Hadithi za mafanikio zina hamasa nzuri, lakini huwa ni hadithi za nyuma, huwa
tunaoneshwa watu hao walitoka sifuri na sasa wapo kileleni.
Hivyo hatuoni kila
hatua waliyopiga na namna walivyopambana na magumu waliyokutana nayo
kwenye safari hiyo.
Njia bora kabisa ya kupata hamasa ya kukusukuma kwenye safari yako ya
mafanikio ni kuzungukwa na wale ambao wanafanya sasa.
Wale ambao ndiyo
wanaanzia sifuri kama wewe na kwa pamoja mnakwenda kileleni.
Hapa chagua
watu ambao unaona kabisa wamejitoa ili kufanikiwa, watu ambao wapo tayari
kupambana na kung’ang’ana mpaka wafanikiwe, kisha ambatana na watu hao,
shikana nao.
Hawa ndiyo
watakaokuonesha wazi namna ya kuvuka changamoto mbalimbali,
kwa sababu hata wao wanazivuka.
Hawa ndiyo watakufundisha maana ya ung’ang’anizi, maana nao wanang’ang’ana.
Na unapochagua watu hao vizuri,
mafanikio ya mmoja wenu yanakuwa mafanikio yenu wote.
