Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA)

ni shirika lisilo la kiserikali lenye lengo la kutoa elimu ya ufahamu wa mambo mbali mbali ya afya katika jamii kwa sasa likiwa limejikita kuongeza ufahamu kuhusu tatizo la USUGU WA DAWA(Antimicrobial resistance)

jamii medical awareness(jma) 

ni shirika lisilo la kiserikali lenye lengo la kutoa elimu ya ufahamu wa mambo mbali mbali ya afya katika jamii kwa sasa likiwa limejikita kuongeza ufahamu kuhusu tatizo la USUGU WA DAWA(Antimicrobial resistance)
*JMA* ilianzishwa mwaka *2017* chini ya udhamini wa *UKAID/HDIF* baada ya kuwa kati ya mawazo 10 bora ya miradi ya kutatua changamoto katika sekta ya afya nchini.Shindano hili liliitwa *MAWAZO CHALLENGE* na liliendeshwa na *SAHARA SPARKS* Tanzania ambapo lilikusanya mawazo *358* kutoka kwa wanafunzi wanaosoma kozi za afya Tanzania.Baada ya mchujo na mafunzo ya kuboresha miradi hiyo,mawazo *bora 10* tu ndio yalipata nafasi ya kufaidika na udhamini huo,JMA team ikiwa moja wapo;ambapo ilisimama na lengo la kutumia sanaa ili kusaidia jamii kubadili tabia katika matumizi sahihi ya dawa na kupambana na tatizo la usugu wa dawa.
Wazo hili la JMA liliasisiwa, kubuniwa na kuwasilishwa na *Fridon Teingisa Mazima*(Bachelor of Pharmacy,MUHAS) na walioliwakilisha katika hatua za mchujo na mafunzo mpaka hatua za mwisho walikua ni *Harieth Peter Ndumwa*(Medicine student,MUHAS) na *Josephat Seleman Hema*(Bachelor of Pharmacy,MUHAS)
Pia walifanya kazi na *Leonia Leornard Mao*(Business Administration,NIT) na *Kelvin Lyimo*(Sociology,UDSM_Presentor,Skonga,EATV) katika kipindi cha mpito kulikuza wazo hili.

Kwa sasa JMA ina members wapatao 40 katika mikoa 5 Tanzania.
JMA Ina usajili,katiba,akaunti ya benki,tovuti(website),kurasa katika mitandao ya kijamii na ofisi ya muda(Iko MUHAS,Dsm)

JMA inafanya kampeni inayolenga jamii kubadili tabia katika matumizi ya dawa na kuepuka matumizi holela ambayo ndio sababu kuu iletayo tatizo hilo.

JMA inatumia sana kama nyimbo,maigizo na katuni katika kufikisha ujumbe kwa jamii na sasa ina kampeni ya mabango/posters kupitia mitandao ya kijamii.

USUGU WA DAWA NI NINI?

Usugu wa Dawa ni hali ya Dawa kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi kama hapo awali
Hapa tunalenga dawa zinazotibu maambukizi yatokanayo na vijidudu vya magonjwa kama bacteria,virus ma fungi
Ni hali ya dawa kushindwa kufanya kazi ipasavyo kutokana na vijidudu vya magonjwa kutengeneza njia za kujilinda na nguvu ya dawa



Matumizi holela ya dawa ndio sababu kuu inayopelekea tatizo hili
Ni kampeni yenye lengo la kuongeza uelewa wa jamii kuhusu Usugu wa Dawa na kuishwawishi jamii kubadili tabia zinazoleta tatizo hilo.
Tatizo hili limetokana na matumizi holela ya dawa kitu ambacho jamii haijakitilia maanani  kwa muda mrefu na kupelekea tatizo la Usugu wa  Dawa.
Kampeni hii endelevu ili kuihimiza jamii ibadili tabia kwenye matumizi sahihi ya Dawa.
For more details please Our website.
www.jma.or.tz
Thank you

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.