Notification texts go here Contact Us Buy Now!

Fahamu kuhusu mkojo, Rangi ya mkojo, harufu na idadi mrangapi uende kukojoa

Mkojo ni sehemu muhimu sana ya utoaji wa taka mwilini.Kazi yake kubwa nikuondoa maji ya ziada na uchafu unaojichanganya baada ya damu kuchujwa na figo.

*JIFUNZE KUHUSU MKOJO,RANGI YA MKOJO,HARUFU YAKE PAMOJA NA IDADI MARA NGAPI UENDE KUKOJOA*


Mkojo ni sehemu muhimu sana ya utoaji wa taka mwilini.Kazi yake kubwa nikuondoa maji ya ziada na uchafu unaojichanganya baada ya damu kuchujwa na figo.


KWANINI MKOJO WA RANGI/KWANINI MKOJO WENYE HARUFU KALI

HII NIKWA SABABU YA VITU VINGI NDANI,bacteria,protein na sukar ya ziada,Hutoka pamoja na mkojo,hivyo uwapo wake wake kweny mkojo hutambulisha tatizo.

-Mkojo ni sehemu ya msingi sana yakutoa sumu na vitu ambavyo pengine vingejijenga ndani ya mwili nakusababisha madhara,hivy unapogundua mkojo wako umebadilika rangi au una harufu kali wakati unakojoa,inaweza kuwa ni dalili ya tatizo kubwa la njia ya mkojo kama maambukizi au SARATANI.

*RANGI YA MKOJO*

-Mkojo hupata rangi yake ya njano kutoka kwenye *_Urochrome_*.Hakuna rangi maalum ya mkojo wa kawaida,mara nyingi rangi ya mkojo hutofautiana kwa mtu na mtu.kutoka njano mpauko,njano iliyo kolea au rangi ya asali huchangiwa na kiwango cha Maji pia.

-Mwili wako unahitaji kiwango fulani cha maji ili ufanye kazi vizuri,hivy kutokunywa maji vya kutosha husababisha mkojo kuwa mzito na ulio kolea rangi.

-Mkojo ukiwa na rangi ya njano mpauko,inaweza ikamaanisha unakunywa maji,maji yakikosekana kemikali zilizopo kwenye mkojo zinaufanya uonekane kukolea njano na jinsi maji yanavyoongezeka ndivyo hivyo rangi hupotea.

-Rangi ya mkojo inaweza pia kuwa ni ishara ya dawa fulani ulizotumia,Mkojo unaweza ukabadilika badilika ukawa wa rangi tofauti.Baadhi ya dawa huubadilisha na kuufanya uwe wa kijani au blue iliyofifia.Ulaji wa karoti hufanya mkojo kuwa wa rangi ya machungwa,wakati vitamins mbalimbali hufanya mkojo kubadilika nakuwa mwekundu hii ni ishara kuwa kuna damu kwenye mkojo.

-Damu kidogo kwenye mkojo ni dalili kwamba kuna tatzo kubwa kama maambukizi ya njia ya mkojo,hali hiyo unapo iona ni muhimu sana kukimbia kwenye vipimo.Kama unahisi damu kwenye mkojo wako ukiwa wenye hali ya mawingu hii inaweza kuashiria ugonjwa umekomaa zaidi.



*HARUFU YA MKOJO*

-Kwa kawaida mkojo hauna harufu kali.Ukihisi harufu kali ya mkojo wako ama wa dawa au wa kitu chchte kile hii inamaanisha moja kwa moja una ugonjwa au mawe kwenye njia ya mkojo (kumbuka njia ya mkojo figo zinahusika pia).

-Magonjwa yanaweza kutengeneza harufu kali inayo fanana na AMONIA.Harufu ya Amonia ni kali ambayo inafanana na harufu ya ukuta uliokojolewa kwa muda mrefu na walevi (watu wanao tumia pombe)

-Wagonjwa wa sukar pia wanaweza kuona mkojo wao una harufu inayo wavutia kutokana na sukari ya ziada iliyopo.

-Baadhi ya vyakula pia hubadilisha rangi ya mkojo chakula kama parachichi.

-Harufu kidogo ya mkojo (isiyo sana) huwa inatokana na utengenezwaji wa kampaundi iitwayo _*Methyl Mercaptam*_,ambayo inapatikana pia kwenye kitunguu swaum.

*JE UKOJOE MARA NGAPI!??*

-Idadi ya safar za kwenda kukojoa ni muhimu kama ilivyo tu rangi na harufu yake katika kutambua hali ya Afya ya mtu.

-Watu wengi hukojoa mara 6 hadi 8 kila siku,lakini unaweza ukakojoa mara nyingi zaidi kutegemea ni kiasi gani cha maji,vinywaji au vyakula ulivy tumia.

-Iwapo unahisi kukojoa mara kwa mara na hukunywa maji yakutosha hii nayo ni tatizo na mara nyingi ni U.T.I au tatizo la kibofu linalo kifanya kiwe na uvimbe.

-Kibofu kikivimba kinafanya uhisi kujaa na kutaka kukojoa mara kwa mara.

-Sababu kubwa inayo mfanya mtu akojoe mara kwa mara nikuvimba tezi dume (prostate),kuugua kisukari na magonjwa ya mfumo wa fahama.

-Ikiwa mtu haendi kukojoa vya kutosha inaweza ikamaanisha kuziba kwa mirija au maambukiz yanayo weza kuwa nikwasababu ya tabia uliyo jijengea yakijizuia kukojoa.

-Watu wengi ambao huchelewa kwenda kukojoa kwasabab ya shughul zao kuna uwezekano mkubwa wakapata matatizo kwenye kibofu hii nikwasabab yakulazimishwa kusinyaa hata kama mkojo umejaa.

-Ili kulinda kibofu chako kunywa maji angalau wastan wa lita 3 mpka 4 kwa siku.

-Ikiwa una tatizo la kuamka usiku kukojoa mara kwa mara basi acha kunywa maji masaa 3 mpka 4 kabla yakulala.

-Epuka na Acha kabisa matumizi ya pombe ni hatar kwenye mfumo huu

-Epuka na Acha vinywaji vyenye Cafein kama Chai kwakuwa husisimua ukuta wa kibofu,mbadala wake unaweza ukatumia maji yenye *tangawizi,asali mbichi,Cow Calcium milk Cand au ile Ginseng*


UFANYE NINI KWANZA WAKATI UKIJIANDAA KWENDA HOSPITAL!!

1. Chukua _Limau/ndimu_
Weka vijiko vikubwa vitano vya juisi ya limau au ndimu na uongeze maji ili kupata robo lita (ml 250) na unywe kutwa mara tatu. Pia unaweza kuongeza asali vijiko vikubwa vitatu ndani yake. Mchanganyiko huu wa limau na maji ya uvuguvugu utakuondolea maumivu yatokanayo na maambukizi na hata kuzuia kutokwa na damu kama tatizo halijawa sugu.

2.Unga wa majani ya Mlonge
Tumia kijiko kimoja cha chakula ndani ya uji, au ndani ya juisi ya matunda kikombe kimoja (robo lita) juisi uliyotengeneza mwenyewe, au katika maji ya uvuguvugu kijiko kimoja kikombe kimoja cha maji (robo lita) kutwa mara tatu au unaweza pia kuongeza kijiko kimoja cha unga wa mlonge kwenye mboga ya aina yoyote au katika wali. Tumia kwa mwezi mmoja mpaka mitatu au tumia tu muda wote kama kinga ya mwili wako dhidi ya magonjwa yote,kumbuka vitu hivi viwili si tiba ya moja kwa moja ya kukuponyesha ila inakukinga nakukupunguzia tatizo


About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.