*KWENU WADADA*
🍇Jee unajua ni kitu gani kinachompa amani na furaha mume wako?
🍇Inakubidi umsome vizuri mume wako ,ila kwa kila mwanaume anaejitambua kipaumbele chake cha kwanza ni UCHUMI\PESA.
🍇Anaweza kurudi nyumbani akiwa na msongo Wa mawazo sababu uchumi wake hauko sawa,madeni ,matatizo kazini,wazazi wake wanamtegemea yeye.
🍇Anapokua katika hali hio wewe ndio Wa kumliwaza ,wewe ndio tulizo lake ,wewe ndio Wa kumuusia kusubiri mitihani ya Allah.
🍇Nyumba yake ni pahala pekee pa mapumziko yake ,nyumba yake ndio utulivu Wa mwili wake na nafsi yake.
🍇Usimzidishie msongo Wa mawazo mpokee kwa tabasam,mpe pole huku ukiwa tayari umeshaandaa mazingira ya salama upendo amani na utulivu.
🍇Haipendezi kuanza kulalamika ,kuanza mizozano,kuanza kesi za mawalama,kuanza gubu ,kumpokea kwa dharau ,kutomjali na kumsimanga.
🍇Muoneshe unavojali na unavoguswa na matatizo yake,mpe moyo ,sio wewe umzidishie matatizo.
🍇Unaweza kulalamika kua mume wangu jeuri ,mkorofi kumbe umeshindwa kumfariji katika wakati mgumu.
🍇Muulize linalomsumbua kwa utaratibu kama hayuko tayari kukuelezea mda huo usilazimishe ,utapomfanya kua yeye ni best friend wako namba moja atakushirikisha kwenye mambo yake yote.
🍇Nguzo za furaha ya Ndoa yako anza kuzisimamisha wewe na hakikisha kua zinadumu.
*🍇Ni ushauri ukiyapenda yachukue ...🍇*
🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇🍇