Notification texts go here Contact Us Buy Now!

EPUKA TABIA HII, VINGINEVYO UTAKUFA MASIKINI

EPUKA TABIA HII, VINGINEVYO UTAKUFA MASIKINI


Source 👉 Isaack Nsumba 


Katika maisha kuna kitu kinaitwa INSTANT GRATIFICATION, ni kitu hatari sana katika mustakabali wa maisha yetu, sifahamu maana nzuri ya Instant gratification kwa KISWAHILI lakini kwa ufupi unaweza kusema👇


Ni ile hali ya kuishi kwa kutaka kuwadhihirishia watu kuwa umefanikiwa ilhali yakua bado haujafanikiwa.


Au kwa tafsiri nyepesi unaweza kusema ni ile hali ya kuishi kwa mashindano, na mara nyingi hali hii huwakuta zaidi👇


(1) WASOMI

(2) WAAJIRIWA

(3) WANAWAKE


-Pamoja na Watu wote wanao ishi kwa MASHINDANO, kwamfano 👇


Mtu unaajiriwa then mwaka wa kwanza tu unataka ununue Gari ambalo halikuingizii pesa mfukoni bali linachukua pesa mfukoni kwako.


Gari ambalo litakuhitaji kila siku uweke mafuta ya kwenda ofisini na kurudi bila kusahau pesa za matengenezo, sasa je, kwa hali hii utatoboa kweli?.


Au kijana umemaliza CHUO, huna kazi inayoeleweka mjini lakini unaishi geto la elfu 60 kwa mwezi, lengo lako kubwa watoto wakali wasione kuwa unaishi geto bovu.


MDADA au MMAMA, unaenda kukopa pesa kwenye vikoba kwa lengo la kununua nguo za gharama, simu kali, vyombo vya ndani, kabati na vinginevyo kisa tuu umemuona jirani yako kila siku anabadilisha nguo mpya au anashusha vitu vipya kila siku.


Hebu nambie, kwa style hii ya maisha utatoboa kweli???.... anyways ukitoboa niko pale nimekaa njoo uniite MBWA 😡


Sasa hapa naomba nisieleweke vibaya maana hamchelewi nyie(Nawajua 😂) ni hivi, kusema yote haya sina maana kuwa labda nazuia au kupingana na tabia ya watu kupendeza au kuvaa vizuri(Lahasha).


Haimaanishi kuwa nazuia watu wasinunue magari au vitu vizuri(NO), ila ninachojaribu kukuzuia mimi ni kuishi MAISHA kwa kutaka kuwadhihirishia watu kuwa umefanikiwa(Ilo tuu basi).


Au labda ngoja nikuulize kitu ndugu yangu, ni kwanini basi hiyo hela unayotumia kutaka kudhihirishia watu kuwa umefanikiwa, usiitumie kama mbegu kwaajili ya maisha ya baadae?.


Kwanini usiwekeze kwenye BIASHARA, ukanunua viwanja au vitu ambavyo THAMANI yake inaongezeka kila baada ya muda flani?.


Alafu kitu kingine usicho kijua ni kwamba, ukiwa na pesa hautohitaji kutumia nguvu nyingi kutuonesha kwamba una hela, tutajua tu automatic maana PESA inaongea.


Mwisho kabisa kwa wale wenye familia, wapenzi, wachumba n.k...hakikisha mwenza wako anafahamu hali yako ya kiuchumi.


Mfanye afahamu kwamba bado upo kwenye utafutaji vinginevyo ukiishi kitajiri na yeye ataishi kitajiri lakini ukimtengenezea MAZINGIRA ya yeye kujua kuwa bado upo kwenye utafutaji basi hata yeye atakuhurumia katika matumizi ya kila siku na bila shaka mwisho wa siku mtafika mbali kimaendeleo.


Anyways, yangu ni hayo na ikumbukwe maneno yangu si SHERIA, kwahiyo ukiona ni kama nakupangia MAISHA fanya kama andiko hili hujawahi kuliona ila ipo siku utanikumbuka 😂

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.