Asili: lebanese
MAHITAJI YA KUPIKA WALI WA TAMBI:
🔽Mchele vikombe 2
🔽Tambi vermicelli kikombe 1
🔽Ghee au mafuta vijiko 3 vya chakula
🔽Chumvi na pilipili manga kiasi
🔽Majani ya kotmir yalokatwa katwa fungu 1 au kiasi
🔽Maji vikombe 4
JINSI YA KUPIKA WALI WA TAMBI:-
1. Osha mchele mara mbili hadi 3 kisha loweka katika maji kwa muda wa dk 15.
2. Tia mafuta au ghee katika sufuria juu ya moto wa kiasi, yakipata moto tia tambi na zikaange hadi ziwe brown. (kuwa makini usiunguze)
3. Chuja maji mchele wako kisha tia katika sufuria pamoja na tambi kisha kaanga kwa muda wa dk 1-2
4. Tia chumvi na pilipili manga koroga vizuri kisha wacha uanze kuchemkia.
5. Punguza moto funika na acha uive taratibu hadi kukaukia vizuri. Epua kisha tupia kotmir na geuza taratibu na wali tayari kwa kula na mboga yoyote. Enjoy
🔽Furahia radha ya chakula cha nyumbani