Notification texts go here Contact Us Buy Now!

KUSTAAFU ⌛

*1*. *Siku moja utastaafu*👴🏿👵🏿.

Hautakua ukienda kazini,hautakua na madaraka tena,hautakua/utapungukiwa  na nguvu ya  ushawishi,mzunguko wako wa pesa utapungua❌💱!

Chunguza/fuatilia 🧐 tarehe yako ya  kustaafu kwenye risiti yako ya malipo ya mshahara🧾.


*2*. *Tumia siku zako za Likizo ya Mwaka*.📅

Chochote utakachokifanya Likizo ndio utakachokifanya ukistaafu.Kama unatumia likizo kulala 😴au kuagalia Luninga📺 ndicho utakachokifanya ukistaafu.Tumia wakati wako wa ziada kujifunza kitu👩🏿‍🏫,kitakuja kuwa na manufaa ukistaafu.


*3*. *Wekeza kwa ajili ya kustaafu kwako💰*.


👨‍👩‍👧‍👦Watoto wako sio uwekezaji kwa ajili ya kustaafu kwako.Usiwategemee watoto/ndugu/ marafiki kama benki yako🏧. Utapoteza heshima  na utu wako😔.


*4.Tafuta shughuli unayoipenda/unaifurahia* wakati bado upo kazini ikuongozee katika kustaafu kwako  mfano kufuga kuku 🐥🐓au miliki duka🏦.

📚Pata ujuzi unaojiuza (📄sio vyeti visivyo na matumizi)


*5.Utastaafia wapi*.

Jijengee nyumba.

🙅🏿‍♂Usistaafu ukiwa bado unapanga nyumba🏠.

🙅🏾Usigome kutoka kwenye nyumba ya serikali🏠.


*6.Ni nani watakua wategemezi wako*.


Wakati unastaafu watoto👨‍👩‍👧‍👦 wako wanatakiwa wawe wamevuka miaka 18 na wanajitegemea wenyewe👩🏾‍🌾👮🏾‍♀👩🏾‍⚕👷🏿👨🏾‍🍳👨🏿‍🏫👨🏿‍💻👨🏿‍🔧👨🏾‍✈.


*7.Usistaafu na ukaendelea kukaa katika jiji kubwa

labda endapo unajimudu kweli kweli💪🏾

Utakua na vyanzo vya fedha hafifu na itakuwia vigumu❌💱.

Ikiwezekana Hamia mahali penye gharama ndogo za maisha ili 💵pensheni yako ikusogeze mbali kidogo.


*8.Miliki mali inayoweza kukodishika au inayoweza kubadilika na kuwa Fedha taslim*

Miliki hisa zinazokunufaisha📈⚖.

Panda Miti ya biashara mfano mirunda🌳, mitiki🌳 nk, Fuga🐓🐐🐑🐖🐄, lima mboga mboga🍆🥬🥒🥕. 

Shughuli hizi zitakuingiza mapato💵 pamoja nakukufanya uwe mwenye afya💪🏾.


*9.Ishi maisha ya kawaida (maisha yasio na makuu🍕🍔🍟🍻)*


Kama hujajenga nyumba kijijini kwenu,

❌🏠usitumie pesa ya wastaafu kujenga,si busara kufanya hivyo, labda kama utageuza kijiji makazi yako ya kudumu📌.


*Tambua kwamba wastaafu wengi wanafariki 🚑mapema sababu ya mambo yafuatayo:-*


1.Hawajajiandaa🏋🏾🏋🏾‍♀ kiakili kustaafu.

2.Kukosa vipato❌💵.

3.Msongo wa mawazo🥺

4.Wanapatwa na  shinikizo la juu la damu/kisukari kutokana na 😟wasiwasi,😣uoga n a sintofahamu nyingi🤔 


*👨🏿‍💻MEZA YAKO PALE KAZINI SIO YA KUDUMU.🧰JIPANGE KWA AJILI YA KUSTAAFU.*

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.