Notification texts go here Contact Us Buy Now!

Chumvi haitakufaa kwa chai asubuhi, ila itakufaa kwa mboga mchana

sivunje uhusiano na mtu sababu tu umegundua kuwa sio rafiki.


Kwenye maisha hatuhitaji marafiki tu. Tunahitaji watu wote.


Kila mtu atakufaa kwa namna tofauti. Hata wale wasio marafiki, kuna kipindi watakufaa.


Sio kila mtu atakufaa kwenye biashara au kipindi unatafuta kazi. 


Na sio kila mtu atakufaa kipindi unajiandaa na harusi yako au kipindi unatafuta mtu wa kukukopesha.


Pia, sio kila mtu atakufaa kipindi unaumwa au kipindi umefiwa.


Jambo moja tunalokosea ni kudhani kuwa *yupo mtu atakayetufaa kwa kila kitu.* Na kwa namna hiyo, tumepoteza watu wengi ambao wangekua na manufaa kwetu.


*Anaekufaa kwa kila kitu ni Mungu pekee.* Binadamu wote watakufaa tu kwa msimu.


Kinachotakiwa ni kutambua kila mtu anaekuzunguka anakufaa kwa nini, na kumtumia kwa hicho ambacho anakufaa.


*Usivunje urafiki wa miaka mitano sababu tu hakuja kwenye msiba ulipofiwa.* Ndani ya miaka mitano, hakukufaa kwa jambo jingine lolote lile?


Chumvi haitakufaa kwa chai asubuhi, ila itakufaa kwa mboga mchana.


Kila mtu atakufaa katika jambo tofauti na katika nyakati tofauti.


Mahusiano bora huongozwa na akili, na sio hisia...

*Nawatikia siku njema*

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.