CHIPSI VURUGA / CHIPS MASALA
(masala chips / masala fries)
Mahitaji ya kupika chipsi vuruga:
- 1) Viazi Kata chips style
- 2) Pilipili hoho na karoti
- 3) Chumvi
- 4) Tomato paste
- 5) Nyama Kata ndogondogo
- 6) Vitunguu Maji na vitunguu thomu
- 7)Nyanya
- 8)mafuta ya kupikia
- 9)Pilipili ya kuwasha (ukipenda)
Namna ya kuandaa chips vuruga:
- -Kaanga Chips Weka Pembeni
- -Kausha nyama vizuri kwa viungo iive na iwe kavu
- -Kaanga Vitunguu maji kisha Weka Thomu
- - Halafu Weka Nyanya na karoti zikaangike
- - Kisha Weka pilipili na pilipili hoho pamoja weka Tomato paste, chumvi na curry powder, acha ichemke mpaka upate rojo zito.
- - Kisha Weka Nyama Changanya Vizuri Kisha Weka chips zako ulizokaanga halafu geuza polepole bila kuvuruga chips moto mdogomdogo.
NB:-unaweza ukatumia nyama yoyote upendayo au sausage pia unaweza ukapika bila nyama au ukiamua unakula na nyama pembeni.
-unaweza kuongeza viungo na mbogamboga zingine ukipenda.
-kwenye comments kuna picha zinazoonesha hatua zake.
picha:web