JASTINA SEHEMU 9
ILIPOISHIA
Kwa kweli uzuri wake ulipitiliza sasa na kuanza kuwachanganya walimu pamoja na wafaunzi na kila aliepishana nae njiani. Wapo waliojikwaa na kudondoka, wapo waliokosa kupata ajali kwa kumshangaa pindi anapopita, lakini kwa Alwin yote hayo yalikuwa yakawaida sana ukizingatia yeye amekua nae. Wakiwa college ukaribu wao ulimjengea uhasama mkubwa Alwin na kujikuta akipewa vitisho mara kwa mara. "Jestina na Alwin munaitwa ofisini" aliingia mwanafunzi darasani na kutoa tangazo hilo. Bila kuchelewa waliinuka na kuelekea ofisini walipoitwa.
ENDELEA NAYO
"Vijana najua mtakuwa na maswali kwanini nimewaita" aliongea mwalimu mkuu huku akiwaangalia wawili hao kwa makini. "hivi punde tu nimepokea barua kutoka wizarani kuwa kumeandaliwa mashindano ya kielimu kwa ajili college zote hapa mjini na kwa kweli sisi tumekuwa wa mwisho kupata taarifa hiyo na mashindano yanatarajiwa kufanyika kesho kutwa" aliendelea kuongea mwalimu mkuu.
"Maswali yanahusu nini" aliuliza Jestina, "mengi yatakuwa ya kielimu hususan upande wa sayansi" alijibu mwalimu. "sawa sisi tumekubali kuiwakilisha shule" walijikuta wakiongea kwa pamoja kisha wakaangaliana na kutabasamu. "sawa basi mnaweza kwenda tukutakane kesho kutwa asubuhi" mwalimu mkuu aliwaruhusu na wao wakaondoka na kuelekea darasani huku kila mmoja akiwaza itakuwaje siku hiyo ambayo hata maandalizi hawakuwa nayo.
Muda wa mapumziko ulifika na wanafunzi wote wakatika madarasani kuelekea sehemu tafauti. "Habari yako Jestina" ilikuwa ni sauti iliotokea nyuma ya Jestina, "safi" alijibu huku akigeuka na macho yake yakagongana na kijana Matt, kijana huyo ni mtanashati sana na wengi wamempa jina la HANDSOME. "tunaweza kuongea kama utakuwa unanafasi" aliomba Matt, "sawa hamna shida" alijibu, hiyo ni sifa kubwa sana aliokuwa nayo Jestina, hakutumia uzuri wake kuwanyanyasa watu kama walivyo waschana wengi.
Waliongea mengi lakini madhumuni ya kikao hicho ilikuwa ni kijana Matt kumueleza Jestina hisia zake juu yake, na alionekana ni bingwa katika tasnia hii ya kutongoza maana hakuwa na historia ya kukataliwa na mwanamke yeyote yule aliemfata. Basi Jestina aliomba muda ili atafakari ombi hilo na kijana Matt hakufanya makosa ya kukubaliana na ombi hilo.
ITAENDELEA