MAHITAJI YA KUPIKA AVOCADO SALSA / KACHUMBARI YA PARACHICHI :
- 3 vjk vya kulia maji ya ndimu
- 2 vjk vya chai asali
- ⅛ kijiko cha chai chumvi
- ½ kijiko cha chai binzari nyembamba
- 1 punje ya kitunguu swaumu kilichopondwa
- ½ kitunguu maji kilichokatwa
- 6 majani ya vitunguu yaliyokatwa na toa kidogo kwa ajili ya kupamba
- ¼ kikombe majani ya giligilani yaliyokatwa na toa kidogo kwa ajili ya kupamba
- 3 parachichi makubwa,yaliyomenywa na kukatwakatwa vipande
- pilipili manga kiasi
JINSI YA KUPIKA AVOCADO SALSA / KACHUMBARI YA PARACHICHI:
- Changanya maji ya ndimu, asali, chumvi, binzari nyembamba na vitunguu swaumu katika bakuli ya size ya kati..changanya vizuri.
- Ongeza vitunguu maji na majani ya vitunguu koroga vizuri.
- Ongeza avocado na majani ya giligilani. Koroga polepole mpaka ichanganyike.
- Pamba kwa majani ya giligilani na majani ya vitunguu ulivyochota kidogo pembeni na weka na pilipili manga. Tayari kwa kula.