Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MAPISHI YA BIRIANI - CHAKULA CHA WEEK END .

Estimated read time: 1 min

BIRIANI

MAHITAJI YA MAPISHI YA BIRIANI

  • Mchele (rice 1/2 kilo)
  • Nyama (beef 1/2 kilo)
  • Vitunguu (onion 2)
  • Kitunguu swaum (garlic 1 kijiko cha chai)
  • Tangawizi (ginger 1 kijiko cha chai)
  • Maziwa mgando (yogurt 1 kikombe cha chai)
  • Hiliki nzima (cardamon 6)
  • Amdalasini nzima (cinamon stick 2)
  • Karafuu nzima (cloves 6)
  • Pilipili mtama nzima (black pepper 8)
  • Curry powder 1/2 kijiko cha chai
  • Binzari manjano (turmaric 1/2 kijiko cha chai)
  • Binzari nyembamba nzima (cumin 1/4 kijiko cha chai)
  • Chumvi (salt)
  • Mafuta (vegetable oil)

JINSI YA KUPIKA BIRIANI

  1. Kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama na uikaange kwa muda wa dakika 10. baada ya hapo tia tangawizi, kitunguu swaum, hiliki(4), amdalasini (1), karafuu (4), pilipili mtama (5), Curry powder, binzari manjano, binzari nyembamba na chumvi. Kisha koroga. Baada ya hapo tia yogurt na uipike mpaka ikauke kisha tia maji kidogo, funika na upunguze moto na uache ichemke kwa muda wa nusu saa.Baada ya hapo nyama itakuwa imeiva na mchuzi kubakia kidogo.Kwahiyo itatakiwa kuiipua.
  2. Loweka mchele kwa dakika 10. kisha chemsha maji mengi kidogo katika sufuria kubwa. baada ya hapo tia hiliki (2) amdalamsini (1) karafuu(2) pilipili mtama (3) chumvi na mafuta kiasi. acha ichemke kidogo kisha tia mchele.Hakikisha maji yameufunika mchele kabisa na uuache uchemke kwa muda wa dakika 8 tu (kwani hautakiwi kuiva kabisa) kisha uipue na uchuje maji yote katika chujio. baada ya hapo chukua sufuria ya kuokea (baking pot kama unayoiona kweye picha) Kisha weka wali nusu na uusambaze sawia kisha weka mchuzi nyama na mchuzi wake pia utandaze na umalizie kwa kuweka leya ya wali uliobakia. Baada ya hapo ufunike na uweke kwenye oven kwenye moto wa 200°C kwa muda wa nusu saa.na baada ya hapo biriani litakuwa tayari kwa kuliwa.
Asante 😋.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.