Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MPIGA PICHA SEHEMU YA 04, 05, 06 NA 07

MPIGA PICHA SEHEMU YA NNE


"Lakini na wewe kaka upunguze hiyo misimamo yako ya ajabu bwana."
"Ok sawa nitapunguza kwanza twende nyumbani mengine tutaongea nyumbani maana wewe nae kwa kupeleleza nakuaminia."
Tulienda mpaka kituo cha daladala na kupanda daladala iliyotupeleka mpaka maeneo ya nyumbani kwetu. Tulifika nyumbani na kula chakula cha usiku kisha kila mmoja akaingia kwenda kulala.
*****************************************
Saa moja na nusu usiku niliingia katika ukumbi ambao ulikuwa unepambwa vyema. Nilikuwa nimebeba kimkoba kidogo ambacho ndani yake nilikuwa nimehifazia kamera yangu ambayo nilikuwa napenda sana kuitumia. Ilikuwa kamera yenyekutoa picha bomba hata kama iwe usiku wa namna gani. Ni kamera ambayo nilimwagiza rafiki yangu mmoja aliekuwa anasoma Uingereza. Nilifika mapema kabla ya shughuri.
Ilipotimu saa tatu juu ya alama.... taa za ukumbi zilizimwa kisha giza likatawala kwa mda wa kama dakika mbili. Ndipo taaa zikawaka. "WAAA"
"Happy birthday to you..... happy birthday to you.......happy birthday dear Zulfa ........ happy birthday to you..... aona yuna aona yuna.............." zilisikika sauti zikiimba kisha kushangilia kwa furaha. Mbele alikuwa kasimama Zulfa huku akiwa kafungwa kitambaa machoni. Alikuwa amependeza kweli. Nguo alizokuwa amevaa zilimfanya apendeze zaidi hata na siku ya kwanza nilipomuona alipokuja studio kupiga picha. Mwanamke wa kiarabu aliyekuwa akifanana sana na Zulfa alienda na kumfungua kitambaa. Mimi nilikuwa pembeni nikiendelea kupiga picha za matukio ambayo yalikuwa yakiendelea. Watu walikuwa wengi mno na wote walikuwa wamependeza kweli. Shughuli iliendelea mpaka majira ya saa saba usiku ndipo shughuli ilipofikia tamati. Niliweka vitu vyangu sawa ili niweze kuondoka. Lakini kabla sijaondoka nilisikia sauti ya Zulfa akiita jina langu.
"Lucas...." Bila kuitika niligeuka na kukutana na Zulfa ambae alikuwa anakuja nilipokuwa.
"Mambo vipi Lucas?"
"Poa mrembo Zulfa. Niambie?"
"Safi nashukuru umekuja kunipiga picha maana toka unipige picha zile nimetokea kupenda utendaji wako wa kazi. Unapiga picha nzuri sana Lucas." Aliongea Zulfa huku akiwa ananiangalia kwa kuibia.
"Zulfa leo umependeza sana. Wewe ni mrembo kweli." Niliogea maneno ambayo sikuwa nategemea kuyaongea.
"Asante Lucas.... hata wewe pia mbona umependeza sana tu." Aliongea Zulfa. Watu wote walikuwa wameshaondoka ukumbini. Na tulikuwa tumebaki mimi na Zulfa tu. Akili yangu ilinituma na kuona huu ndio mda muafaka wa kumwambia Zulfa yangu ya moyoni. Wakati wa kushusha mzigo ambao nimeubeba moyoni mwangu kwa mda.
"Nafurahi tumekutana na wewe kwa mara nyingine Zulfa. Na mda huu nilikuwa nausubili sana maana kuna kitu toka mara ya kwanza nimekuona kimejengeka moyoni mwangu. Zulfa naposema wewe ni mzuri namanisha kweli nayo yasema japo wengi najua wamesha kutamkia neno kama hili. Mara ya kwanza nilipokuona tu moyo, mawazo na akili yangu yote ilisimama kwa mda. Hakika uzuri wako ulinipa mpasuko wa moyo. Nilivutiwa na wewe na nikatokea kukupenda siku hiyo hiyo. Hivyo basi naomba............" kelele za kugongwa kwa mlango wa chumba changu zilinishitua na kunikatisha kuendelea kuota ndoto ile. Mambo yote yaliyokuwa yanatokea kumbe ilikuwa ni ndoto tu. Nilinyanyuka pale kitandani na kwenda kufungua mlango. Nilimkuta mama kasimama mlangoni.
"Vipi baba unaumwa?" Aliniuliza mama.
"Hapana mama niko sawa. Ila sema uchovu tu wa jana unachangia. Shikamo..." Niliongea huku mkono wangu ukipikicha macho yangu.
"Marahaba mwanangu....Inaelekea saa mbili.... zimebaki dakika chache ifike saa mbili kamili. Nimeona huamki tu ndio nikaamua nije nikugongee mlango mwanangu. Maana sio kawaida yako kuchelewa kuamka kiasi hiki." Aliongea mama
"Haaaaa ....aaaaaahhhhh...... Ok sawa asante mama acha nikajiandae niwahi kazini." Niliongea huku nikipiga miayo. Nilirudi chumbani kwangu na kuchukua taulo na mswaki kisha nikatoka kuelekea bafuni.
Saa tatu asubuhi nilikuwa kazini. Mambo yalikuwa yanaenda kama kawaida. Tulikuwa tunapiga story mimi pamoja na wafanyakazi wangu, maana hatukuwa na kazi ya kutuweka bize.
"Tino vipi tuliongea kitu jana na nikakupa kazi ya kufanya vipi umefikia wapi?" Nilimuuliza swali Tino
"Kazi...! Kazi ipitena?......." aliuniuliza swali Tino na kabla sijamjibu kitu alikumbuka na kujibu mwenyewe.
"Aaaaa ile kazi. Nimesha kumbuka. Unajua nini kaka ile jana nimetoka tu hapa nilikwenda mpaka maeneo ya nyumbani kwao." Aliongea Tino.
"Eeheee ndio ikawaje sasa?" Nilihoji.
"Subili nikupe mchongo boss.... mbona unapapala kama sio mtoto wa town vile."
"Haya nisha subili... nakusikiliza ongea."
"Unatakiwa uwe mpole maana mchezo huu hauitaji hasira. Kwanza boss hebu niambie ukweli ni serious kabsa au unazingua tu maana......"
"Sasa Tino mimi nitazingua nini na unajua kabsa toka tujuane mimi na wewe sijawahi kukwambia inshu kama hii. Niko serious kabsa, ila naona wewe kama unataka kuni-let down."
"Kama uko serious basi sawa.... mimi jana ile nilienda mpaka kwao, maana pale kwao uwa natinga mara kwa mara, kaka yake na Zulfa mimi huwa ni jamaa yangu sana. Nilipofika kwao nikamulizia kama kaka yake Zulfa yupo pale nyumbani. Na nilie muuliza hakuwa mwingine alikuwa boya fulani hivi anafanya kazi pale." Tino alitulia kuongea kidogo
"Mmmm.......! .......eehhhheee......" niliongea ili kumfanya Tino aendelee kunipa mkanda mzima.
"Afu unajua nini boss tumekuwa kama tuna bahati mbaya.... " aliongea Tino maneno ambayo yalinishitua kidogo.
*******************

MPIGA PICHA SEHEMU YA TANO


"Kwa nini tena Tino...... bahati mbaya ipi hiyo?" Nilimtupia swali tino huku nikizidi kumtolea macho.
"Zulfa bado anasoma na mda wowote kati ya kesho au kesho kutwa anarudi shule."
"Anarudi shule? Si shule zimefungwa ama?"
"Ndio anarudi shule.... afu shule zilizofungwa ni za advance. Zulfa bado ndio kwanza yuko kidato cha tatu."
"Tino hebu acha utani bwana... Zulfa yuko kidato cha tatu? Haki ya Mungu utakuwa unanidanganya wewe."
"Aaaaa bosi lini tena tumeanza utani mpaka nikudanganye. Ni kweli Zulfa anasoma kidato cha tatu." Aliongea Tino maneno ambayo yalizidi kunipa wakati mgumu.
"Kwahiyo unataka kuniambia leo au kesho Zulfa anaondoka?" Nilimuuliza swali Tino
"Ndio hivyo ila sikufanya makosa nilifanikiwa kupata namba yake." Aliongea Tino huku akinikabizi zile namba. Kisha akaendelea kuongea.
"Hizi namba ukipiga akawa hapatikani basi ujue tiali kasha kwenda shule, maana huwa anaacha simu nyumbani. Huwa haendi na simu shuleni." Alimaliza kuongea Tino. Kisha mimi bila kupoteza mda niliamua kuzipigia zile namba za Zulfa. Baada ya kuzipigia zile namba kweli zilikuwa hazipatikani.
*********************************************
**
Baada ya kazi tulitoka nje tukawa tunapiga story mbili tatu. Baada ya story kunoga alikuja mdada mmoja.
Alikuwa amevaa nguo zilizo raruka. Japo nguo zake zilionekana kuchanika chanika lakini uzuri wake wa asili ulionekana.
"Kaka samahani naomba unisaidie japo pesa ya kula na siku mbili sijaweka kitu chochote tumboni." Aliongea yule msichana aliyekuwa amevaa nguo zilizokuwa zimechanika. Baada ya kumtizama kwa mda nilijikuta nikimuonea huruma na kumshika mkono kisha tukaongozana nae kuelekea kwenye mgahawa uliokuwa karibu na pale ofisini kwangu.
Nilifika nikamwagizia chakula. Alianza kukifakamia kile chakula kwa fujo. Kipindi hicho mimi nilikuwa namwangalia tu jinsi alivyokuwa anafanya.
Plet ya kwanza aliimaliza. Nikamuliza kama ameshiba. Akadai hapana. Nilimwita mhudumu na kumuomba amwongeze nyingine. Plet ya pili ililetwa. Aliendelea kula mpaka ilipofika nusu ndipo akadai kuwa ameshiba.
"Usiogope dada kama ujashiba endelea."
"Hapana kaka nimeshiba... asante sana." Aliongea huku akiwa ananiangalia kwa kuibia.
"Ok kama umeshiba hamna tatizo.... kwahiyo sasa hivi unaelekea wapi?"
"Safari yangu haijurikani mwisho.... lakini kwa sasa nitaendelea kutembea tembea tu." Alinijibu yule dada.
"Hapana sio vizuri kama huna mahali pakwenda haitakiwi kutembea tembea hovyo hapa mjini maana vibaka niwengi sana." Moyo wa kutoa msaada kwa msichana yule nisie mfahamu ulizidi kuongezeka. Niliwaza kumpa msaada zaidi ili kumuepusha na mateso aliyokuwa anayapitia.
"Twende ofisini kwangu." Nilimwambia kisha tukaongozana nae na kurudi mpaka ofisini kwangu.
"Majaliwa..... kaa na huyu binti ngoja niende hapa nikachukue kitu marazmoja nakuja. Nilimkabizi yule binti nisiemfahamu kwa mfanyakazi wangu Majliwa kisha mimi nikaondoka. Nilienda dukani nikanunua nguo ili nije nimpatie yule binti ili aweza kubadilisha. Baada ya kufika dukani nilinunua nguo kisha nikaanza kurudi. Nilipofika dukani sikuweza kumuona yule binti. Na nilipo muuliza Majariwa. Alianza kujibu kwa kujing'atang'ata hali hii ilionesha kuwa Majaliwa hakuwa anajua yule binti kaelekea wapi. Nilimwambia Majaliwa anisaidie tumtafute yule binti. Tulizunguka mitaa ya karibu lakini hatukuweza kumuona tena. Binti yule alikuwa tiali kasha toeka maeneo yale. Baada ya jitihada za kumtafuta kugonga mwamba tulirudi ofisini na kuendelea na ratiba zingine. Japo mawazo yangu yalikuwa kwa yule binti.
Siku zilipita bila kuweza kumuona tena yule binti. Lakini kila nilipokuwa nikiziona zile nguo nilizonunua kwa ajiri yake niliweza kumkumbuka. Akili yangu ilinituma na kuwaza kuna siri kubwa sana juu ya yule binti ambayo napaswa kuifahamu. Siku zilizidi kwenda hatimae matumaini ya kumpata binti yule yalipotea.
****************************************
Siku moja majila ya usiku nikiwa njiani kuelekea nyumbani mara nilisikia sauti ya mtu akipiga kelele za kuomba msaada. Uoga uliniingia nikawaza kukimbia na kushindwa kwenda kutoa msaada maana nilihisi ni mchezo ambao umekuwa ukitumiwa na vijana wa mjini ili kuweza kuwaibia watu. Lakini kilio cha kuomba msaada kilinivuta na moyo wa huruma ulinitawala na wazo la kwenda kutoa msaada likanijia. Ujasili wa ajabu ulinifika nikaelekea eneo la tukio. Nilikuta vijana watatu wakimvua nguo kwa nguvu msicha ili waweze kumfanyia kitu kibaya. Nilianza kupambana na wale vijana niliwatupia makonde ya uhakika. Baada ya kumpiga mmoja kati ya wale vijana, wengine waliogopa na kuanza kukimbia. Nilimnyanya yule dada toka pale chini kwa kumshika mkono. Dada wa watu alikuwa ameficha uso wake kwa aibu. Nguo aliyokuwa amevaa ilikuwa imechanika nazani ni kutokana na purukushani kutoka kwa wale vijana waliokuwa wanataka kumbaka. Kuchanika kwa nguo yake kulifanya sehemu kubwa za mwili wake zibaki wazi. Aibu nami ilinishika nikaamua kuangalia pembeni kisha nikavua shati langu na kumpa avae huku mimi nikiwa nimebaki na t-shet ndogo iliyokatwa mikono saizi ya mabega. T-shet ambayo ilikuwa inaendana na mwili wangu
"Shika.... kamata hii vaa." Niliongea huku nikiwa nimeangalia pembeni. Yule dada alipokea lile shart langu kisha akalivaa. Hakika shart lile liliweza kumsitili kwa kiasi chake. Tulitembea na yule dada toka maeneo yale yaliyokuwa na giza mpaka tukafika eneo ambalo lilikuwa na mwanga. Taa za umeme za barabarani zilipokuwa zinawaka.
"Ilikuwaje hao watu wakawa wanataka kukubaka?"
"Walinikuta nimelala...." aliongea yule dada sauti ya yule dada ilifanana na ya yule binti ambae alikuja kwangu akiwa anataka msaada. Baada ya kusikia sauti ile nilimtazama yule dada kwa umakini na kugundua kweli alikuwa ndiye.
******************

MPIGA PICHA SEHEMU YA SITA


"Inakuwaje unalala vichochoroni? Huoni kuwa nihatari sana kwako?" Nilimuuliza maswali yule dada.
"Kaka mimi sio mwenyeji kwenye mji huu na sina pa kwenda maana sina ndugu wala rafiki wa kusema nitaenda kulala kwake." Aliongea yule dada.
"Unasema hauna ndugu......? Ndugu zako wako wapi? Na huku umekuja kujaje?" Nilimuliza maswali mfululizo yule dada.
"Ni historia ndefu kaka yangu...." aliongea yule dada.
"Kwanza samahani naomba kufahamu jina lako unaitwa nani? Maana leo sio mara ya kwanza tunakutana." Niliongea huku tukiwa tunazidi kutembea na yule dada barabarani. Kwa jinsi alivyokuwa amevaa ile shart ilikuwa ngumu kwa mtu yeyote tuliekutana nae kutambua kuwa yule dada alikuwa mtoto wa mtaani. Shart langu lilimfanya aonekane mtoto wa mjini kwa aina ile ya uvaaji. Tofauti ilikuwa iko chini kwenye miguu alikuwa kavaa kanda mbili.
"Naitwa Harriet...."
Alitaja jina lake
"Mbona una jina zuri kiasi hiki imekuwaje uko mtaani unazurura. Nini kilikupata?"
"Ni story ndefu kaka lakini kwakuwa wewe unaonekana ni mstaarabu acha tu leo nikwambie." Aliongea Harriet huku safari yetu ikiwa inaendelea. Nilingalia saa yangu ya mkononi ilikuwa imetimu saa sita na dakika arobaini na mbili za usiku. Kwa mda ule nyumbani kwetu walikuwa wamesha funga hivyo nilikuwa nawaza wapi pa kumpeleka Harriet.
"Kabla hujaniambia hiyo story yako naomba nikuulize kitu Harriet...."
"Uliza tu kaka wala usijali..... ila na mimi naomba kujua unaitwa nani kaka. Aliongea Harriet.
"Ok mimi naitwa Lucas.... Harriet unaniamini?"
Nilimuuliza swali Harriet ambae hakujibu badala yake alikaa kimya bila kuzungumza kitu chochote.
"Mmh kimya nacho ni jibu... hakika najua huniamini, lakini kwa leo naomba tu uniamini..." niliongea maneno ambayo hakika kwa Harriet yalikuwa kama fumbo. Nilimshika mkono Harriet kisha tukakata kulia na kuiacha barabara kuu na kushika barabara ndongo iliotupeleka mpaka mahali palipokuwa na nyumba za kulala wageni. Nilifika mapokezi nikiwa nimemshika Harriet mokono. Niliulizia chumba na kwa bahati zuri tulipata chumba. Nililipia kisha tulipngozana na mhudumu wa gest house ile mpaka kilipo chumba. Alifika akafungua mlango kisha mimi na Harriet tukaingia. Mhudumu alitukabizi funguo kisha akaondoka.
Harriet alikuwa bado anashangaa bila kusema kitu chochote.
"Nenda kaoge.." niliongea maneno ambayo yalimtoa Harriet katika dimbwi lile la mawazo mazito alilokuwa kazama.
Harriet alielekea bafuni kwenda kuoga nakuniacha mimi nikiwa pale chumbani. Baada ya dakika nane Harriet alitoka bafuni akiwa kasha maliza kuoga.
"Harriet mimi ni mtu mwema na usiwe na mashaka yeyote juu yangu. Naomba tu uniamini na ujue pia kuwa uko mikono salama dada yangu." Niliongea maneno ambayo na uhakika yalimtia moyo Harriet. Taratibu Harriet alianza kujiamini kama mwanzo.
"Harriet samahani kwanza kwa usumbufu. Lakini najua kwa mda huu na mahali hapa ndio panafaa kuniambia nini hasa kilikusibu historia ya maisha yako. Na imekuaje uko hapa unateseka mtaani?"
Harriet alikohoa kidogo kisha akanitazama usoni na kuanza kuongea.
"Kwa majina kama nilivyo jitambulisha mwanzo naitwa Harriet Hadson. Mimi ni mzaliwa wa Mbeya baba ni mhehe na mama ni mbena. Nilizaliwa mia miaka 19 iliyopita. Nilikuwa mtoto wa pekee katika familia yetu. Nikiwa na umri wa miaka kumi wazazi wangu walifariki kwa ajari mbaya ya gari." Alisita kuongea kisha akaanza kulia. Nilianza kumbembeleza na kumpa pole kwa yaliyotokea. Ulipita mda ndipo akanyamaza kisha akaendelea kunisimulia. "Kipindi wanafariki wazazi wangu nilikuwa bado mdogo sana nilikuwa nisoma darasa la tano katika shule moja ya private. Wazazi wangu walikuwa wananipenda sana walinipatia elimu bora. Walinilea kama yai....... Basi baada ya wazazi kufariki ndugu wa pande zote mbili waliafikiana mimi niende nikalelewe na baba yangu mkubwa ambae ni kaka yake na baba. Mali zote walizokuwa wameacha wazazi wangu zilibaki chini ya uangalizi wa baba mkubwa. Mwanzo maisha yalikuwa mazuri sikatai lakini kadli siku zilivyokuwa zinazidi kwenda mambo yalizidi kuharibika. Nikiwa darasa la saba nilihamishwa shule kutoka shule ya private ambayo nilikuwa nasomea awali na kurudishwa shule za government. Kisa baba alidai naharibu pesa kwa kusoma shule za gharama huku akidai kuwa sina akiri. Hivyo nasababisha upotevu wa pesa. Sikuvunjika moyo niliendelea kusoma kwa bidii hatimae nikamaliza darasa la saba na nikabahatika kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza. Miaka minne badae nilikuwa nisha maliza elimu ya sekondari. Sikubahatika kuvmchaguliwa kujiunga na elimu ya kidato cha sita. Nakumbuka nilipata division four ya point 27. Nikaomba wanipeleke chuo lakini walikataa. Sikuwa na kimbilio hivyo niliamua kukaa tu nyumbani.
Nikiwa na miaka kumi na nane nilipata mchumba ambae tulijuana tu kupitia mitandao ya kijamii. Nilitokea kumpenda sana Vedasto tena sana japo hatukuwa tumewahi kuonana lakini nilimuona kupitia picha zake facebook. Vedasto alionesha kunipenda niliamini alikuwa ananipenda. Hii yote niliona kupitia message zake alizokuwa ananitumia. Kila mara alikuwa akinipigia simu. Hakika alikuwa akinijali sana.
Baada ya uhusiano wetu kitimiza miezi sita Vedasto alinishawishi na kunitaka nije Mwanza. Maneno ya Vedasto niliyapokea hii yote ilisababishwa pia na mateso niliyokuwa nayapata nyumbani. Niliona ni bora nitoloke nyumbani nije Mwanza kwa Vedasto ili nije niolewe." Alizidi kuongea Harriet maneno ambayo yalizidi kuumiza moyo wangu.
"Enh....! Ulipofika Mwanza ikawaje?" Nilimuliza swali Harriet
"Nilitoroka nyumbani na kupanda basi.... pesa za nauli alinitumia. Siku iliyofata nilifika Mwanza Vedasto alinipokea lakini cha kushangaza hakunipeleka nyumbani kwao. Alinikomeshea nyumba ya kulala wageni. Vedasto aliniahidi anakuja kunitambulisha kwa wazazi wake. Aliniahidi anakuja kunioa. Lakini baad tu ya kuona mwili wangu na kunichezea alibadili mawazo na kunitelekeza gest. Vedasto alinitelekeza gest. Baada ya pesa alizokuwa amelipia gest kuisha nilifukuzwa. Sikuwa na pa kukimbilia nililazimika kuingia mtaani na kuwa mmoja ya omba omba wa mtaani." Alimaliza kuongea Harriet. Nilipotazama saa yangu ilikuwa imetimu saa kumi za usiku.
******************

MPIGA PICHA SEHEMU YA SABA


"Pole sana Harriet hizi ni changamoto tu katika maisha. Ndio mana wahenga walisema hujafa hujaumbika......"
"Asante...... nashukuru kaka Lucas. "
"Mmmm!!! Sawa usijali Harriet unajua toka mara ya kwanza nimekuona moyo wa huruma ulinijia nilitamani sana nikusaidie. Sizani kama unakumbuka kuna siku ulinikuta ofisini ukadai unanjaa? Nilikuchukua na kukupeleka kwenye kimgahawa ukahudumiwa chakula. Lakini baada ya kula tulipotezana."
"Nakumbuka ndio lakini sikujua kama ni wewe aise.... asante sana kwa moyo wako wa ukalimu." Aliongea Harriet.
"Toka siku hiyo nilikutafuta sana lakini sikuweza kukupata lakini leo nashukuru Mungu katukutanisha tena... nahitaji nikusaidie Harriet." Nilimwambia Harriet
Harriet alitikisa kichwa kukubali nilichomwambia. Mda mchache usingizi ulimkamata Harriet na kuanza kumuongoza jinsi ulivyokuwa unataka wenyewe. Harriet alilala usingizi. Mimi nilinyanyuka pale kitandani na kumlaza Harriet vizuri kisha na mimi nikalala huku nikiwa nimekaa. Nilikaa chini kwenye sakafu kisha nikaegamia kitanda. Usingizi ulinipitia pale chini.
Kelele za kugongwa kwa mlango zilituamsha toka usingizini Harriet alikuwa wa kwanza kushituka, kisha akaniamsha na mimi. Nilinyanyuka na kuuendea mlango kisha nikaufungua. Nilikutana na sura ya mhudumu ambae alikuwa ametuhudumia usiku.
"Vipi dada? Nilimuuliza swali mhudumu yule.
"Mda wa usafi kaka na pia mda wa umeisha, kwa pesa ambayo mlilipia jana, sijajua kama unaongeza mda mwingine."
"Ooooo.....! Kwani ni saa ngapi sasa?"
"Saa tano kasoro za asubuhi?"
"Saa tano?" Nilijibu kwa kuhamaki huku nikitupia jicho kwenye saa yangu katika mkono wangu wa kushoto.
"Ok sawa naomba niongeze mda nitalipia hamna shida dada yangu." Nilimwambia yule dada ambae alikubali kisha akaaga na kuondoka.
Nilirudi ndani nikamkuta Harriet akiwa kakaa pale kitandani.
"Umeamkaje?"
"Salama tu kaka sijui wewe?"
"Inshallah Mungu anasaidia nimeamka salama."
Baada ya salamu nilimuaga Harriet kisha nikatoka nje na kwenda kununua kifungua kinywa pamoja na mswaki na dawa ya meno nilinunua kisha nikarudi ndani. Nilifika nikamkabizi Harriet mswaki pamoja na dawa kisha Harriet alinyanyuka na kuelekea bafuni. Harriet akiwa bado yuko bafuni nilimuaga na kumwambia kuwa nitarudi mda mfupi pia akimaliza kunawa ale chakula asinisubili.
Nilitoka mle ndani na kwenda mpaka katika moja ya duka la nguo lililokuwa mtaa ule na kununua nguo kwa ajili ya Harriet. Baada ya kumaliza nilirudi mpaka kwenye ile gest na kwenda moja kwa moja katika chumba nilichokuwa nimemwacha Harriet. Nilifika na kumkuta Harriet akiendelea kunywa chai. Nilifika na kumpatia zile nguo. Baada ya kumaliza kunywa chai nilitoka mle ndani na kumpisha Harriet ili aweze kubadili nguo. Na baada ya dakika tano Harriet aliniita niingie ndani. Niliingia ndani na kumkuta Harriet akiwa kapendeza sana. Nguo zile zilimkaa vyema sana Harriet. Ule urembo wa Harriet uliojificha kisa maisha ya shida ulionekana.
"Asante sana Lucas kwa wema wako japo sina cha kukulipa, lakini naamini Mungu atakulipa." Aliongea Harriet
"Usijali Harriet......." nilimjibu Harriet kisha nikamwomba tutoke mle kwenye kile chumba cha guest. Tulikabizi kile chumba kisha nikalipia gharama. Tulipotoka nje ya ile guest nilichukua simu yangu kumpigia simu Sarafina nikimwomba tukutane nyumbani kwake. Tulipofika barabara kuu tulipanda bajaji mimi na Harriet.
"Tupeleke kirumba." Nilimwambia dereva bajaji.
Baada ya dakika tano tulikuwa tushafika maeneo ya kirumba tulishuka kwenye bajaji na kuanza kutembea kuelekea nyumba ambayo alikuwa akiishi Sarafina. Sarafina alitupokea kisha tukaingia ndani.
"Sarafina huyu hapa ni mgeni wangu anaitwa Harriet ni mtu wangu wa karibu sana." Nilimtambulisha harriet kwa Sarafina baada ya salamu.
"Nashukuru kukufahamu Harriet karibu." Aliongea Sarafina huku wakipeana mikono na Harriet.
"Asante Sarafina nami a nashukuru kukufahamu." Alijibu Harriet.
"Naona mmesha fahamiana sasa naomba Sarafina tutoke nje mara moja namaongezi na wewe." Nilimwambia Sarafina kisha tukaongozana kmimi na Sarafina tukatoka nje na kumwacha Harriet mle ndani.
"Sarafina kama unavyo muona huyo dada hapo ni mtu wangu wa karibu kama nilivyokuwa nimekwambia mwanzo. Sasa nashindwa kumpeleka home si unajua tena wazazi wangu walivyo. Naomba kama unanafasi akute anakaa hapa kwako kwa siku hizi kazaa ambazo atakuwepo Mjini." Nilimwambia Sarafina.
Sarafina hakukataa alikubali ombi langu la Harriet kukuta anaishi kwake.
**********************************
Siku zilizidi kwenda Harriet akiendelea kuishi na Sarafina. Jukumu la kuwatimizia mahitaji lilikuwa juu yangu na mara kwa mara nilikuwa nawatembelea Harriet pamoja na Sarafina. Baada ya miezi mitatu toka nijuane na Harriet nilimtafitia kazi katika moja ya duka la nguo za wanawake na watoto. Baada ya kupata mshahara wa mwezi mmoja Harriet alitafuta chumba na kupanga. Vitu vyote vya ndani nilimnunulia mimi. Maisha mapya yalianza. Taratibu na ukaribu wangu mimi na Harriet ulizidi kuongezeka hatimae tulijikuta tukiangukia katika mapenzi. Kiukweli Harriet alikuwa msichana mzuri sana alikuwa na umbo zuri sana ambalo linamfanya mwanaume yeyote ashindwe kujizuia. Mapenzi ya siri bila kutambulishana kwa wazazi yalipamba moto.
Maisha yalizidi kwenda huku umarufu ukizidi kuongezeka zaidi. Ofisi yetu ilikuwa habari ya mjini. Kwa sherehe yoyote iliyokuwa inafanyika Mwanza. Kama mpigaji picha hatatoka kwetu basi sherehe inakuwa bado haijakamilika.
Maendeo ya studio yangu yalisababisha ninunue usafiri. Nilimiliki nyumba pia tulipangisha vyumba vitatu mtaa wa samaki samaki. Nilianza kufaidi matunda ya kazi yangu.
********************** ITAENDELEA


About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.