MAANDAZI YA KUOKA (maandazi ya kupambia)
![]() |
MAHITAJI YA KUPIKA MAANDAZI YA KUOKA
- °unga wa ngano nusu
- °Siagi au blueband vijiko 2 vya mchuzi
- °Vanilla au hiliki ya unga kijiko 1 cha chai
- °Hamira ya chenga kijiko 1 chai
- °Chumvi 1/4 kijiko chai
- °Sukari kijiko cha mchuzi 1 1/4
- °Maji ya uvugu vugu kukandia au tui la nazi au maziwa
KUANDAA NA NA KUOKA MAANDAZI YA KUOKA
- Tia unga katika beseni kisha tia hamira, chumvi, sukari, vanilla, na siagi kisha changanya unga wako vizuri.
- Baada ya hapo tia maji kidogo kidogo na anza kukanda unga wako kanda kwa dakika 3 ila usiulainishe saana.
- Acha Kwa dakika kadhaa kisha kata na acha tena kidogo. ..paka mafuta katika chombo cha bati kisha panga maandazi yako na kisha paka tena mafuta juu ya maandazi na tia katika oven au jiko la mkaa kwa muda mchache maandazi yako yatakua tayari kuliwa.
NB:
- -uandaaji wake ni vilevile kama maandazi ya kawaida ya mafuta tofauti yake haya unayaoka tu.
- -kwenye kukata usifanye membamba sana kwani yakipoa yatakuwa magumu, hivyo ukate manene kiasi ili yawe laini
- -kama huna oven unapikia jiko la mkaa.
