Notification texts go here Contact Us Buy Now!

Nini husababisha Muwasho Sehemu za Siri?

(1) Maambukizi ya Fangasi Ukeni (2) Ugonjwa wa kuvimba uke (Vulvovaginitis) (3) Kuvimba Uke baada ya hedhi kukoma (Postmenopausal Atrophic Vaginitis) (4) Maambukizi ya Trikomonasi (Trichomonas Infection) (5) Ugonjwa wa Minyoo (Pinworm Infection) (6) Inflamesheni ya Urethra (Urethritis) (7) Genital Warts (8) Saratani ya sehemu ya nje ya Uke (Vulvar Cancer) (9) Ugonjwa wa Wasiwasi (Generalized Anxiety Disorder) (10) Ugonjwa wa Sjogren (Sjogren's Syndrome) (11) Kisukari
Nini husababisha Muwasho Sehemu za Siri za Mwanamke?









(1) Maambukizi ya Fangasi Ukeni (Vaginal Yeast Infection)

Ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosababishwa na fangasi waitwao Candida. Dalili kuu ni uwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.

(2) Ugonjwa wa kuvimba uke (Vulvovaginitis)

Ni ugonjwa unaoathiri kwa kuvimbisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, mkojo kuuma na kukereketa wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu ukeni.

(3) Kuvimba Uke baada ya hedhi kukoma (Postmenopausal Atrophic Vaginitis)

Ni ugonjwa wa kuvimba kwa uke baada ya hedhi kukoma. Hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.
(4) Maambukizi ya Trikomonasi (Trichomonas Infection)
Ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aitwaye Trichomonas vaginalis. Dalili kuu ni muwasho katika uke au uume na kutokwa na uchafu ukeni.
(5) Ugonjwa wa Minyoo (Pinworm Infection)
Ni maambukizi ya minyoo wadogo sana wenye umbo la pini wanaoweza kuambukiza utumbo na kusambaa maeneo mbalimbali. Ugonjwa huu huwatokea sana watoto wa kati ya miaka 5 na 10.
(6) Inflamesheni ya Urethra (Urethritis)
Ni maambukizi kwenye urethra (ujia wa kutolea mkojo nje) yanasababisha kuvimba kwa urethra. Dalili kuu ni mkojo kuchoma, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kutokwa uchafu.


(7) Genital Warts

Ni vivimbe vidogo vinavyotokea juu ya ngozi sehemu za siri. Ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiana na unasababishwa na virusi viitavyo Human papillomavirus (HPV). Vivimbe vinaweza sababisha muwashona maumivu.

(8) Saratani ya sehemu ya nje ya Uke (Vulvar Cancer)

Ni saratani ya sehemu ya nje ya uke inayoambatana na kuwashwa sehemu ya nje ya uke.

(9) Ugonjwa wa Wasiwasi (Generalized Anxiety Disorder)

Ni ugonjwa ambao unaotokana na hofu ya matukio fulani. Wakati mwingine husababisha kujikuna sehemu mbalimbali hata sehemu za siri.

(10) Ugonjwa wa Sjogren (Sjogren's Syndrome)

Ni ugonjwa katika mfumo wa kinga ya mwili unaoathiri tezi zinazosaidia mwili kutengeneza unyevu nyevu kwenye macho na mdomo. Ugonjwa huu huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume.

(11) Kisukari

Ni ugonjwa sugu wa kimetaboliki unaosababishwa na kasoro katika utengenezaji wa Insulin au utendaji kazi wake. Kisukari kilichokomaa kinaweza sababisha maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kizunguzungu na kuwashwa sehemu za siri.


Zifahamu tiba ya muwasho Sehemu za siri



Nini husababisha Muwasho Sehemu za Siri za Mwanamke?




Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.