MAHITAJI YA KUPIKA KASHATA ZA UNGA WA UBUYU
- -unga Wa ubuyu 1/2
- -sukari 1/2
- - Rangi kijiko 1 cha chakula
- -vanilla kifuniko 1
- - Maji vikombe 2
- -pilipi manga
Jinsi ya kupika kashata za unga Wa ubuyu
- Chukua unga Wa ubuyu chekecha upate ule mzuri na safi ,
- kisha weka maji yako jikoni tia sukari ,Rangi ,vanilla na pilipili manga kisha koroga mpaka uone mchanganyiko wako unatoa povu na ukigusa unanata ,
- weka unga wako anza kusonga kama ugali hivi ,
- andaaa sinia paka mafuta epulia hapo kisha usukume na sukumio la chapati kisha kata dizaini upendayo .
- Enjoy kashata za ubuyu.