MOYO ULIOJAA MAUMIVU
SEHEMU YA 09
Ilikuwa kazi kubwa na ambayo ilifanya kila kitu kuwa chepesi mno kwani watu hao walifanya kazi kwa nguvu kubwa na hatimaye kila mmoja kuamini kwamba zile picha zilieditiwa na hakukuwa na ukweli wowote ule.
Baada ya hapo, Theo aliendelea na maisha yake kama kawaida. Aliingiza kiasi kikubwa cha pesa, aliheshimiwa na kuonekana hakukuwa na msanii aliyekuwa na roho nzuri, mwenye nguvu ya kubadilisha hali yoyote ile isipokuwa yeye tu.
Pesa zilimnukia, alifanya kila kitu kwa umakini mkubwa, benki, mitandao ya simu, mashirika ya ndege na kampuni nyingine zilimfuata na kutaka kutangaza pamoja naye, kazi yake ikawa moja tu, kupiga pesa kila siku.
Alikuwa na mafanikio makubwa, akaunti yake ilikuwa na bilioni moja, alipambana kuhakikisha anakuwa na mafanikio zaidi ya hayo aliyokuwanayo kipindi hicho.
Baada ya kupita miaka miwili, huku akiwa na miaka ishirini na nne, Watanzania wakaanza kupiga kelele za kumtaka aoe na kujenga familia yake kwani miaka ilikuwa ikikatika na hakukuwa na yeyote ambaye alijua mwanaume huyo alikuwa akitoka na nani
Hicho ndicho kilikuwa kilio chake, ni kama kampeni kubwa ya kumtaka aoe ilianza kufanyika, kweye mitandao, watu waliweka mabango ya kumtaka mwanaume huyo amtafute mwanamke wa kumuoa ili maisha yake, utajiri wake uwe na mtu mwingine wa kumsimamia.
Mara ya kwanza alichukulia kama utani lakini baada ya siku kuendelea kwenda mbele huku Watanzania wakimsisitizia, aliamini kwamba kweli wakati huo waliamua, walihitaji kumjua mwanamke aliyekuwa na bahati ya kuolewa naye.
“Nioe?” alijiuliza.
*
*
*
Je, nini kitaendelea?
