo wangu juu ya maisha. Mtoto huyu alisema: 
"Ninakuangalia ili niikumbuke Sura yako, siku nikikukuta mbinguni niweze kukutambua na kukushukuru tena."

Je wewe utakumbukwa Kwa lipi utakapoondoka kwenye hiyo ofisi au mahali unapoishi? 

Je kuna mtu atatamani kuona uso wako tena siku za usoni? Nawatakieni siku njema

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.