Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JIJI LA KICHAWI SEHEMU YA 05

JIJI LA KICHAWI 5

SIMULIZI ZA JOSHUA / 8 months ago




JIJI LA KICHAWI

0713111547 whatsapp

``ok mpenzi wangu’’

``USIJE UKALOGWA UKAFANYA MAPENZI NA MWANAMKE MWINGINE POPOTE PALE SASA NYOOSHA MKONO WAKO’’

Msichana Yule wa kipepo alinyoosha mkono na kumvisha isaya pete ya kichawi ,pete isiyoonekana ‘’

Isaya hakuwa na kipingamizi alivaa pete ile ndani ya dakika moja binti Yule alitoweka

Isaya alijiketia chini na kuanza kulia .,alilia sana huku akijisemea

``bora ningemsikiliza sharifu balaa gani limenikuta daaaaah’’

Isaya hakuweza kulala tena alibaki macho mpaka asubuhi ilipofika asubuhi simu yake iliita

Alipoitizama aliona namba ya sharifu

``we mzee acha bata hujatosheka njoo chukua gari ‘’

``nakuja mzee baba ,nakuja sasa hivi’’

``ok’’

Isaya alijikongoja na kuanza kuondoka kuelekea kazini

Kazi ilianza isaya aliendelea kufanya ruti zake akiwa na daladala ,sharifu alikuwa akimtazama isaya tu toka asubuhi mpaka mchana ule ,hakuelewa hali ya mwenzake ,isaya alikuwa amenyongonyea sana akionekana kama mtu mwenye mawazo mengi,sharifu alivunja ukimya na kumuuliza mwenzake

``hey mzee leo kuna nini au kahaba kakuchosha kama hujazoea mapigo bob lazima u blow’’

``wapi mwanangu hamna ‘’

``nini shida sasa kama tatizo siyo hilo’’

``usijali mzee niko poa sana’’

Sharifu alipomwona isaya anakwepesha mada ,aliamua kumwachilia tu ila kiukweli hali ya isaya ila mshangaza sana …

Ilipofika jioni isaya alirudisha gari ,kisha alijipanga kurudi katika chumba chake alichopanga ,isaya alikuwa anawaza sana kurudi geto kwani vituko alivyokuwa akiviona kila siku vilikuwa vinamtesa sana na kumtisha

Isaya alifika mlangoni na kufungua mlango wake akiwa na hofu kubwa sana ,aliingia ndani na kuwasha redio yake kisha alielekea bafuni kuoga ,baada ya kuoga alijitupa ndani na kuanza kulala

Isaya alimwomba Mungu siku hiyo amwepushe na vioja ,kila siku toka afike pale hajawahi kulala bila usumbufu ,

Isaya alishangazwa sana na siku hiyo hakuamini kama imefika asubuhi bila ya chochote kibaya kutokea, isaya aliamka asubuhi na kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake ,alielekea kazini akiwa na furaha sana

Alipofika tu alikutana na sharifu ameshatia kambi

```oi oi oi oi niaje mzee baba’’

``vipi wewe mbona raha sana man’’

``raha lazima mkuu’’

Walichukua gari na tayari kuingizana mjini

Isaya alipofika stendi dada mmoja alimjia dirishani akiwa amebeba karanga na maandazi

``karanga karanga kaka chukua ‘’

Isaya alinunua karanga huku akimtazama binti huyo kwa matamanio makubwa sana

Binti Yule alikuwa mrembo na mwenye kuvutia sana ,isaya alijikuta akimwambia binti yule

``samahani dada jina lako nani’’

``naitwa ashura kaka yangu ‘’

``ohoooo ashura waweza ingia ndani ya gari tuongee’’

``sawa kaka usijali ‘’

Bila kipingamizi ashura alijepenyeza siti ya mbele alipo dereva


JE NINI KITAENDELEAAAAAAA

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.