MAHITAJI YA KUPIKA MUFFIN ZA ZABIBU:
🔸Unga wa ngano vikombe 2
🔸Sukari 2/3 kikombe
🔸Baking powder kijiko 1 cha cha chakula
🔸Chumvi 1/2 kijiko cha chai
🔸Mayai 2
🔸Maziwa kikombe 1
🔸Siagi iloyeyushwa 1/3 kikombe
🔸Vanilla kijiko 1 cha chai
🔸Zabibu mbichi vikombe 2, safisha vizuri
JINSI YA KUPIKA MUFFIN ZA ZABIBU
1. Washa oven joto 180°C. Kisha paka mafuta muffin tray. Weka pembeni.
2. Katika bakuli kubwa changanya vizuri unga, baking powder, chumvi na sukari. Weka pembeni
3. Katika bakuli lingine korogq kuchanganya maziwa, siagi pamoja na vanilla kisha mwagia katika mchanganyiko wa unga na changanya vizuri hadi unga uwe mtepe. (Usichanganye sana).
4. Nyunyiza sukari katika zabibu kisha tia katika mchanganyiko wa unga na zichanganye taratibu.
5. Chota unga wako kwa kijiko na tia katika muffin tray hakikisha haujazi hadi juu kisha tia katika oven na oka kwa muda wa dk 20 au hadi kiasi ukichoma kijiti kati chatoka safi.
6. Toa katika oven na wacha zipoe. Zikipoa zitakuwa tayari kwa kula kwa chai au kahawa.