🍪 .VILEJA VYA NJUGU NA CHERRY KWA JUU
🍪. MAHITAJI YA KUPIKA VILEJA VYA NJUGU NA CHERRY KWA JUU
1. SUKARI YAKUSAGA MAGI 1
2. SIAGI IWE NYEPESI MAGI 1
3. UNGA WAGANO MAGI 2
4. NJUGU ZAKU KANGA KISHA ZITWANGE ZIWE VIPANGE
5. CHERRY AMA JAM AMA ZABIBU
6. YAYI 1 LIPIGE
7. VANILA KIJIKO 1 CHAI
Washa jiko kwanza 180'c
🍪 JINSI YAKUTAYARISHA VILEJA VYA NJUGU NA CHERRY KWA JUU
1. KWENYE BAKULI TIA SIAGI NA KOROGA KWA MWIKO SASA TIA SUKARI ENDELEA KUKOROGA MPAKA IWE LAINI
TIA LILE YAYI KIDOGO KIDOGO LOTE KISHA TIA UNGA NA ENDELEA KUKOROGA MPAKA UNGA MLAINI.
2. FANYA VIDONGE VIDOGO VYA DUARA VYOTE KISHA VI ZUNGURUSHE KWENYE ZILE NJUGU.
3. VIPANGE JUU YA TRAY NA WEKA CHERRY JUU AMA UNACHO PENDA
4. PIKA KWA DAKIKA 20 TO 25 MINUTES