MAHITAJI YA KUPIKA MAYAI NA NYAMA
- mayai 8
- Nyama ya kusaga nusu kilo
- Tangawizi ilosagwa kijiko 1
- Cumin powder kijiko 1
- bizari nzima (cumin) ulosagwa kijiko 1
- Pilipili manga ilosagwa kijiko 1
- Pilipili ya unga (kama unapenda)
- Mafuta ya kupikia na chumvi
JINSI YA KUPIKA MAYAI NA NYAMA
- Chemsha nyama na viungo vyote bila maji kama nyama ni laini (lamb) kama si laini tia maji kidogo. Iwache mpaka ikauke iwe kavu kabisa. Wacha ipowe.
- Kata mayai kwa urefu hakikisha kila yai unalikata katikati. Toa viini vya yai vichanganye na ile nyama ilopowa.
- Changanya nyama na viini na yai moja kati ya yale mawili yalobaki. Changanya mpaka mchanganyiko uwe mlaini ambao unaweza kutengeneza duara bila kupasuka. Kama unapasuka ongeza yai moja lakini sio lile lilobakia kati ya yale mawili.
- Chukuwa vile vipande vya yai na mchanganyiko wa nyama tengeneza kama kwenye picha hapo juu.
- Weka mafuta jikoni. Piga lile yai lilobaki, choma kama unavuochoka katles. ENJOY 😃by livna