Watu wengi wamekuwa wakipata ma mfupi wa kulala kutokana na shuhuli nyingi kama vile kazi au masomo au pia kwa ajili ya starehe zako binafsi sana sana kwa wale wanaopenda kukesha kuangalia movie usiku kucha na kujikuta haupati usingizi au unalala kwa mda mfupi sana.
Mimi ni mmoja ya watu ambao nina tabia ya kutumia laptop yangu sana hasa nyakati za usiku huwa naandika post nyingi sana muda wa usiku na wakati mwingine najikuta nalala lisaa au masaa mawili au matatu. kwahyo kwa kipindi kirefu nikajikuta system yangu ya kulala imebadilika kuwa sipati usingi nyakati za usiku ambao ndio mda niliotakiwa kulala na mchana nikawa nakosa concetration katika kazi zangu, ndipo nilipoamua kuingi google na kutafuta sababu za mimi kutokuwa na concetration na kupoteza focus katika kazi ndipo nilikutana na article iliolezea sababu kuu ya tatizo hilo ni kutokumzisha mwili hasa nyakati za usiku. Na madhara ya kuto lala hasa nyakati za usiku ni mengi ni kama vile
- kuongezeka kwa stress hormone (cartisol) mwilini
- kupungua uwezo wa kufikiri na kukumbuka (loss of memory)
- kutokujiamini au kukosaimani kwa watu uwapendao (relationship stress).
- uongeza uwezekano wa kupata ajali hasa wanao tumia vyombo vya usafiri.
- kupungua kwa utendaji kazi wa mwili.
- kupunguza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake na kukosa nguvu za kiume kwa wanaume.
Tabia hii ya kukosa usingizi au kuto kulala ikiendelea kwa muda mrefu upelekea magonjwa sugu kama kisukari, heart attack, heart failure/strock, msongo wa mawazo(depression) na kukosa hamu ya tendo la ndoa kabisa
TAARIFA ZINGINE MUHIMU:
DONDOO 9 MUHIMU SANA KWA WALEZI/WAZAZI NA WAZAZI WATARAJIWA WOTE