MAHITAJI
Nanasi 1 kata toa maganda na ukatekate vipandevipande
sukari vikombe 2
ndimu vijiko 4 vya kula
maji kikombe 1
hiliki(ukipenda)
JINSI YA KUPIKA
1.Chemsha nanasi hadi likiwa laini lipondeponde
2.Tia sukari ktk sufuria na maji ukoroge mpaka iyeyuke
3.Iweke jikoni ichemke mpaka uone inanatanata ktk vidole tahadhali isiungue
4.Tia nanasi lako na maji ya ndimu changanya ,iwache ichemke kwa moto mdogo mdogo mpaka iwe nzito kama jam zengine kisha epua ,tayari kwa matumizi waweza kula na mkate,banzi au kwa biashara.
NB:- njia hii hii iliyotumika kupikia jam ya nanasi, unaweza kutumia kwa kupikia jam ya tunda lingine lolote kama embe, papai, tikiti, nyanya, strawberries, cherries n.k
Pia unaweza ukachanganya tunda zaidi ya moja mfano nanasi na embe, embe na passion, nanasi na passion n.k(vizuri zaidi upate matunda yaliyoiva vizuri)
-jam unaweza kuitumia kupaka ktk mikate, gundishie biskuti, paka ktk swissrole cake, kupaka ktk baadhi za keki kwa kugundishia pamoja, gandishia vileja vyajicho La ngamia.