Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA 05, 06, 07, 08, 09

SAFARI YA KUZIMU EPISODE YA TANO

MTUNZI-OPPAH
0678635182
     tulipoishia namba nne
   na kama mtu anabisha dawa hii apa amuone mtoto yule pale alinyoosha kidole pale nilipo
         tuendelee

    huyu mpumbavu anataka kuharibu kila kitu ngoja nimfundishe malaya huyu aliongea mama huku akikunja sura  ghafla niliona kama mionzi ikitoka kwa mama na kuelekea kwa yule mzee ndipo hapo mzee alianza kulalamika jamani sionii sionii nisaidieni alilia sana
       watu wengi waliondoka kwenye msiba baada ya kuona kuna mambo ya kishirikina walibaki watu kadhaa tu ambao walimsapot mama na hawakujua tabia yake kiundani muda ulipita na wakati wa kuaga maiti ulifika
    watu waliaga na ilifika zamu ya mke wangu kwenda kuaga mwili laaah haulaaa alishangaa baada ya kukuta gogo likiwa ndo limeveshwa suti alianguka na kupoteza fahamu. waliangaika kumpepea mpaka akazinduka na kumuuliza kuwa umeona nini. alificha mke wangu na kusema aah nilishindwa kujizuia kutokana nampenda mume wangu. ila moyoni mwake alisema hapa kuna mchezo unaendelea wa kishirikina lazima nitafute ukweli!!
    muda ulikwenda na walipeleka lile gogo kwenye makaburi na kuanza taratibu za mazishi walizika na wakamaliza!!!!!
       ilipofika usiku sasa mama alituchukuwa na kwenda kwenye kwenye vikao vyao vya kichawi  jamani kazi ishaisha na si mnajua kesho mkuu wetu anakuja kwa hiyo inabidi tuiteuwe misukule ambayo lazima iliwe nyama siku hiyo. tulipelekwa mbele na kuangalia walionona walichagua na mimi nikiwepo ndani ya orodha watakaoliwa nyama siku inayofuata
     Asubuh ilifika na mke pamoja na watoto wangu waliaga na kuanza safari ya kurudi dar walipofika stendi mke wangu alimpigia simu rafki yake na kumwambia mm sitorud leo ila nenda kawapokee wanangu ubungo sawa! sawa shoga. aliwapandisha watoto gari kesha yeye kurud kutafuta kambi

    HAIWEZEKANI LAZIMA NIMPATE MUME WANGU AKIWA MZIMA!!!??????


SAFARI YA KUZIMU EPISODE YA SITA


       Tulipoishia epsode ya tano
   mke wangu aliwapandisha watoto gari kisha yeye akabaki sumbawanga ili atafute ukweli kuhusu kifo changu
       sasa endelea

wakati yeye akiwa anarud baada ya kuwapandisha watoto gari kumbe mama alikuwa akimwona live kabisa bila ya chenga. hahahahaaa alicheka mama huku akisema aah huyu mke wako nae anajifanya anataka kujua ukweli ngoja nitampoteza.
           mama usifanye hivyo mbona unanitesa sana mwanao kwan kuna kibaya kipi nilichokutendea???? funga mdomo wako mbwa wewe alininyamazisha mama kwa kufoka huku akisema huyu mwanamke anajifanya mjanja ngoja tutaonyeshana mm na yeye kisha akazima tv yake ya kichawi ambayo kilikuwa chungu kikubwa
            Haiwezekani mume wangu apotee kiholela kama hivi lazima nijue kila kitu aliongea huku akirud kijijini huku akiwa ajui kama mama alikuwa ameshamuona kwenye tv yake yake ya kichawi. muda ulienda na muda wa jioni aliomba sehemu ya kulala walau hata kwa siku moja lakin mwenye nyumba ile ambae alikuwa bibi kizee alimwambia sawa na lakin mbona nikikuangalia kama unamatatizo makubwa alihoji bibi yule nilimwambia ndio bibi ila kesho nntakusimulia yote
         kama kawaida usiku ulifika na siku hiyo ilibidi tuliwe nyama mm pamoja na misukule wenzangu lkn cha kushukuru siku hiyo huyo mkuu wao hakufika kabisa hapo mama aliamua kuchukuwa mkono wa mtoto mdogo na kuuweka skioni baada ya sekunde kadhaa alianza kuongea. eeeh mkuu leo hutowasili nn. aya sawa kiongozi. kisha aliutoa ule mkono skioni mwake
          jamani mkuu wetu hatowasili leo mpaka kesho kutokana na matatizo huku anga ya kwao sasa mithili hatujala nyama kipindi kirefu sana leo tuchinje misukule kadhaa ili tutoe hamu na kesho mkuu atakapofika tutaichinja yote itakayobaki aliongea mama kauli hiyo ilinistua mimi lakini wale wenzangu hawakuogopa wala nini walianza kuchaguwa misukule lakin mimi nilikuwepo lakin mama aliwaambia huyo ni kwa ajili ya mkuu wetu kesho.
      looooh kwa mara ya kwanza nilishuhudia watu wakichinjwa kama ngo'mbe walilia kwa uchungu sana msukule mmoja alichinjwa mpaka akanya mavi mazito wachawi walichekaa yaan waliona jambo la kawaida tu. walikula nyama huku wakionyesha hali ya kusifia kuwa nyama tamu
          baada ya kumaliza kula nyama mama alisimama na kutoa tangazo jamani kuna mtu mmoja anajileta kufuatilia mambo yasiyo muhusu ni mke wa mussa alininyooshea kidole. mchawi mmoja alidakia na kumwambia  mkuu unaonaje anaefuatilia nae awe nyama ya mkuu wetu kesho. wachawi walicheka kuonyesha kukubaliana kisha wakaanza kupiga ngoma huku wakicheza uchi kabisa kisha kikao kikafungwa
         ilipofika asubuhi mke wangu alimueleza kila kitu yule bibi na bibi akamwambia mjukuu wangu hii vita ni ngumu sema nitakusaidia kwa udi na uvumba mpaka utakapompata mumeo.  mke wangu alifurah lakin hakujua nini kinafuata kwenye hiyo vitaaa....... je nini kitaendelea???

SAFARI YA KIZIMU EPISODE YA 7

     
 tulipoishia ya sita
     nntakusaidia mwanangu ila hii vita siyo ya kitoto kama unavyofikiri.  aliongea yule bibi maneno yaliyomshangaza kidogo mke wangu
    TUNAENDELEA YA SABA
nikiwa ndani mule na wale misukule wenzangu ndipo mama alikuja na kisado cha unga kama kawaida walishangilia ila mm kutokana na kukaa mda mrefu nilikuwa nishaanza kula ule unga na mimi nikawa mmoja wapo. mama alieka ndoo chini tulianza kugombania ule unga. nilifanikisha kupata lepe la unga mkononi mwangu nakuanza kubugia kama kichaa.
           mama alicheka kisha akachukuwa ndoo yake na kuondoka. nilikaa pembeni nikiwaacha wale jamaa wakiwa wanacheza kama mizuzu. nilianza kujiuliza maisha haya humu mm mpaka na hapa wakishanikata tu ulimi sitorud tena  kuwa binadamu na kwa nini nife kizembe kama hivi??lazima nipambane kama wa kiume mpaka tone langu la mwisho lakin sio kufa kama hivi.. nilitafakari na nilipata wazo????
        kwa upande wa mke wangu yule bibi alimwambia mke wangu apeleke michanga ya makaburi kumi kila kaburi na michanga yake  mamq hivi nitaweza kwel alihoj mke wangu ndio kama kweli unamtaka mumeo lazima ufanye hivyo la sivyo leo wanamla nyama inabidi tufanye haraka ili tuweze kumnusuru mume wako aliongea kikongwe huyo.
         mke wangu alikusanya hiyo michanga na kupeleka kwa yule bibi kisha bibi akaiweka kwenye chombo maalum kilichofuata alichinja jogoo kubwa na kumuamuru mke wangu anyonye damu ya jogoo yule mke wangu alitii alifyonza yote mpaka ikaisha bibi akampa dawa nyngne akameza kisha akamwambia sasa tusubir usiku kwa ajili ya vita tu!!!!!
     ilipofika usiku wachawi walikusanyika wengi ile mbaya na kama kawaida mama alituchukuwa nilishangaa baada ya kuona wachawi wapo wengi apo nilikumbuka leo ni siku kuu ya kafara na leo lazima nife mussa mimi. mama unaniuaaa nililalamika lakin waliendelea na shughuli zao kama kawaida na ikafika muda wa sadaka
     tulikuwa misukule wengi sana wa kuchinjwa kutokana wachaw walikuwa weng kwa hiyo walikusanya misukule kutoka pande tofauti tofauti
looh nilishangaa kumuona baba yangu ambae tulimzikaga kitambo sana daaah kumbe mama ni mshenzi kias hiki mpaka baba yaan mume wake mzee shomvi nae alimuweka msukule. ambae ni baba anguuuu!?? niliita babaaa lakin hakuskia wala kuonyesha ishara yeyote ya kuitwa na mtu
      wakat wa sadaka uliwadia na baadhi ya misukule ilikuwa ikiendelea kuchinjwa ilifika zamu yangu ya kuchinjwa niliwekwa kwenye jabari kubwa na mchawi alieshika panga aliinua juuu na lakini ghafla????? je nini kitaendelea

SAFARI YA KUZIMU  EPISODE YA MWISHOO

 
        Tulipoishia
 niliwekwa juu ya jabari kubwa na yule mchawi alinyanyua panga lake lakin ghafla
      tuendelee
  lakin ghafla niliona akirushwa mbali kama mtu aliepigwa na kitu kizito nilishangaa na kuanza kujiuliza nn kinaendelea wachawi wengine walistuka na kuanza kujipanga kwa ajili ya vita
     loooh nilipogeuza macho nilimkuta mke wangu akiwa na yule bibi kizee wakiwa wanapambana na kundi hilo kubwa la wachawi na safari hii mke wangu aliniona vizuri kutokana na dawa aliyotumia ya yule bibi.  walipambana kwa mda mrefu na walifanikisha kuua wachawi wengi
     wale wengine kutoka taifa jingine baada ya kuona kimenuka walipotea kimiujiza. nilishuhudia mchezo live bila ya chenga. mama yangu alibaki na kuendelea kupambana na yule bibi lakin baada ya kuona kazidiwa nae alipotea kiuchawi
      yule bibi baada ya kuona vita vimeisha alituchukuwa wote kimiujiza na kwenda mpaka kwake. akatupa dawa na wote tukawa  tunaonekana na hata wale wenzangu waliokuwa mazezeta walirud katika hali yao ya kawaida walijishangaa nini kimetokea mpka wapo vile. mke wangu alifurah kwa kuona nimerud katika hali ya kawaida alilia machozi ya furaha
        ilipofika asubuh yule bibi aliita watu wote kijijini na kuanza kuelezea mwanzo mwisho mpaka tulivyotekwa. na baadae alituamuru tutoke. looooh watu walishangaa baada ya kuonana na ndugu zao ambao waliwazika kitambo na hicho.
jamani huyu mama ni mwanaharam twendeni tukamchome moto mbwa yule aliongea mmoja kati ya wana kijiji mwenye hasira kali ambae alisapotiwa na kila mtu.
       tulikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa mama lakini cha ajabu tulimkuta amekufa yaan ni wa kitambo sana. nilihuzunika kutokana hakutubu zambi zake.
      watu walishangilia na kuondoka lakin tulibaki mimi,mke wangu pamoja na yule bibi. kwa kuwa alikuwa mama yangu isingekuwa vizur kumwacha vile niliandaa mazingira ya kumzika. na tulifanikisha kuzika japo tulikuwa watatu tu.
      tulimshukuru yule bibi na tulimuaga bibi hakuwa na hiyana alitupa baraka zote na kisha tukaanza safari ya kuondoka. tulifika dar mida ya saa 3 usiku na kukodi gari mpaka nyumbani  niliwakuta wanangu wamelala na mimi nililala
       niliamka baada ya kuskia kama kuna kelele mlangoni nilitoka nje. loooh nilikuta watu kibao pamoja na waandishi wa habari wakitaka ukweli wa kila kitu. niliwaeleza kila kitu mwanzo mpaka mwisho wa safari.  maisha yangu yalirud upya na furaha ilirud tena ndani ya nyumba

     NASHKURU SANA KWA KUWA NA MIMI MWANZO MPAKA MWISHO WA STORI NA MIMI SINA CHA KUWALIPA. ZAIDI NIMEIPENDA SAPOTI YENU MPAKA TUNAKAMILISHA SIMULIZI YETU HII AHSANTENIIIIIII
        TUKUTANE KATIKA VIGONGO VINGINE INSHAALLAH

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.