🌿Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.
🌿Usiruhusu mtu yoyote amwite mwanao “Mchumba”, “Mke wangu” au “Mme wangu”.
🌿Kila wakati mwanao anapoenda kucheza na wenzake, hakikisha unafuatilia kujua wanacheza nini, siku hizi hata watoto wanafundishana michezo michafu na wengine wana maambukizi....
🌿Kama mwanao ameonyesha kutopenda kwenda kwa mtu fulani usimlazimishe, pia chunguza kwa ukaribu ili kujua sababu.
🌿Inashauriwa kupitia kwanza mwenyewe movie yoyote kabla ya kuruhusu mwanao waiangalie.
🌿Mwanao anapofikisha umri wa miaka 3 anza kumfundisha jinsi ya kusafisha sehemu zake za siri mwenyewe, na umuonye asiruhusu mtu yoyote kumshika sehemu hizo.
🌿Mfundishe mwanao thamani ya kuishi bila kufuata mkumbo.
🌿Mwanao akilalamika kuhusu mtu fulani, usikae kimya.
🌿Usipende kumruhusu mwanao kulala na housegirl au houseboy au mgeni. Huwezi jua tabia za watu na wanayomtendea usiku!!!!
*_Kama unadhani Dondoo hizi ni Muhimu.Tafadhali soma na uwapelekee wengine.
*Dondoo 9 muhimu sana kwa walezi /Wazazi na Wazazi watarajiwa wote*
Usivue nguo mbele ya mwanao pindi akifikisha miaka 2 au zaidi. Jifunze kumwomba akupishe.