Notification texts go here Contact Us Buy Now!
Machapisho

Uvumilivu kufanywa Ishara ya Mapenzi

Hii ni aina nyingine ya matarajio ambayo sio halisi kwani kiukweli kila mtu analo jukumu la kufanya bidii kuwa mtu mwema, hivyo hauhitaji kubeba ‘uzembe’ wa mwingine kwa kisingizio tuu cha kuwa unaonyesha upendo hususani pale ambapo ni kwa uzembe tuu au kutokujali kwake mwenza husika amefanya jambo fulani.


Kwa jinsi kasumba hii ilivyo enea sio ajabu kukuta mtu akifanya mambo mabaya kwa mwenza wake kwa makusudi ili tuu eti apime kama kweli mwenza wake ni mvumilivu.


Kumbuka hapa hatumaanishi kuwa kusamehe ni kosa. Hapana, kusameheana ni muhimu, lakini sio kwamba ni muhimu tuu katika mapenzi. Kusameheana ni jambo la asili, na tunapaswa kusameheana kwa mambo mengi nje hata ya mahusiano. 


Tunachosema ni kuwa kuna  kasumba ya baadhi yetu kuona kuwa wanayo ‘haki’ ya msingi ya kukosea eti tuu kwakuwa tuu mwenza wake analazimika kusamehe ili kuonyesha kweli anao upendo wa dhati.

Amini usiamini, kasumba hii ya kutarajia aina ya pekee ya kusamehewa na kuvumiliwa kwa kisingizio tuu cha kuwa upo kwenye mapenzi na mwenza wako, hurudisha nyuma maendeleo ya mahusiano yenu kwani mwenzi wako nae ni binadamu na kumbuka anayo matarajio mengine ya maisha, isitoshe na yeye anahitaji upendo na kujaliwa na wewe, hivyo kutarajia kwako kusamehewa na kuvumiliwa kuna mnyima haki mwenza wako.

Hatimaye kutegemea kwako kusamehewa kila wakati, kunamfanya mwenza wako atilie mashaka upendo wako kwake.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.