Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JIJI LA KICHAWI SEHEMU YA MWISHO

JIJI LA KICHAWI

SIMULIZI ZA JOSHUA / 8 months ago

JIJI LA KICHAWI (MWISHO)

Binti Yule alianza kumnyonga isaya kichawi ,isaya alilia sana alitoa sauti ya uchungu sana

``kwiiiii kwiiii nakufa nisamehe mpenzi wangu ,nisamehe tafadhali’’

``haya umejua kosa lako’

```ndio nimejua sasa’’

``nini sema haraka lasivyo nakutoa uhai sasa hivi ‘’

``nimetongoza mwanamke na uliniambia nisitongoze mwanamke yoyote’’

``hahahahhahh kumbe unajua eee sasa ikawaje?????’’

JE NINI KITAENDELEA…………………………

Isaya alipewa adhabu ya hali ya juu dada Yule wakichawi alimpiga kofi sehemu ya kisogoni

Ghafla isaya alijikuta akiwa katika ulimwengu mwingine kabisa

Alijikuta yupo ndani yam situ mkubwa sana ,kila upande aliokuwepo hakuona mtu alizunguka kila mahali huku akipiga kelele ila haukupatikana msaada wowote

Isaya aliangalia juu mawinguni na kujisemea

``eeeee MUNGU wangu nimekukosea nini mja wako ,nisamehe kama nimekuudhi sijui kwanini napatwa na mambo kama haya ‘’

Isaya akiwa amejiinamia chini alihisi mkono wa mtu ukimgusa kisogoni ,ghafla alijikuta akiwa kitandani huku akitetemeka sana ,isaya aliinuka kutoka kitandani usiku ule na kukimbia mpaka kwa boss wake alijisemea moyoni ``nimechoka maisha haya ya ajabu jiji la ajabu hili lazima niondoke ngoja nikamkabidhi boss funguo zake’’


Isaya aliondoka kwa haraka hadi mlangoni kwa boss ilikua ni saa nane za usiku

``hodiiii hodiii’’

Akiwa anabisha hodi walinzi walimkamata

``wewe nini sasa hivi watu wamelala sasa unasumbua’’

Isaya alibidi kurudi nyumbani


Alipofika ndani alipokelewa na kiicheko

``hahahahahaah umeenda kunishtaki siyo’’

Binti Yule alijitokeza tena ,isaya huku akitetemeka alijibu

``nisamehe pia niache niishi maisha yangu nisamehe tafadhali’’

Dada Yule alijibu

``umekosea mwenyewe ‘’


Ilipofika asubuhi kazi iliendelea kama kawaida isaya alijibidisha kufanya kazi na kujitahidi kusahau yote yaliyomkuta ,siku zilienda isaya akiteswa sana na dada Yule wakichawi mara nyingi alichukuliwa usiku na kulazimishwa kufanya mapenzi na majini ,isaya hakupenda maisha hayo ila hakua na namna

Siku moja isaya akiwa anatoka kazini alikutana na baba mmoja akiwa ameshikilia biblia kubwa mkononi

Baba Yule alimsalimu

```habari yako kaka’’

``shwari vipi’’

``salama ndugu unaendeleaje mpendwa ‘’

``gudi nini shida’’

``ndugu Mungu kaniongoza kuwa upon a tatizo kubwa sana’’

``nini wewe nyie ndio wale matapeli manajikuta waatumishi wa Mungu’’

``Mungu akusamehe sana ndugu mimi sio kama hao’’

``ok sema na shida gani mbwa wewe nitakuitia polisi hapa tapeli wewe’’

Isaya alikua ni mtata sana na mkorofi kupita maelezo alitamani kumpiga mzee wa watu

Mzee Yule alianza kuongea

``sikia kaka una tatizo kubwa sana ndugu ,

``tatizo gani acha maneno lete mambo’’

``unasumbuliwa na nguvu za kichawi hapo ulipo dada wa kichawi ameweka agano na wewe mara nyingi unachukuliwa usiku kufanya nao mapenzi’’

Isaya alivyosikia hivyo alishindwa kuvumilia alidondoka moja kwa moja chini kwa uoga

Mchungaji Yule alianza kukemea mapepo yote ,ndani ya muda kidogo kama dakika kumi na tano isaya alinyanyuka akiwa mzima na mwenye nguvu

Alimshukuru mtumishi Yule na kuahidi kujiunga na kanisa lake

Maisha yaliendelea isaya hakupata tena usumbufu maishani aliishi kwa raha mustarehe hakuamini kama ni yeye angeweza kuishi katika jiji la wachawi kwa amani na utulivu

…………………………………… MWISHO……………………….

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.