NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA
Mtunzi Nyemo Chilongani
Katika kipindi hicho nilikuwa na furaha sana kwa sababu ndoto zangu ambazo nilijiwekea katika maisha yangu niliziona kuanza kutimia katika muda mchache ujao.
Katika kipindi chote ambacho nilikuwa katika chuo hicho nikipata elimu yangu, kichwani mwangu kulikuwa na ndoto nyingi, ndoto za kuwa mwandishi mkubwa ambaye ningekuja kuheshimika na jamii yote, mwandishi ambaye ningeweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta zote za uandishi nchini Tanzania.
Kila nilipokuwa nikimwangalia mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Charles Hilary, nikajiona nikizidi kupata nguvu zaidi za kusoma kwa sana, nilitamani sana kuwa kama yeye katika maisha yangu.
Nilikuwa na kiu sana ya kuwa mwandishi bora na kisha kutafuta nafasi ya kutangaza katika shirika lolote kubwa la Habari kama la BBC, CNN, Al Jazeera au shirika lolote ambalo lilikuwa likitambulika kimataifa.
Hapo ndipo ambapo nilipofikiria kitu kimoja ambacho nilitakiwa kufanya, kitu ambacho kingekuwa cha hatari sana katika maisha yangu.
Nakumbuka siku hiyo mara baada ya kutoka katika ‘field’ yangu niliyoifanyia katika kituo cha utangazaji cha Global TV, nikarudi nyumbani na kutulia chumbani kwangu.
Siku hiyo sikuonekana kuwa na furaha kabisa, kichwa changu kilikuwa kikifikiria ni kwa namna gani ningeweza kuwaambia wazazi wangu kuhusu kile nilichokuwa nikikifikiria kichwani mwangu.
Kiukweli nilihitaji sana ushirikiano kutoka kwa wazazi wangu, wao ndiyo walikuwa watu sahihi ambao kamwe wasingeweza kunishauri kitu kibaya.
Nilitulia chumbani kwangu kitandani, hakukuwa na siku ambayo niliwaona wazazi wangu wakichelewa kurudi nyumbani kama siku hiyo.
Muda wote macho yangu yalikuwa yakiangalia saa yangu ya mkononi, nilitamani sana waingie nyumbani hapo na kuwaambia kile nichokuwa nimepanga kuwaambia.
Saa 2:23 usiku nikasikia muungurumo wa gari kutoka nje ya nyumba yetu, sikutaka kujiuliza zaidi, nikajua fika kwamba wazazi wangu walikuwa wakiingia ndani ya eneo la nyumba yetu.
Sikutaka kutoka wala kuonyesha kwamba nina presha, nikatulia chumbani mpaka pale walipoingia ndani na kuelekea chumbani kwao.
Baadaye walipotoka kwa ajili ya kula chakula cha usiku, nikaelekea mezani na kuanza kula pamoja nao.
Kwa wakati huo kichwa changu kilikuwa kikifikiria mengi, sikujua kama wangeweza kunielewa juu ya kile nilichotaka kuwaambia. Katika kipindi chote ambacho tulikuwa tukila, muonekano wangu ulionekana kuwa si wa kawaida, nilionekana kuwa na kitu moyoni mwangu.
“Thomas!” niliisikia sauti ya baba ikiniita, nikashtuka kutoka katika lindi la mawazo.
“Naam!” niliitikia huku nikionekana kushtuka.
“Unawaza nini?” aliniuliza baba huku akiacha kula.
“Siwazi kitu baba,” nilimwambia huku macho yangu yakionyesha dhahiri kwamba nilimdanganya.
“Hapana. Hauko kawaida leo. Hebu tueleze unawaza nini,” aliniambia.
Nilibaki kimya kwa muda, nikaanza kufikiria ni kitu gani nilichotakiwa kuwaambia. Nikaanza kujiuliza kama lilikuwa jambo sahihi kuwaambia kile nilichopanga kuwaambia ili wanishauri au nilitakiwa kukaa kimya na kuwashtukiza hapo baadaye.
“Kuna nini kipenzi,” mama aliingilia kwa kuniuliza swali. Nikayapeleka macho yangu usoni mwake.
“Nataka kuwa mwandishi mkubwa wa habari,” niliwaambia.
“Hilo tunalifahamu na umekuwa ukituambia kila siku. Nakumbuka huwa unatuambia kwamba unataka kuwa kama Charles Hilary, si ndiyo?” aliniambia baba na kuniuliza.
“Ndiyo. Natamani sana nifanye kazi katika mashirika makubwa ya habari duniani,” niliwaambia.
“Kila kitu kinaanza kwa hatua Thomas, huwezi kuwa mwandishi mkubwa wa habari na wakati haujapitia katika mashirika madogo.
Unakumbuka kuwa hata Charles Hilary kabla ya kujiunga na BBC alikuwa akifanya kazi ITV?” baba alisema na kuniuliza.
“Nakumbuka.”
“Basi hutakiwi kuwa na presha. Kuna siku utakuwa mwandishi mkubwa tu,” aliniambia.
“Kuna kitu nimekifikiria na ningehitaji ushauri wenu,” niliwaambia.
“Kitu gani?”
“Nataka nitengeneze makala yangu ihusuyo mambo fulani, na kama ikiwezekana basi nisafiri,” niliwaambia.
“Kuandaa makala yahitaji utulivu mkubwa sana.
Wewe unataka kusafiri kuelekea wapi kuiandika hiyo makala yako?” baba aliniuliza.
“Nataka kwenda Darfur, nchini Sudan,” niliwaambia.
Kila mmoja akashtuka, wote wakaacha kula na kuniangalia kwa macho yaliyoonyesha kutokuamini kile nilichokisema.
Wakanikazia macho zaidi, nilionekana kuongea kitu kilichowashtua mno. Nikamuona baba akiisogeza sahani yake mbele kuonyesha kwamba alikuwa ameshiba.
“Unasemaje?” aliniuliza huku akionekana kushtuka.
“Nataka kwenda Darfur,” nilimjibu.
Chakula hakikulika tena, kila mmoja alionekana kushiba, maneno niliyowaambia kwamba nilitaka kwenda nchini Sudan tena katika Mji wa Darfur yaliwashtua sana. Waliufahamu vilivyo mji huo na yale mauaji yaliyokuwa yakiendelea huko.
Hapa ningependa kuwaambia wale watu ambao hawakuwa wakiijua hii Darfur ambayo nilikuwa nimeizungumzia mahali hapo. Darfur ni mji mkubwa ambao unapatikana nchini Sudan. Mji huu ndiyo umekuwa na machafuko mengi ambayo yamepelekea nchi nzima kutokuwa na maelewano.
Watu walikuwa wakiishi kwa hofu huko, wakulima walihofia kuelekea mashambani mwao jambo ambalo lilipelekea nchi kuingia katika njaa kali.
Nchi hii ilionekana kama kuwa na laana kwani toka kipindi ambacho machafuko hayo yalianza, mvua nazo zilianza kunyesha kwa nadra sana.
Waandishi wa habari waliokuwa wakielekea katika mji huo wengi kuuawa kinyama kwa sababu wao wenyewe hawakutaka kufuatiliwa na maisha yao au kitu chochote kilichokuwa kikiendelea huko.
Nilibaki pale mezani kwa muda, mara nikaichukua simu yangu na kisha kumpigia simu mpenzi wangu niliyekuwa nae katika kipindi kile, Myra na kisha kumwambia kile ambacho nilikuwa nimekifikiria kukifanya kwa wakati ule.
Nilipompa taarifa Myra, nae alikuwa sawa na wazazi wangu, alikataa kata kata kunikubalia nielekee nchini Sudan.
“Hapana mpenzi” Myra aliniambia kwa sauti iliyojaa wasiwasi.
“Itanibidi nifanye hivyo Mage. Ni lazima niende Sudan. Haijalishi wewe hautaki au wazazi wangu hawataki, NI LAZIMA nilekee Sudan” Nilimwambia Myra.
Huo ndio uamuzi ambao nilikuwa nimeupanga.
Nikaanza kufikiria gharama ambazo zingenigharimu mpaka kukamilisha kila kitu, kitu cha kwanza kilikuwa kamera, nilihitaji kuwa na kamera ya video na ya picha. Pia nikahitaji kuwa na begi kubwa la mgongoni pamoja na kiasi fulani cha fedha ambacho kingeniwezesha kukitumia katika kipindi ambacho ningekwenda nchini Sudan.
Vitu hivyo havikuwa na shida sana, pia nilitakiwa kuwa na kitambulisho cha uandishi wa habari ambacho ningekionyesha kwa kila mtu ambaye angetaka kukiona hasa wale wafuasi wa upande wa pili ambao walikuwa kinyume na serikali ya Sudan.
Hapa ndipo nilipoamua kuwasiliana na rafiki yangu, Hamza Kimosa ambaye nilimwambia anitengenezee kitabulisho cha uandishi wa habari cha shirika la Aljazeera huku nikiwa nimemtumia picha ya itambulisho hicho ambayo niliipata kwenye mtandao.
“Ni LAZIMA niende Darfur hata kama hawataki. Hata kuwatoroka nitawatoroka tu” Nilijisemea katika kipindi ambacho nilikuwa nikielekea chumbani kwangu.
*
Nilichukia sana na wala sikutaka kuongea nao, niliwaona kuwa kama wasaliti katika maisha yangu ambao hawakutaka kuniruhusu kufanya kitu ambacho kingenifanya kufaidika katika maisha yangu.
Siku iliyofuata nikaanza kuondoka kuelekea nyumbani alipokuwa akiishi Hamza, rafiki yangu ambaye alikuwa mtaalamu na mambo ya Graphic.
Nilimkuta Hamza na hivyo kumtaka anionyeshee kitambulisho cha mwandishi wa habari wa shirika la habari la Aljazeera na kisha kunionyeshea.
Kitambulisho kile kilionekana kutengenezwa katika utaalamu wa hali ya juu, japokuwa kilikuwa kikionekana kwenye kompyuta lakini kilionekana kuvutia sana.
“Kwa hiyo jina niweke Thomas Chilongani kama kawaida au?” Hamza aliniuliza.
“Nope. Weka Iqram Ibrahim” Nilimwambia.
Pale pale Hamza akabadilisha na kisha kuliweka jina lile.
Kichwani mwangu nilikwishajua kwamba katika kipindi kile nilikuwa nikielekea katika nchi ambayo ilikuwa na waumini wengi wa dini ya Kiislamu, hivyo nilihakikisha kwamba nafanya kila jitihada ili nionekane kuwa mtu wao ili hata kama nitahitaji vitu fulani kutoka kwao basi niweze kuvipata kwa urahisi.
Siku hiyo nilikamilisha kila kitu kilichokuwa kikihitajika na kisha kuondoka kuelekea nyumbani.
Nilichokifanya kwa wakati huo ni kuelekea katika mashine ya ATM na kisha kuchukua kiasi cha fedha cha shilingi milioni mbili na kuanza kuelekea Posta kwa ajili ya manunuzi ya kamera.
Nikapata kamera mbili ambazo zilionekana kuwa bora na kuanza kurudi nyumbani.
Kwa wakati huo, nilitaka kufanya mambo yangu kwa siri sana, sikutaka mtu yeyote nyumbani afahamu kwani kwa kuwafanya wafahamu basi wangeweza kunizuia kwenda kwa kutumia maneno yao ya kunikatisha tamaa na kunitisha.
Ingawa nchi ambayo nilikuwa ikielekea katika kipindi hicho ilionekana kuwa nchi ya hatari, lakini moyoni mwangu wala sikuonekana kuwa na wasiwasi wowote ule, nilikuwa nikizidi kujipa matumaini kwamba kila kitu kingekwenda kama ambavyo kilitakiwa kiwe.
Nilipanga kuandaa makala moja kubwa na ya maana sana katika kila chombo cha habari ambacho kingediriki kuonyesha makala hiyo ambayo ilikuwa imeandaliwa na kijana mbunifu ambaye alikuwa na uwezo wa kuelezea mambo mengi kwa undani zaidi, Thomas Chilongani.
Saa 11:15 jioni, ndege ikaanza kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum uliokuwa katika jiji la Khartoum.
Hali ya hewa haikuwa nzuri sana, joto liionekana kuwa juu kwa kiasi fulani. Mimi pamoja na abiria wenzangu tukaanza kutoka nje ya uwanja ule.
Macho yangu yalikuwa yakiangalia katika kila upande, nilijitahidi kutaka kuyazoea mazingira ya jiji lile.
Watu wengi ambao walikuwa wakionekana katika macho yangu walikuwa wamevaa kanzu pamoja na vilemba vichwani, mavazi yale ndio yalionekana kuwa makubwa sana katika nchi ile.
Nilipofika nje ya uwanja ule, moja kwa moja nikamfuata dereva wa teksi na kutaka aniepeleke sehemu yoyote ambayo ingeniwezesha kubadilisha fedha zangu na kuwa paundi, fedha ambayo ilikuwa ikitumiwa nchini humo.
Baada ya kumwambia kitu nilichotaka kukifanya, akaniambia niingie ndani ya gari lake na kisha safari kuanza.
Mji wa Khatoum haukuwa mzuri sana, majengo yao yalikuwa kama ya kizamani sana, kwa jinsi ulivyokuwa ukionekana mji ule, hali ilionyesha dhahiri kwamba sehemu kubwa ya nchi ile ilikuwa ni jangwa.
Mitaa ya jiji lile ilikuwa katika mpangilio mzuri japokuwa haukuwa ukivutia sana. Kwa kila mtu ambaye nilikuwa nikimuona alikuwa akionekana kuwa na kanzu jambo ambalo likanifanya hata mimi pia kutamani kununua kanzu ili nionekane kuwa mmoja wapo.
Safari yetu ile iliishia njie ya duka moja kubwa ambalo nikaingia ndani na kisha kutoa kiasi cha shilingi milioni saba na kisha kunibadilishia katika fedha zao za paundi ya Sudan ambayo walikuwa wakiitumia.
Kutokana na nchi ile kubwa imeanguka sana katika uchumi, fedha zangu nilizozipata zilikuwa nyingi sana.
Kitu cha kwanza nilichokifanya ni kumlipa dereva fedha zake na kisha kumtaka kunipeleka katika hoteli yoyote ambayo haikuwa na gharama kubwa.
Huku tukiwa njiani kuelekea katika hoteli hiyo, nikamwambia kwamba nilikuwa na uhitaji wa kununua kanzu na kiremba na yeye kuniita muuzaji na kununua, sikutaka kuchelewa, nikanunua na kisha kuvivaa pale pale.
“How do I look? (Naonekana vipi?)” Nilimuuliza dereva yule.
“Like a Sudanese (Kama Msudani)” Dereva alinijibu huku akionyesha tabasamu pana.
Si wanajeshi wa Umoja wa Mataifa tu ambao walikuwa wakirandaranda mitaani bali hata wanajeshi wa Umoja wa Afrika (A.U) nao walikuwa wametapakaa katika mitaa ile, kwa picha ambayo ilionekana, sehemu ile haikuonekana kuwa ya usalama hata kidogo.
Baada ya dakika chache dereva akasimamisha gari lile nje ya hoteli moja ndogo iliyoitwa Selima Oasis.
Nikateremka, nikamlipa dereva kiasi ambacho alikuwa ameihitaji na kisha kuelekea katika sehemu ya kaunta na kukutana na msichana mrembo. Nikaanza kumuuliza kuhusu vyumba na kisha kulipia na kupelekwa katika chumba ambacho nilitakiwa kukaa katika siku ambazo ningekuwa hapo Sudan.
Sehemu ambayo nilitamani sana kufika tayari nilikuwa nimekwishafika. Sikujali kama wazazi wangenitafuta na kunikosa, nilichokuwa nikikijali kwa wakati huo ni kutengeneza makala yangu tu. Nilibaki chumbani mule huku nikianza kuifikiria safari yangu ya kuelekea Darfur, magharibi mwa nchi hiyo ya Sudan.
Ingawa ilionekana kuwa sehemu iliyokuwa na hatari lakini wala sikuonekana kujali kabisa, sikuwa na woga wowote moyoni mwangu, nilikuwa nimedhamiria kwa moyo mmoja kwamba ilikuwa ni lazima nifanye kazi ambayo ilikuwa imenleta mahali pale, sikujali kupigwa risasi, kuchomwa moto au kuchinjwa, kile nilichokuwa nikikihitaji kwa wakati huo ni kufanya kazi yangu ambayo niliiona kuwa bora na kuniingizia fedha na kunitambulisha kama mwandishi wa habari wa Kimataifa.
*
Ukiachana na magari hayo ya jeshi, vile vile kulikuwa na magari makubwa ambayo yalikuwa yakitumika kupeleka vyakula katika nchi hiyo.
Sudan ilikuwa na njaa, watu walikuwa bize kuyakimbia makazi yao hasa wale ambao waliishi sehemu za nje ya Jiji la Khatoum.
Mashambani, wakulima hawakufika huko kulima kwa sababu waliogopa. Vyombo vingi vya habari vilikuwa vikitangaza mara kwa mara vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa vikiendelea kutokea nchini humo.
Darfur ndio ilikuwa sehemu iliyokuwa na mapigano makubwa. Japokuwa sikuwa nimefika huko lakini nilijua tu kwamba sehemu hiyo ilikuwa ni ya hatari mno, kama ungeingia unatembea basi kile ambacho kingerudishwa kingekuwa ni mwili wako tu bila pumzi.
Nilikaa na kuiangalia televisheni na habari za mauaji ambazo zilikuwa zikiendelea kutokea Darfur, niliporidhika, nikainuka na kulifuata begi langu. Nikalifungua na kuanza kutoa kitu kimoja baada ya kingine.
Nikaitoa kamera na kuiweka juu ya meza huku nikiwa nimeiseti sawasawa na pale nilipokaa.
Hapo ndipo ambao nikaanza kujirekodi, makala ambayo nilikuwa nimekwenda kuifanya Darfur ikaanzia hapo.
Niliongea maneno mengi kwa Lugha ya Kingereza huku nikiwataka watazamaji wawe makini kuangalia kila kitakachokwenda kuonekana pamoja na kukisikia kile ambacho nilikuwa ninatarajia kukiongea.
Nilipoona inatosha, nikaizima kamera.
Nikatoa vitu vingine zaidi na zaidi, kazi ambayo ilikuwa mbele yangu ilikuwa kubwa tena ya kujitoa mhanga lakini sikujali, nilichokijali ni kuajiriwa katika moja ya makampuni makubwa ya habari tu. Siku hiyo sikutaka kufanya mambo mengi, nikalala.
Tukakubaliana na kumuacha kwenda kujiandaa kwa ajili ya safari hiyo ya kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na mauaji ya kikatili.
Mimi ndiye nilikuwa mwandishi wa habari, na mimi ndiye nilijifanya kuwa mlinzi katika maisha yake bila kujua kwamba Darfur ilikuwa ni sehemu gani, ilikuwa na hatari kwa kiasi gani.
Akakubaliana nami, hakujali sana kuhusu fedha, kitu alichojua ni kwamba nilitoka katika Shirika la Habari la Aljazeera na ndiyo maana alijisikia fahari kukubali kutaka kufanya kazi pamoja nami, hakujua kwamba hata kile kitambulisho ambacho nilimuonyeshea kilikuwa cha bandia.
Alichojua ni kwamba alikuwa akifanya kazi na mwandishi wa habari kutoka Aljazeera kumbe ukweli ni kwamba alikuwa akifanya kazi na Mwananchi wa kawaida tu, yaani kama yeye.
*
Sudan ilikuwa nchi kubwa sana zaidi ya nilifikiria kabla.
Nilipomuuliza dada wa mapokezi katika hoteli ile, alinishangaa sana kwamba ilikuwaje nihitaji kuelekea Darfur na wakati mapigano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe yalikuwa yakiendelea huko?
Nilimtoa wasiwasi na kutaka kunipa maelekezo mengi kuhusu safari ya kwenda katika mji huo iana na kwenda katika mji huo ambao ulionekana kuwa tishio sana.
Dada yule akaanza kunielezea mambo mengi na hata umbali aliniambia kwamba kulikuwa na zaidi ya kilometa elfu nane kutoka katika jiji la Khatoum.
Umbali ule ukanishtua sana, sikutegemea kama kungekuwa na umbali wa namna ile. Hapo nilifikiria kupanda ndege, ila tatizo lililokuja ni kwamba hakukuwa na uwanja wowote wa ndege huko Darfur uliokuwa ukitumika katika kipindi hicho cha mapigano.
Maneno ya dada yule yalinichosha kupita kawaida, ni mabasi tu ndio ambayo yalikuwa yakifanya safari ya kwenda huko kwa kutumia barabara ya lami ambayo ilikuwa ikiunganisha mpaka Kurdufan, kilometa mia tano kabla ya kuingia Darfur.
Niliporidhika na maelezo yake, nikarudi chumbani na kujiandaa na safari, asubuhi ya siku iliyofuata, safari ikaanza huku nikiwa pamoja na Majeed.
Ndani ya basi hatukuwa watu wengi, tulikuwa tumekaa katika viti vya nyuma kabisa.
Lugha ya Kiarabu ndio ambayo ilikuwa ikisikika ndani ya basi lile, sikuwa nikielewa kitu chochote kile lakini kila nilipotaka kuambiwa kile kilichokuwa kikiongelewa, Majeed alikuwa akiniambia.
Safari ilikuwa ni ya kuchosha sana, mizigo mingi ilikuwa imepakiwa ndani ya basi lile, kila basi lilipokuwa likisimama, hali ya hewa ilikuwa ikibadilika kabisa, ilikuwa ni ya joto kali sana.
Kichwa changu katika kipindi hicho kilikuwa kikifikiria kitu kimoja tu, kufika Darfur na kuanza kufanya kile ambacho kilikuwa kimenifanya kufika ndani ya nchi ile.
Dereva alikuwa akiendesha gari kwa kasi. Ndani ya gari hakukuwa na mtu yeyote aliyejali mwendo ule mkali, ni kama watu walionekana kutokuwa na habari, walikuwa wakiendelea kupiga stori kama kawaida. Ndani ya saa nane, tukawa tumefika Ad Duwaym, Kusini mwa Jiji la Khatoum.
Hapa kidogo ilikuwa ikinishangaza sana, Mji wa Darfur ulikuwa ukipatikana Magharibi mwa nchi ya Sudan, sasa ilikuwaje katika kipindi hicho tulikuwa tukielekea Kusini. Maswali hayo wala sikutaka kuyauliza, nilibaki nayo moyoni huku nikisubiri muda muafaka wa kuuliza utakapofika.
Kama ilivyokuwa Khatoum ndivyo ilivyokuwa hapo Ad Duwaym, kulikuwa na idadi kubwa ya watu huku magari mengi ya Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika yakiwa mahali hapo.
Hapo tukaruhusiwa kushuka na kuanza kununua vyakula. Hali ilikuwa ngumu sana kwangu, vyakula ambavyo vilipatikana hapo havikuwa sawa na mimi.
[22:31, 3/19/2019] +255 717 339 102: SEHEMU YA 16
Chakula ambacho nilihisi ningeweza kukila kilikuwa ni nyama ya ngamia tu, nyama tamu ambayo mara nyingi nilikuwa nikiila nchini Tanzania hasa katika kipindi cha Idd Al Hadji na El Fitri ambapo rafiki yangu, Ustadhi Maliki alipokuwa akituletea.
Baada ya nusu saa tukaingia ndani ya basi na kuendelea na safari yetu. Hakukuwa na safari ambayo ilikuwa inachosha kama ile.
Muda mwingi nilikuwa nikiiangalia saa yangu ya mkononi ambayo nilikuwa nimeiseti katika majira ya Sudan.
Safari iliendelea zaidi, sehemu kubwa ya nchi hiyo ilikuwa ni jangwa kubwa, tena jangwa lile ambalo lilikuwa na joto kali katika kipindi cha mchana.
Baada ya saa nane nyingine kupita, tukaingia katika Mji wa Kust na kuunganisha kuutafuta Mji wa Rabak ambapo hapo tungechukua barabara ya kuelekea Darfur.
Mchoko wa safari bado ulikuwa mkubwa mno, saa nne na robo usiku tukaingia Rabak ambapo hapo tulitakiwa kulala.
Usingizi haukupatikana hata kidogo, tulishinda usiku mzima tukipiga stori na Majeed ambaye hakuonekana kuwa na amani katika safari ile.
Bado niliendelea kumfariji na kumtoa hofu. Tulikula na kuendelea kupiga stori. Ilipofika saa kumi na mbili alfajiri, tukaanza tena safari ya kuelekea Darfur.
Hapo Rabak tuliwachukua abiria wengine waliokuwa wamefika na mabasi kutoka Sannar, Sanjar na Al Qadarif miji ambayo ilikuwa ikipatikana Mashariki mwa nchi ya Sudan.
Majeed ndiye ambaye alionekana kunichosha zaidi hasa mara baada ya kunitaarifu kwamba hata nusu ya safari tulikuwa hatujamaliza, tulisafiri kwa saa kumi na sita lakini cha ajabu eti hata nusu ya safari haikuwa imekwisha.
Safari ikaendelea zaidi, tayari nilionekana kukata tamaa ya kufika mapema, jua lilipochomoza mpaka kuwa la utosini ndipo tukafika Al Ubayyid. Hapo tukanunua chakula na kula tena.
Hali ya joto ilinisumbua, nilitamani kuvua shati langu lakini sikufanya hivyo kwa kutotaka kuonekana vibaya mbele za macho ya watu waliokuwa na asili ya Uarabu.
Safari ikaendelea zaidi, saa tano na robo usiku ndipo tukaingia An Nunud, kilometa mia saba kabla ya kuingia Darfur. Nikatoka garini na kukaa nje.
Kila abiria alichoka, nilibaki nikiongea na Majeed kwa kipindi kirefu zaidi huku nikitaka kufahamu mengi kuhusiana na Darfur.
“Kwa hiyo nitajua vipi kama tumeingia Darfur?” nilimuuliza Majeed.
“Utajua tu.”
“Nitajua tu. Kivipi?” nilimuuliza.
“Swali lako litajibika kirahisi sana,” Majeed aliniambia.
“Sijakuelewa.”
“Kimuonekano. Utakavyouona muonekano, utajua tu kwamba tutakuwa tumeanza kuingia Darfur,” Majeed aliniambia.
Sikutaka kuuliza maswali mengine zaidi, kiu yangu ilikuwa ni kuanza kuona dalili hizo ambazo niliambiwa kwamba ningejua tu kwamba tulikuwa tumeingia Darfur.
Ilipofika asubuhi tukaanza safari. Katika kipindi hiki kulikuwa kumebaki vituo viwili vikubwa, cha kwanza kilikuwa Nyala na cha pili kilikuwa Al Fashir.
Hiki kituo cha Al Fashir kilikuwa ndani ya Darfur ila huku pembeni pembeni kabisa katika upande wa Kusini mwa Mji wa Darfur.
Hapo ndipo ungekuwa mwisho wa safari yetu, japokuwa katika kipindi hicho nilitaka kuelekea katika sehemu iliyo na mapigano zaidi ya Al Junaynah, lakini Majeed aliniambia kwamba basi lisingeweza kufika huko.
“Kwa nini?” nilimuuliza.
“Huko ndipo kwenye mapigano yenyewe, huko hakuna amani hata kidogo,” Majeed aliniambia.
“Safi sana. Uko ndipo pazuri, na huko ndipo nilipotaka kwenda,” nilimwambia Majeed ambaye alionekana kushtuka zaidi.
Safari iliendelea, abiria wengi waliishia hapo Al Ubayyid. Kipindi cha nyuma ndani ya basi tulikuwa zaidi ya watu sitini lakini katika kipindi hicho tulikuwa tumebakia watu kumi na sita tu, wengine walikuwa wamekwishashuka.
Safari haikuishia hapo iliendelea zaidi na zaidi mpaka tukaingia Nyala, kituo cha mwisho kabla ya kuingia kituo cha Al Fashir, mwisho wa safari ya basi lile.
Safari ya kuelekea Al Fashir ikaanza. Hapa ningependa kuongea kitu kimoja kwa wale ambao waliweza kuongea mengi hata kabla safari ya kufika Darfur haikukamilika.
Darfur ndiyo mji mkubwa nchini Sudan na ndiyo maana mapigano yaliyokuwa yakiendelea huko yaliweza kuiathiri sana nchi hiyo.
Safari ya kuelekea katika mji mdogo wa Al Fashir ilikuwa ikiendelea. Hapa pia ningependa kuongea kitu kimoja ili kwa wale walioshangaa wasishangae tena.
Umbali wa kutoka Khatoum mpaka Darfur ilikuwa ni wa kilometa 8000 ila kilometa hizo ni mpaka pale ambapo unaingia katika Mji wa Nyala ambao upo Kusini mwa mji huo wa Darfur.
Umbali kutoka Khatoum mpaka hapo Nyala haukuwa ukipishana sana na umbali kutoka Nyala mpaka mwisho wa basi lile, Al Fashir.
Darfur ile ilikuwa kubwa sana, upana wake ulimshangaza kila mtu kiasi kwamba kuna wakati nchi ya Chad ikang’ang’ania kwamba Darfur ilikuwa ni sehemu ya nchi yao.
Darfur ilikuwa kubwa, eneo kubwa la Darfur lilikuwa jangwa kubwa, jangwa ambalo lilikuwa na joto kali katika kipindi cha mchana.
Umbali huo mkubwa ndio ukanifanya kupata majibu ya sababu ambayo ilimfanya dereva kuendesha gari kwa kasi kubwa zaidi ya magari ambayo yalikuwa yakisafiri katika ardhi ya Tanzania.
Nakumbuka nilikwishawahi kwenda Nairobi kwa kutumia mabasi ambayo yalikuwa yakikimbia sana, ila kwa mabasi yale ambayo yalikuwa yakisafiri kuelekea Darfur, mwendo wake ulikuwa ni mara mbili ya mabasi ya huku Tanzania.
Dereva alikanyaga mafuta hasa, muda mwingi nilikuwa na hofu lakini hakukuwa na mtu aliyehofu chochote kile, walionekana kuzoea.
Hapo ndipo ambapo safari ilionekana kuchosha sana, tulisafiri usiku na mchana na hatimaye kuingia Al Fashir, mji ambao basi lile lilikuwa limefikia mwisho.
Nikateremka na kumshukuru Mungu kwa kunifikisha salama katika ardhi ya Mji wa Al Fashir. Nilichokifanya ni kwenda kwenye kimgahawa kidogo na kupata chakula,
Kumbuka kwamba hapo tayari tuliingia katika mji wa Darfur ila hatukuwa tumefika katika sehemu ile ambayo ilikuwa na mapigano makubwa.
Baada ya kukaa mahali hapo kwa muda wa masaa mawili, ndipo tukaanza safari ya kuelekea sehemu iliyo na mapigano makali, Al Junaynah.
Usafiri haukuwa wa basi tena, madereva wengi walikuwa wakiogopa kuelekea huko kwa hiyo tulichokifanya ni kutumia usafiri wa farasi ambao ndiyo ulikuwa usafiri uliokuwa ukitumika katika kipindi hicho sehemu hiyo.
Katika safari ya kuelekea Al Junaynah hatukuwa peke yetu, tulikuwa na watu zaidi ya kumi ambao nao walikuwa wakielekea huko.
Farasi walikuwa wakikimbia kwa kasi kubwa, na kwa kutumia farasi hao huku tukipumzika katika sehemu mbalimbali hasa nyakati za usiku na pale ambapo farasi walipochoka, tuliweza kutumia siku sita na ndipo tukaanza kuingia katika Mji wa Al Junaynah.
Mpaka hapo wala sikutaka kuuliza zaidi kama tulikuwa tumeingia katika mji huo au la, magari mengi ya Umoja wa Mataifa yalionekana machoni mwetu, mara kwa mara walikuwa wakitusimamisha na kutuuliza baadhi ya maswali na waliporidhika na majibu yetu, tulikuwa tukiendelea na safari kama kawaida.
Tukafika katika sehemu ambayo wala haikuwa ikieleweka kabisa, macho yangu yakatua katika vitu vyeupe ambavyo nikashikwa na shauku kubwa ya kutaka kuvijua ni vitu gani.
Nilichokifanya ni kuanza kuwaambia wenzangu kwamba ilikuwa ni lazima nijue vitu vile vilikuwa ni nini. Watu wote walikataa lakini nilipowalazimisha zaidi, wakakubaliana nami.
Nikateremka juu ya farasi pamoja na Majeed na kuanza kuelekea kule ambapo kulikuwa na mchanga mwingi. Sikuamini kile ambacho nilikuwa nikikiona mahali pale, yalikuwa ni mafuvu ya watu.
Kwanza nikapigwa na mshtuko sana, toka nizaliwe sikuwahi kuyaona mafuvu ya watu, wakati huo ndio ilikuwa mara ya kwanza.
Kuna vitu vingine huwa tunavipuuzia sana kila tunavyoviona kwenye televisheni, ila ukweli ni kwamba vinatisha kupita kawaida. Mafuvu ya watu yanatisha sana.
Nilichokifanya huku nikijivisha ujasiri, nikamwambia Majeed achukue kamera na kuanza kazi mahali hapo. Nikaanza kuongea huku Majeed akinirekodi, kwa kuniangalia harakahara, sikuonekana kuongea nikiwa na amani, lakini ukweli nilikuwa na hofu sana.
Kitendo changu cha kuyainamia mafuvu yale nilikiona kuwa cha ujasiri sana. Mafuvu ambayo yalikuwepo mahali pale yalikuwa ni mafuvu ya tofauti tofauti.
Kulikuwa na mafuvu ya watoto wadogo na pia kulikuwa na mafuvu ya watu wakubwa. Eneo hilo lilionekana kutokuwa na amani katika kipindi cha nyuma, kuna watu ambao waliteketezwa kwa kupigwa risasi mahali hapo.
Mafuvu yalikuwa mengi mahali hapo, kwa idadi ya haraka haraka ya kuhesabu huku nikiwa na hofu, yalikuwa yakifikia hata mia tatu. Watu wengine ambao tulikuwa tukisafiri pamoja katika farasi wale walibaki wakiniangalia katika kipindi hicho ambacho nilikuwa nikitengeneza makala yangu.
Tulikaa mahali pale kwa takribani dakika arobaini na tano na ndipo tukaendelea na safari yetu. Moyoni nilikuwa na majonzi makubwa, hofu ilizidi kuongezeka na kujua huko tulipokuwa tukienda ilikuwa ni hatari.
Nikaanza kujiuliza maswali mengi kwamba kama pale mwanzo wa kuingia Al Junaynah kulikuwa na mafuvu mengi kiasi kile, vipi huko katikati ya mji huo ambao mapigano yalikuwa makubwa zaidi? Kila nilichokuwa nikijiuliza nilikosa jibu kabisa.
Kamera yangu ya picha za kawaida ilikuwa imetumika kwa kupiga picha zaidi ya kumi huku zikiwa zimebakia picha sitini hata kabla ya mkanda kuisha.
Kwa wakati huo, kichwa changu kilikuwa na mawazo mengi sana, nilikuwa nikijifikiria juu ya mambo ambayo ningeweza kukutana nayo katikati ya mji wa Darfur.
Kumbukumbu za mafuvu yale ambayo ulikutana nayo ziliniogopesha kupita kawaida, amani ikaanza kupotea moyoni mwangu huku ujasiri ambao nilikuwa nao ukianza kuyeyuka.
Tuliendelea kwenda na wale farasi, sehemu ambayo tulikuwa tukipita ilikuwa jangwa moja kubwa, hakukuwa na nyumba nyingi sana.
Hapa labda ningependa kuzungumza kitu kimoja.
Kwa sababu asilimia tisini ya nchi ya Sudan ilikuwa ni jangwa basi lilikuwa ni jambo la kawaida sana kukutana na wakinamama njiani wakiwa wamebeba mitungi ya maji huku wakitembea kwa mwendo mrefu kutokana na maji kuwa ya shida sana katika nchi nyingi zilizokuwa na majangwa.
Tukafika sehemu moja ambayo kulikuwa na miti zaidi ya ishirini ikiwa imesimamishwa kwa kuchomekwa mchangani.
Nilibaki nimeduwaa huku nikiwa nimeikodolea macho miti ile.
Sikutaka kuendelea na safari, nilichokifanya ni kuwaambia watu ambao nilikuwa nao kwamba nilitaka kuona ni kitu gani ambacho kilitokea mahali pale mpaka miti ile kuchomekwa mchangani.
Kama kawaida yao, wote wakawa wabishi, hawakutaka kukubaliana nami kwamba twende kule na kuiona miti ile. Nilipoona wanakataa, nikawakumbusha kwamba mimi ni mwandishi wa habari niliyekuwa na wajibu wa kufahamu vitu vingi kuhusu.
Kuwa mwandishi wa habari katika nchi kama ya Sudan kulikuwa na uzuri wake, watu walikuwa wakikusikiliza sana, hii ilitokana ni kwa sababu waliamini kama wewe mwandishi ungekuwa unaelezea mambo mengi yaliyotokea katika nchi hiyo basi ingekuwa rahisi kwenda kwenye vyombo vya habari na kutangaza na hatimaye kupata msaada kutoka katika nchi za Magharibi.
Mtunzi Nyemo Chilongani
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 01
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2005, mwaka ambao nilimaliza kuchukua Diploma yangu ya Uandishi wa habari katika Chuo cha Uandishi cha DSJ (Dar es Salaam School of Journalism) kilichokuwa Mtaa wa Bungoni, Buguruni jijini Dar es Salaam.Katika kipindi hicho nilikuwa na furaha sana kwa sababu ndoto zangu ambazo nilijiwekea katika maisha yangu niliziona kuanza kutimia katika muda mchache ujao.
Katika kipindi chote ambacho nilikuwa katika chuo hicho nikipata elimu yangu, kichwani mwangu kulikuwa na ndoto nyingi, ndoto za kuwa mwandishi mkubwa ambaye ningekuja kuheshimika na jamii yote, mwandishi ambaye ningeweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta zote za uandishi nchini Tanzania.
Kila nilipokuwa nikimwangalia mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Charles Hilary, nikajiona nikizidi kupata nguvu zaidi za kusoma kwa sana, nilitamani sana kuwa kama yeye katika maisha yangu.
Nilikuwa na kiu sana ya kuwa mwandishi bora na kisha kutafuta nafasi ya kutangaza katika shirika lolote kubwa la Habari kama la BBC, CNN, Al Jazeera au shirika lolote ambalo lilikuwa likitambulika kimataifa.
Hapo ndipo ambapo nilipofikiria kitu kimoja ambacho nilitakiwa kufanya, kitu ambacho kingekuwa cha hatari sana katika maisha yangu.
Nakumbuka siku hiyo mara baada ya kutoka katika ‘field’ yangu niliyoifanyia katika kituo cha utangazaji cha Global TV, nikarudi nyumbani na kutulia chumbani kwangu.
Siku hiyo sikuonekana kuwa na furaha kabisa, kichwa changu kilikuwa kikifikiria ni kwa namna gani ningeweza kuwaambia wazazi wangu kuhusu kile nilichokuwa nikikifikiria kichwani mwangu.
Kiukweli nilihitaji sana ushirikiano kutoka kwa wazazi wangu, wao ndiyo walikuwa watu sahihi ambao kamwe wasingeweza kunishauri kitu kibaya.
Nilitulia chumbani kwangu kitandani, hakukuwa na siku ambayo niliwaona wazazi wangu wakichelewa kurudi nyumbani kama siku hiyo.
Muda wote macho yangu yalikuwa yakiangalia saa yangu ya mkononi, nilitamani sana waingie nyumbani hapo na kuwaambia kile nichokuwa nimepanga kuwaambia.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 02
Saa 2:23 usiku nikasikia muungurumo wa gari kutoka nje ya nyumba yetu, sikutaka kujiuliza zaidi, nikajua fika kwamba wazazi wangu walikuwa wakiingia ndani ya eneo la nyumba yetu.
Sikutaka kutoka wala kuonyesha kwamba nina presha, nikatulia chumbani mpaka pale walipoingia ndani na kuelekea chumbani kwao.
Baadaye walipotoka kwa ajili ya kula chakula cha usiku, nikaelekea mezani na kuanza kula pamoja nao.
Kwa wakati huo kichwa changu kilikuwa kikifikiria mengi, sikujua kama wangeweza kunielewa juu ya kile nilichotaka kuwaambia. Katika kipindi chote ambacho tulikuwa tukila, muonekano wangu ulionekana kuwa si wa kawaida, nilionekana kuwa na kitu moyoni mwangu.
“Thomas!” niliisikia sauti ya baba ikiniita, nikashtuka kutoka katika lindi la mawazo.
“Naam!” niliitikia huku nikionekana kushtuka.
“Unawaza nini?” aliniuliza baba huku akiacha kula.
“Siwazi kitu baba,” nilimwambia huku macho yangu yakionyesha dhahiri kwamba nilimdanganya.
“Hapana. Hauko kawaida leo. Hebu tueleze unawaza nini,” aliniambia.
Nilibaki kimya kwa muda, nikaanza kufikiria ni kitu gani nilichotakiwa kuwaambia. Nikaanza kujiuliza kama lilikuwa jambo sahihi kuwaambia kile nilichopanga kuwaambia ili wanishauri au nilitakiwa kukaa kimya na kuwashtukiza hapo baadaye.
“Kuna nini kipenzi,” mama aliingilia kwa kuniuliza swali. Nikayapeleka macho yangu usoni mwake.
“Nataka kuwa mwandishi mkubwa wa habari,” niliwaambia.
“Hilo tunalifahamu na umekuwa ukituambia kila siku. Nakumbuka huwa unatuambia kwamba unataka kuwa kama Charles Hilary, si ndiyo?” aliniambia baba na kuniuliza.
“Ndiyo. Natamani sana nifanye kazi katika mashirika makubwa ya habari duniani,” niliwaambia.
“Kila kitu kinaanza kwa hatua Thomas, huwezi kuwa mwandishi mkubwa wa habari na wakati haujapitia katika mashirika madogo.
Unakumbuka kuwa hata Charles Hilary kabla ya kujiunga na BBC alikuwa akifanya kazi ITV?” baba alisema na kuniuliza.
“Nakumbuka.”
“Basi hutakiwi kuwa na presha. Kuna siku utakuwa mwandishi mkubwa tu,” aliniambia.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 03
Nikabaki kimya kwa muda, baba aliniondoa katika kile nilichokuwa nimekifikiria kabla, alijitahidi kuniambia maneno mengi kwamba ningekuwa mwandishi mkubwa wa habari kama tu ningekuwa mvumilivu na kufanya kazi katika mashirika madogo, sikukubaliana na maneno yake kabisa.“Kuna kitu nimekifikiria na ningehitaji ushauri wenu,” niliwaambia.
“Kitu gani?”
“Nataka nitengeneze makala yangu ihusuyo mambo fulani, na kama ikiwezekana basi nisafiri,” niliwaambia.
“Kuandaa makala yahitaji utulivu mkubwa sana.
Wewe unataka kusafiri kuelekea wapi kuiandika hiyo makala yako?” baba aliniuliza.
“Nataka kwenda Darfur, nchini Sudan,” niliwaambia.
Kila mmoja akashtuka, wote wakaacha kula na kuniangalia kwa macho yaliyoonyesha kutokuamini kile nilichokisema.
Wakanikazia macho zaidi, nilionekana kuongea kitu kilichowashtua mno. Nikamuona baba akiisogeza sahani yake mbele kuonyesha kwamba alikuwa ameshiba.
“Unasemaje?” aliniuliza huku akionekana kushtuka.
“Nataka kwenda Darfur,” nilimjibu.
Chakula hakikulika tena, kila mmoja alionekana kushiba, maneno niliyowaambia kwamba nilitaka kwenda nchini Sudan tena katika Mji wa Darfur yaliwashtua sana. Waliufahamu vilivyo mji huo na yale mauaji yaliyokuwa yakiendelea huko.
Hapa ningependa kuwaambia wale watu ambao hawakuwa wakiijua hii Darfur ambayo nilikuwa nimeizungumzia mahali hapo. Darfur ni mji mkubwa ambao unapatikana nchini Sudan. Mji huu ndiyo umekuwa na machafuko mengi ambayo yamepelekea nchi nzima kutokuwa na maelewano.
Watu walikuwa wakiishi kwa hofu huko, wakulima walihofia kuelekea mashambani mwao jambo ambalo lilipelekea nchi kuingia katika njaa kali.
Nchi hii ilionekana kama kuwa na laana kwani toka kipindi ambacho machafuko hayo yalianza, mvua nazo zilianza kunyesha kwa nadra sana.
Waandishi wa habari waliokuwa wakielekea katika mji huo wengi kuuawa kinyama kwa sababu wao wenyewe hawakutaka kufuatiliwa na maisha yao au kitu chochote kilichokuwa kikiendelea huko.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 05
Nilibaki pale mezani kwa muda, mara nikaichukua simu yangu na kisha kumpigia simu mpenzi wangu niliyekuwa nae katika kipindi kile, Myra na kisha kumwambia kile ambacho nilikuwa nimekifikiria kukifanya kwa wakati ule.
Nilipompa taarifa Myra, nae alikuwa sawa na wazazi wangu, alikataa kata kata kunikubalia nielekee nchini Sudan.
“Hapana mpenzi” Myra aliniambia kwa sauti iliyojaa wasiwasi.
“Itanibidi nifanye hivyo Mage. Ni lazima niende Sudan. Haijalishi wewe hautaki au wazazi wangu hawataki, NI LAZIMA nilekee Sudan” Nilimwambia Myra.
Huo ndio uamuzi ambao nilikuwa nimeupanga.
Nikaanza kufikiria gharama ambazo zingenigharimu mpaka kukamilisha kila kitu, kitu cha kwanza kilikuwa kamera, nilihitaji kuwa na kamera ya video na ya picha. Pia nikahitaji kuwa na begi kubwa la mgongoni pamoja na kiasi fulani cha fedha ambacho kingeniwezesha kukitumia katika kipindi ambacho ningekwenda nchini Sudan.
Vitu hivyo havikuwa na shida sana, pia nilitakiwa kuwa na kitambulisho cha uandishi wa habari ambacho ningekionyesha kwa kila mtu ambaye angetaka kukiona hasa wale wafuasi wa upande wa pili ambao walikuwa kinyume na serikali ya Sudan.
Hapa ndipo nilipoamua kuwasiliana na rafiki yangu, Hamza Kimosa ambaye nilimwambia anitengenezee kitabulisho cha uandishi wa habari cha shirika la Aljazeera huku nikiwa nimemtumia picha ya itambulisho hicho ambayo niliipata kwenye mtandao.
“Ni LAZIMA niende Darfur hata kama hawataki. Hata kuwatoroka nitawatoroka tu” Nilijisemea katika kipindi ambacho nilikuwa nikielekea chumbani kwangu.
*
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 06
Nilijisikia vibaya sana hasa mara baada ya wazazi wangu kunikatalia kile ambacho nilitaka kukifanya kwa wakati huo.Nilichukia sana na wala sikutaka kuongea nao, niliwaona kuwa kama wasaliti katika maisha yangu ambao hawakutaka kuniruhusu kufanya kitu ambacho kingenifanya kufaidika katika maisha yangu.
Siku iliyofuata nikaanza kuondoka kuelekea nyumbani alipokuwa akiishi Hamza, rafiki yangu ambaye alikuwa mtaalamu na mambo ya Graphic.
Nilimkuta Hamza na hivyo kumtaka anionyeshee kitambulisho cha mwandishi wa habari wa shirika la habari la Aljazeera na kisha kunionyeshea.
Kitambulisho kile kilionekana kutengenezwa katika utaalamu wa hali ya juu, japokuwa kilikuwa kikionekana kwenye kompyuta lakini kilionekana kuvutia sana.
“Kwa hiyo jina niweke Thomas Chilongani kama kawaida au?” Hamza aliniuliza.
“Nope. Weka Iqram Ibrahim” Nilimwambia.
Pale pale Hamza akabadilisha na kisha kuliweka jina lile.
Kichwani mwangu nilikwishajua kwamba katika kipindi kile nilikuwa nikielekea katika nchi ambayo ilikuwa na waumini wengi wa dini ya Kiislamu, hivyo nilihakikisha kwamba nafanya kila jitihada ili nionekane kuwa mtu wao ili hata kama nitahitaji vitu fulani kutoka kwao basi niweze kuvipata kwa urahisi.
Siku hiyo nilikamilisha kila kitu kilichokuwa kikihitajika na kisha kuondoka kuelekea nyumbani.
Nilichokifanya kwa wakati huo ni kuelekea katika mashine ya ATM na kisha kuchukua kiasi cha fedha cha shilingi milioni mbili na kuanza kuelekea Posta kwa ajili ya manunuzi ya kamera.
Nikapata kamera mbili ambazo zilionekana kuwa bora na kuanza kurudi nyumbani.
Kwa wakati huo, nilitaka kufanya mambo yangu kwa siri sana, sikutaka mtu yeyote nyumbani afahamu kwani kwa kuwafanya wafahamu basi wangeweza kunizuia kwenda kwa kutumia maneno yao ya kunikatisha tamaa na kunitisha.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 08
Ingawa nchi ambayo nilikuwa ikielekea katika kipindi hicho ilionekana kuwa nchi ya hatari, lakini moyoni mwangu wala sikuonekana kuwa na wasiwasi wowote ule, nilikuwa nikizidi kujipa matumaini kwamba kila kitu kingekwenda kama ambavyo kilitakiwa kiwe.
Nilipanga kuandaa makala moja kubwa na ya maana sana katika kila chombo cha habari ambacho kingediriki kuonyesha makala hiyo ambayo ilikuwa imeandaliwa na kijana mbunifu ambaye alikuwa na uwezo wa kuelezea mambo mengi kwa undani zaidi, Thomas Chilongani.
Saa 11:15 jioni, ndege ikaanza kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum uliokuwa katika jiji la Khartoum.
Hali ya hewa haikuwa nzuri sana, joto liionekana kuwa juu kwa kiasi fulani. Mimi pamoja na abiria wenzangu tukaanza kutoka nje ya uwanja ule.
Macho yangu yalikuwa yakiangalia katika kila upande, nilijitahidi kutaka kuyazoea mazingira ya jiji lile.
Watu wengi ambao walikuwa wakionekana katika macho yangu walikuwa wamevaa kanzu pamoja na vilemba vichwani, mavazi yale ndio yalionekana kuwa makubwa sana katika nchi ile.
Nilipofika nje ya uwanja ule, moja kwa moja nikamfuata dereva wa teksi na kutaka aniepeleke sehemu yoyote ambayo ingeniwezesha kubadilisha fedha zangu na kuwa paundi, fedha ambayo ilikuwa ikitumiwa nchini humo.
Baada ya kumwambia kitu nilichotaka kukifanya, akaniambia niingie ndani ya gari lake na kisha safari kuanza.
Mji wa Khatoum haukuwa mzuri sana, majengo yao yalikuwa kama ya kizamani sana, kwa jinsi ulivyokuwa ukionekana mji ule, hali ilionyesha dhahiri kwamba sehemu kubwa ya nchi ile ilikuwa ni jangwa.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 09
Mitaa ya jiji lile ilikuwa katika mpangilio mzuri japokuwa haukuwa ukivutia sana. Kwa kila mtu ambaye nilikuwa nikimuona alikuwa akionekana kuwa na kanzu jambo ambalo likanifanya hata mimi pia kutamani kununua kanzu ili nionekane kuwa mmoja wapo.
Safari yetu ile iliishia njie ya duka moja kubwa ambalo nikaingia ndani na kisha kutoa kiasi cha shilingi milioni saba na kisha kunibadilishia katika fedha zao za paundi ya Sudan ambayo walikuwa wakiitumia.
Kutokana na nchi ile kubwa imeanguka sana katika uchumi, fedha zangu nilizozipata zilikuwa nyingi sana.
Kitu cha kwanza nilichokifanya ni kumlipa dereva fedha zake na kisha kumtaka kunipeleka katika hoteli yoyote ambayo haikuwa na gharama kubwa.
Huku tukiwa njiani kuelekea katika hoteli hiyo, nikamwambia kwamba nilikuwa na uhitaji wa kununua kanzu na kiremba na yeye kuniita muuzaji na kununua, sikutaka kuchelewa, nikanunua na kisha kuvivaa pale pale.
“How do I look? (Naonekana vipi?)” Nilimuuliza dereva yule.
“Like a Sudanese (Kama Msudani)” Dereva alinijibu huku akionyesha tabasamu pana.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 10
Kutokana na nchi ile kuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yalikuwa yakiendelea, wanajeshi wa majeshi ya Umoja wa Mataifa walikuwa wametapakaa katika kila kona huku wakiwa kwenye magari yao ambayo yalionekana kutengenezwa kwa ajili ya vita tu.Si wanajeshi wa Umoja wa Mataifa tu ambao walikuwa wakirandaranda mitaani bali hata wanajeshi wa Umoja wa Afrika (A.U) nao walikuwa wametapakaa katika mitaa ile, kwa picha ambayo ilionekana, sehemu ile haikuonekana kuwa ya usalama hata kidogo.
Baada ya dakika chache dereva akasimamisha gari lile nje ya hoteli moja ndogo iliyoitwa Selima Oasis.
Nikateremka, nikamlipa dereva kiasi ambacho alikuwa ameihitaji na kisha kuelekea katika sehemu ya kaunta na kukutana na msichana mrembo. Nikaanza kumuuliza kuhusu vyumba na kisha kulipia na kupelekwa katika chumba ambacho nilitakiwa kukaa katika siku ambazo ningekuwa hapo Sudan.
Sehemu ambayo nilitamani sana kufika tayari nilikuwa nimekwishafika. Sikujali kama wazazi wangenitafuta na kunikosa, nilichokuwa nikikijali kwa wakati huo ni kutengeneza makala yangu tu. Nilibaki chumbani mule huku nikianza kuifikiria safari yangu ya kuelekea Darfur, magharibi mwa nchi hiyo ya Sudan.
Ingawa ilionekana kuwa sehemu iliyokuwa na hatari lakini wala sikuonekana kujali kabisa, sikuwa na woga wowote moyoni mwangu, nilikuwa nimedhamiria kwa moyo mmoja kwamba ilikuwa ni lazima nifanye kazi ambayo ilikuwa imenleta mahali pale, sikujali kupigwa risasi, kuchomwa moto au kuchinjwa, kile nilichokuwa nikikihitaji kwa wakati huo ni kufanya kazi yangu ambayo niliiona kuwa bora na kuniingizia fedha na kunitambulisha kama mwandishi wa habari wa Kimataifa.
*
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 11
Kwa muonekano wa harakaharaka, Sudan haikuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa na amani kama Tanzania, katika kila kona, magari ya kijeshi ya Umoja wa Mataifa pamoja na yale ya Umoja wa Afrika yalikuwa yakionekana.Ukiachana na magari hayo ya jeshi, vile vile kulikuwa na magari makubwa ambayo yalikuwa yakitumika kupeleka vyakula katika nchi hiyo.
Sudan ilikuwa na njaa, watu walikuwa bize kuyakimbia makazi yao hasa wale ambao waliishi sehemu za nje ya Jiji la Khatoum.
Mashambani, wakulima hawakufika huko kulima kwa sababu waliogopa. Vyombo vingi vya habari vilikuwa vikitangaza mara kwa mara vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyokuwa vikiendelea kutokea nchini humo.
Darfur ndio ilikuwa sehemu iliyokuwa na mapigano makubwa. Japokuwa sikuwa nimefika huko lakini nilijua tu kwamba sehemu hiyo ilikuwa ni ya hatari mno, kama ungeingia unatembea basi kile ambacho kingerudishwa kingekuwa ni mwili wako tu bila pumzi.
Nilikaa na kuiangalia televisheni na habari za mauaji ambazo zilikuwa zikiendelea kutokea Darfur, niliporidhika, nikainuka na kulifuata begi langu. Nikalifungua na kuanza kutoa kitu kimoja baada ya kingine.
Nikaitoa kamera na kuiweka juu ya meza huku nikiwa nimeiseti sawasawa na pale nilipokaa.
Hapo ndipo ambao nikaanza kujirekodi, makala ambayo nilikuwa nimekwenda kuifanya Darfur ikaanzia hapo.
Niliongea maneno mengi kwa Lugha ya Kingereza huku nikiwataka watazamaji wawe makini kuangalia kila kitakachokwenda kuonekana pamoja na kukisikia kile ambacho nilikuwa ninatarajia kukiongea.
Nilipoona inatosha, nikaizima kamera.
Nikatoa vitu vingine zaidi na zaidi, kazi ambayo ilikuwa mbele yangu ilikuwa kubwa tena ya kujitoa mhanga lakini sikujali, nilichokijali ni kuajiriwa katika moja ya makampuni makubwa ya habari tu. Siku hiyo sikutaka kufanya mambo mengi, nikalala.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 14
Ni ndani ya dakika thelathini tu, tena nikiwa nimeongea maneno mengi ya ushawishi, Majeed akakubali kwenda pamoja nami Darfur huku nikiwa nimemhakikishia ulinzi mkubwa katika kipindi ambacho tungekuwa huko.Tukakubaliana na kumuacha kwenda kujiandaa kwa ajili ya safari hiyo ya kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na mauaji ya kikatili.
Mimi ndiye nilikuwa mwandishi wa habari, na mimi ndiye nilijifanya kuwa mlinzi katika maisha yake bila kujua kwamba Darfur ilikuwa ni sehemu gani, ilikuwa na hatari kwa kiasi gani.
Akakubaliana nami, hakujali sana kuhusu fedha, kitu alichojua ni kwamba nilitoka katika Shirika la Habari la Aljazeera na ndiyo maana alijisikia fahari kukubali kutaka kufanya kazi pamoja nami, hakujua kwamba hata kile kitambulisho ambacho nilimuonyeshea kilikuwa cha bandia.
Alichojua ni kwamba alikuwa akifanya kazi na mwandishi wa habari kutoka Aljazeera kumbe ukweli ni kwamba alikuwa akifanya kazi na Mwananchi wa kawaida tu, yaani kama yeye.
*
Sudan ilikuwa nchi kubwa sana zaidi ya nilifikiria kabla.
Nilipomuuliza dada wa mapokezi katika hoteli ile, alinishangaa sana kwamba ilikuwaje nihitaji kuelekea Darfur na wakati mapigano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe yalikuwa yakiendelea huko?
Nilimtoa wasiwasi na kutaka kunipa maelekezo mengi kuhusu safari ya kwenda katika mji huo iana na kwenda katika mji huo ambao ulionekana kuwa tishio sana.
Dada yule akaanza kunielezea mambo mengi na hata umbali aliniambia kwamba kulikuwa na zaidi ya kilometa elfu nane kutoka katika jiji la Khatoum.
Umbali ule ukanishtua sana, sikutegemea kama kungekuwa na umbali wa namna ile. Hapo nilifikiria kupanda ndege, ila tatizo lililokuja ni kwamba hakukuwa na uwanja wowote wa ndege huko Darfur uliokuwa ukitumika katika kipindi hicho cha mapigano.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 15
Maneno ya dada yule yalinichosha kupita kawaida, ni mabasi tu ndio ambayo yalikuwa yakifanya safari ya kwenda huko kwa kutumia barabara ya lami ambayo ilikuwa ikiunganisha mpaka Kurdufan, kilometa mia tano kabla ya kuingia Darfur.
Niliporidhika na maelezo yake, nikarudi chumbani na kujiandaa na safari, asubuhi ya siku iliyofuata, safari ikaanza huku nikiwa pamoja na Majeed.
Ndani ya basi hatukuwa watu wengi, tulikuwa tumekaa katika viti vya nyuma kabisa.
Lugha ya Kiarabu ndio ambayo ilikuwa ikisikika ndani ya basi lile, sikuwa nikielewa kitu chochote kile lakini kila nilipotaka kuambiwa kile kilichokuwa kikiongelewa, Majeed alikuwa akiniambia.
Safari ilikuwa ni ya kuchosha sana, mizigo mingi ilikuwa imepakiwa ndani ya basi lile, kila basi lilipokuwa likisimama, hali ya hewa ilikuwa ikibadilika kabisa, ilikuwa ni ya joto kali sana.
Kichwa changu katika kipindi hicho kilikuwa kikifikiria kitu kimoja tu, kufika Darfur na kuanza kufanya kile ambacho kilikuwa kimenifanya kufika ndani ya nchi ile.
Dereva alikuwa akiendesha gari kwa kasi. Ndani ya gari hakukuwa na mtu yeyote aliyejali mwendo ule mkali, ni kama watu walionekana kutokuwa na habari, walikuwa wakiendelea kupiga stori kama kawaida. Ndani ya saa nane, tukawa tumefika Ad Duwaym, Kusini mwa Jiji la Khatoum.
Hapa kidogo ilikuwa ikinishangaza sana, Mji wa Darfur ulikuwa ukipatikana Magharibi mwa nchi ya Sudan, sasa ilikuwaje katika kipindi hicho tulikuwa tukielekea Kusini. Maswali hayo wala sikutaka kuyauliza, nilibaki nayo moyoni huku nikisubiri muda muafaka wa kuuliza utakapofika.
Kama ilivyokuwa Khatoum ndivyo ilivyokuwa hapo Ad Duwaym, kulikuwa na idadi kubwa ya watu huku magari mengi ya Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika yakiwa mahali hapo.
Hapo tukaruhusiwa kushuka na kuanza kununua vyakula. Hali ilikuwa ngumu sana kwangu, vyakula ambavyo vilipatikana hapo havikuwa sawa na mimi.
[22:31, 3/19/2019] +255 717 339 102: SEHEMU YA 16
Chakula ambacho nilihisi ningeweza kukila kilikuwa ni nyama ya ngamia tu, nyama tamu ambayo mara nyingi nilikuwa nikiila nchini Tanzania hasa katika kipindi cha Idd Al Hadji na El Fitri ambapo rafiki yangu, Ustadhi Maliki alipokuwa akituletea.
Baada ya nusu saa tukaingia ndani ya basi na kuendelea na safari yetu. Hakukuwa na safari ambayo ilikuwa inachosha kama ile.
Muda mwingi nilikuwa nikiiangalia saa yangu ya mkononi ambayo nilikuwa nimeiseti katika majira ya Sudan.
Safari iliendelea zaidi, sehemu kubwa ya nchi hiyo ilikuwa ni jangwa kubwa, tena jangwa lile ambalo lilikuwa na joto kali katika kipindi cha mchana.
Baada ya saa nane nyingine kupita, tukaingia katika Mji wa Kust na kuunganisha kuutafuta Mji wa Rabak ambapo hapo tungechukua barabara ya kuelekea Darfur.
Mchoko wa safari bado ulikuwa mkubwa mno, saa nne na robo usiku tukaingia Rabak ambapo hapo tulitakiwa kulala.
Usingizi haukupatikana hata kidogo, tulishinda usiku mzima tukipiga stori na Majeed ambaye hakuonekana kuwa na amani katika safari ile.
Bado niliendelea kumfariji na kumtoa hofu. Tulikula na kuendelea kupiga stori. Ilipofika saa kumi na mbili alfajiri, tukaanza tena safari ya kuelekea Darfur.
Hapo Rabak tuliwachukua abiria wengine waliokuwa wamefika na mabasi kutoka Sannar, Sanjar na Al Qadarif miji ambayo ilikuwa ikipatikana Mashariki mwa nchi ya Sudan.
Majeed ndiye ambaye alionekana kunichosha zaidi hasa mara baada ya kunitaarifu kwamba hata nusu ya safari tulikuwa hatujamaliza, tulisafiri kwa saa kumi na sita lakini cha ajabu eti hata nusu ya safari haikuwa imekwisha.
Safari ikaendelea zaidi, tayari nilionekana kukata tamaa ya kufika mapema, jua lilipochomoza mpaka kuwa la utosini ndipo tukafika Al Ubayyid. Hapo tukanunua chakula na kula tena.
Hali ya joto ilinisumbua, nilitamani kuvua shati langu lakini sikufanya hivyo kwa kutotaka kuonekana vibaya mbele za macho ya watu waliokuwa na asili ya Uarabu.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 17
Safari ikaendelea zaidi, saa tano na robo usiku ndipo tukaingia An Nunud, kilometa mia saba kabla ya kuingia Darfur. Nikatoka garini na kukaa nje.
Kila abiria alichoka, nilibaki nikiongea na Majeed kwa kipindi kirefu zaidi huku nikitaka kufahamu mengi kuhusiana na Darfur.
“Kwa hiyo nitajua vipi kama tumeingia Darfur?” nilimuuliza Majeed.
“Utajua tu.”
“Nitajua tu. Kivipi?” nilimuuliza.
“Swali lako litajibika kirahisi sana,” Majeed aliniambia.
“Sijakuelewa.”
“Kimuonekano. Utakavyouona muonekano, utajua tu kwamba tutakuwa tumeanza kuingia Darfur,” Majeed aliniambia.
Sikutaka kuuliza maswali mengine zaidi, kiu yangu ilikuwa ni kuanza kuona dalili hizo ambazo niliambiwa kwamba ningejua tu kwamba tulikuwa tumeingia Darfur.
Ilipofika asubuhi tukaanza safari. Katika kipindi hiki kulikuwa kumebaki vituo viwili vikubwa, cha kwanza kilikuwa Nyala na cha pili kilikuwa Al Fashir.
Hiki kituo cha Al Fashir kilikuwa ndani ya Darfur ila huku pembeni pembeni kabisa katika upande wa Kusini mwa Mji wa Darfur.
Hapo ndipo ungekuwa mwisho wa safari yetu, japokuwa katika kipindi hicho nilitaka kuelekea katika sehemu iliyo na mapigano zaidi ya Al Junaynah, lakini Majeed aliniambia kwamba basi lisingeweza kufika huko.
“Kwa nini?” nilimuuliza.
“Huko ndipo kwenye mapigano yenyewe, huko hakuna amani hata kidogo,” Majeed aliniambia.
“Safi sana. Uko ndipo pazuri, na huko ndipo nilipotaka kwenda,” nilimwambia Majeed ambaye alionekana kushtuka zaidi.
Safari iliendelea, abiria wengi waliishia hapo Al Ubayyid. Kipindi cha nyuma ndani ya basi tulikuwa zaidi ya watu sitini lakini katika kipindi hicho tulikuwa tumebakia watu kumi na sita tu, wengine walikuwa wamekwishashuka.
Safari haikuishia hapo iliendelea zaidi na zaidi mpaka tukaingia Nyala, kituo cha mwisho kabla ya kuingia kituo cha Al Fashir, mwisho wa safari ya basi lile.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 18
Safari ya kuelekea Al Fashir ikaanza. Hapa ningependa kuongea kitu kimoja kwa wale ambao waliweza kuongea mengi hata kabla safari ya kufika Darfur haikukamilika.
Darfur ndiyo mji mkubwa nchini Sudan na ndiyo maana mapigano yaliyokuwa yakiendelea huko yaliweza kuiathiri sana nchi hiyo.
Safari ya kuelekea katika mji mdogo wa Al Fashir ilikuwa ikiendelea. Hapa pia ningependa kuongea kitu kimoja ili kwa wale walioshangaa wasishangae tena.
Umbali wa kutoka Khatoum mpaka Darfur ilikuwa ni wa kilometa 8000 ila kilometa hizo ni mpaka pale ambapo unaingia katika Mji wa Nyala ambao upo Kusini mwa mji huo wa Darfur.
Umbali kutoka Khatoum mpaka hapo Nyala haukuwa ukipishana sana na umbali kutoka Nyala mpaka mwisho wa basi lile, Al Fashir.
Darfur ile ilikuwa kubwa sana, upana wake ulimshangaza kila mtu kiasi kwamba kuna wakati nchi ya Chad ikang’ang’ania kwamba Darfur ilikuwa ni sehemu ya nchi yao.
Darfur ilikuwa kubwa, eneo kubwa la Darfur lilikuwa jangwa kubwa, jangwa ambalo lilikuwa na joto kali katika kipindi cha mchana.
Umbali huo mkubwa ndio ukanifanya kupata majibu ya sababu ambayo ilimfanya dereva kuendesha gari kwa kasi kubwa zaidi ya magari ambayo yalikuwa yakisafiri katika ardhi ya Tanzania.
Nakumbuka nilikwishawahi kwenda Nairobi kwa kutumia mabasi ambayo yalikuwa yakikimbia sana, ila kwa mabasi yale ambayo yalikuwa yakisafiri kuelekea Darfur, mwendo wake ulikuwa ni mara mbili ya mabasi ya huku Tanzania.
Dereva alikanyaga mafuta hasa, muda mwingi nilikuwa na hofu lakini hakukuwa na mtu aliyehofu chochote kile, walionekana kuzoea.
Hapo ndipo ambapo safari ilionekana kuchosha sana, tulisafiri usiku na mchana na hatimaye kuingia Al Fashir, mji ambao basi lile lilikuwa limefikia mwisho.
Nikateremka na kumshukuru Mungu kwa kunifikisha salama katika ardhi ya Mji wa Al Fashir. Nilichokifanya ni kwenda kwenye kimgahawa kidogo na kupata chakula,
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 19
Kumbuka kwamba hapo tayari tuliingia katika mji wa Darfur ila hatukuwa tumefika katika sehemu ile ambayo ilikuwa na mapigano makubwa.
Baada ya kukaa mahali hapo kwa muda wa masaa mawili, ndipo tukaanza safari ya kuelekea sehemu iliyo na mapigano makali, Al Junaynah.
Usafiri haukuwa wa basi tena, madereva wengi walikuwa wakiogopa kuelekea huko kwa hiyo tulichokifanya ni kutumia usafiri wa farasi ambao ndiyo ulikuwa usafiri uliokuwa ukitumika katika kipindi hicho sehemu hiyo.
Katika safari ya kuelekea Al Junaynah hatukuwa peke yetu, tulikuwa na watu zaidi ya kumi ambao nao walikuwa wakielekea huko.
Farasi walikuwa wakikimbia kwa kasi kubwa, na kwa kutumia farasi hao huku tukipumzika katika sehemu mbalimbali hasa nyakati za usiku na pale ambapo farasi walipochoka, tuliweza kutumia siku sita na ndipo tukaanza kuingia katika Mji wa Al Junaynah.
Mpaka hapo wala sikutaka kuuliza zaidi kama tulikuwa tumeingia katika mji huo au la, magari mengi ya Umoja wa Mataifa yalionekana machoni mwetu, mara kwa mara walikuwa wakitusimamisha na kutuuliza baadhi ya maswali na waliporidhika na majibu yetu, tulikuwa tukiendelea na safari kama kawaida.
Tukafika katika sehemu ambayo wala haikuwa ikieleweka kabisa, macho yangu yakatua katika vitu vyeupe ambavyo nikashikwa na shauku kubwa ya kutaka kuvijua ni vitu gani.
Nilichokifanya ni kuanza kuwaambia wenzangu kwamba ilikuwa ni lazima nijue vitu vile vilikuwa ni nini. Watu wote walikataa lakini nilipowalazimisha zaidi, wakakubaliana nami.
Nikateremka juu ya farasi pamoja na Majeed na kuanza kuelekea kule ambapo kulikuwa na mchanga mwingi. Sikuamini kile ambacho nilikuwa nikikiona mahali pale, yalikuwa ni mafuvu ya watu.
Kwanza nikapigwa na mshtuko sana, toka nizaliwe sikuwahi kuyaona mafuvu ya watu, wakati huo ndio ilikuwa mara ya kwanza.
Kuna vitu vingine huwa tunavipuuzia sana kila tunavyoviona kwenye televisheni, ila ukweli ni kwamba vinatisha kupita kawaida. Mafuvu ya watu yanatisha sana.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 20
Nilichokifanya huku nikijivisha ujasiri, nikamwambia Majeed achukue kamera na kuanza kazi mahali hapo. Nikaanza kuongea huku Majeed akinirekodi, kwa kuniangalia harakahara, sikuonekana kuongea nikiwa na amani, lakini ukweli nilikuwa na hofu sana.
Kitendo changu cha kuyainamia mafuvu yale nilikiona kuwa cha ujasiri sana. Mafuvu ambayo yalikuwepo mahali pale yalikuwa ni mafuvu ya tofauti tofauti.
Kulikuwa na mafuvu ya watoto wadogo na pia kulikuwa na mafuvu ya watu wakubwa. Eneo hilo lilionekana kutokuwa na amani katika kipindi cha nyuma, kuna watu ambao waliteketezwa kwa kupigwa risasi mahali hapo.
Mafuvu yalikuwa mengi mahali hapo, kwa idadi ya haraka haraka ya kuhesabu huku nikiwa na hofu, yalikuwa yakifikia hata mia tatu. Watu wengine ambao tulikuwa tukisafiri pamoja katika farasi wale walibaki wakiniangalia katika kipindi hicho ambacho nilikuwa nikitengeneza makala yangu.
Tulikaa mahali pale kwa takribani dakika arobaini na tano na ndipo tukaendelea na safari yetu. Moyoni nilikuwa na majonzi makubwa, hofu ilizidi kuongezeka na kujua huko tulipokuwa tukienda ilikuwa ni hatari.
Nikaanza kujiuliza maswali mengi kwamba kama pale mwanzo wa kuingia Al Junaynah kulikuwa na mafuvu mengi kiasi kile, vipi huko katikati ya mji huo ambao mapigano yalikuwa makubwa zaidi? Kila nilichokuwa nikijiuliza nilikosa jibu kabisa.
NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA SEHEMU YA 21