Inasemekana
*MAMBO yanayosababisha baadhi ya makundi ya whasapp kufa. (Inaweza ikawauma wengine lakini ndio ukweli)*
*1. Mtu anaweza akatoa mada na hakuna mtu akachangia na wakati huo huo mtu mwingine akatoa wazo watu wakachangia faster. Je kuna watu wana umuhimu kuliko watu wengine?*
*2. Kutokujibu salamu hasa hasa pale aliyetoa siyo rafiki yako. ....ubaguzi!*
*3. Baadhi ya watu katika kundi hujifanya ni zaidi ya wengine hata kudharau wengine.*
*4. Baadhi ya watu katika kundi ni viburi na wajivuni...wapo katika kundi lakini hawachangii wala kuunga mkono na wakati wao wakisema jambo, wanataka wengine wote kukubaliana na maoni yao.*
*5. Baadhi ya watu hawachangii jambo lolote la msingi isipokuwa vichekesho na vituko tu!*
*6. Baadhi ya watu hawajui jinsi ya kuzungumza*
*7. Baadhi ya watu wanapapara*
8.Wengine hawachangii chochote ila kazi yao ni kuja na mitazamo hasi tu.
*9. Baadhi ya wanachama wapo wapo tu yaani kama wasimamia au kutazama mechi ya mpira wa miguu.*